Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mbali na kutumia mitandao na makongamano au mikutano kudai Katiba Mpya, nashauri wanaharakati, wanasiasa na wadau wengine waandae vipeperushi vyenye kueleza umuhimu wa katiba mpya na kuvisambaza kadri inavyowezekana.
Vipeperushi vieleze mapungufu yaliyoko katika katiba ya sasa na hatari au athari zake kwa makundi mbalimbali katika jamii mfano wafugaji, wakulima,wafanyakazi n.k bila kusahau madhara yake kwa nchi nzima.
Vipeperushi vieleze mifano ya madhara tuliyopata kutokana na hii Katiba kama vile chaguzi za hovyo kama ule wa mwaka jana, madaraka makubwa ya Raisi kama kuvunjia watu nyumba Kimara lucha ya kuwa na zui la mahakama, n.k.
Mfano mwingine uwe ni watumishi wa umma kukaa miaka sita bila ya nyongeza ya mishahara ya kisheria ya kila mwaka enzi za Magufuli, n.k.
Vipeperushi yaliyotokea kwenye zao la korosho kulikotona na maagizo ya mtu mmoja mwenye madaraka makubwa, n.k.
Vipeperushi vigusie mauji,wizi,ufisadi na jinsi katiba hii inayowezesha watawala kuwalinda wahalifu wa vitendo hivi, n.k.
Kwa kifupi, yako mengi ya kuelezwa sambamba na kutaja faida tutazozipata kutokana na Katiba Mpya iwapo itapatikana
Vipeperushi visambazwe sokoni, misikitini, mashuleni, vyuoni, kwenye mabasi na daladala na sehemu nyingine zenye mikusanyiko.
Kwa kifupi, zitumike mbinu, njia na resource zote zilizopo katika mapambano haya ya kudai Katiba Mpya bila kuchoka.
Hakuna mjomba wala shangazi kutoka nje ataekuja kutusaidia katika mapambano haya, bali ni sisi watanzania wenyewe kwa umoja wetu.
Pamoja tutashinda.Itachukua muda gani, hiyo si hoja.
Penye nia, pana njia.
NB:Kudai Katiba Mpya, kusambaza vipeperushi vya aina hiyo, si kosa, bali ni kutekeleza na kuutumia uhuru wa Katiba hii tuliyonayo kivitendo zaidi.