Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Jukwaa la Wakristo Tanzania madai yenu kuhusu suala la ulinzi na usalama nawashauri muipate Katiba Inayopendekezwa na muisome kwa makini Katiba hiyo katika SURA YA 17 mtapata majibu mazuri ya wasiwasi wenu kuhusu usalama wa nchi.
Kuhusu suala la Muundo wa Serikali, wajameni SURA YA 7 ya Katiba Inayopendekezwa imeeleza wazi wazi juu ya Muundo wa Jamhuri ya Muungano katika IBARA YA 73.
Kuhusu masuala ya mauaji ya watu wenye ualbino, nadhani kila siku mnasikia wahusika wanavyokamatwa haswa waganga wa jadi pamoja na wauaji, lakini pia kuna kesi mbalimbali zinaendelea na nyingine zimeshatolewa hukumu kali.
Kuhusu kuwataka waumini wenu wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu mlizozitaja hapo mmechemsha, kwasababu msidhani kuwa waumini wote watafanya hivyo, nina amini wapo waumini wenye busara na wenye uelewa juu ya ukweli wa mambo mazuri yaliyoelezwa ndani ya Katiba Inayopendekezwa ambao hawatapoteza haki yao ya kufanya hivyo mlivyopanga.
Lakini pia hivi hamuoni kuwa mtakuwa mmemkosea Mwenyezi Mungu kwa kuwashinikiza waumini wenu waipinge Katiba hiyo? Kwani hata Biblia yenyewe inasema ya Kaisari mpeni Kaisari nay a Mungu mpeni Mungu, sasa udikteta huo mnaowafanyia waumini mmeupata wapi? Dini mnaiingiza na siasa tena jamanai? Tanzania ni nchi isiyokuwa na dini, kuweni makini msije mkaulizwa na Muumba wenu je kwanini mliwanyima haki waumini wenu katika Mamlaka ya Dunia. Kuwenu mfano wa mbele katika kuelimisha waumini badala ya kuwashinikiza waikatae. Huo sio uungwana kabisaaaaa!.