Madai ya kulipwa fidia kwa usumbufu wanaonifanyia benki ya DTB

Madai ya kulipwa fidia kwa usumbufu wanaonifanyia benki ya DTB

Statics

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2017
Posts
394
Reaction score
1,015
Wakuu ,
Wiki iliyopita Ijumaa kwenye moja ya ATM ya DTB hapa mjini nilienda kutoa pesa laki moja...

Kilichotokea pesa haikutoka na kwenye account yangu wamekata pesa.. nikawafata customer care mda huohuo wakaniambia mtandao unasumbua pesa yako utarudishiwa baadae... hawakurudisha

Kesho yake Jumamosi nikawafata, wakanipa form ya kujaza ( ATM TRANSACTION QUERIES ), wakaniambia pesa nitarudishiwa baada ya masaa 48 ya kazi hivyo wakaniambia nije kufatilia Jumatano kama pesa haikurudishwa...

Jana Jumatano nilikwenda wakaniaminisha wataniwekea baadae siku hiyohiyo,, ila hawakuweka

Leo pia nimekwenda nikawakazia kwamba nataka waniwekee pesa yangu muda huohuo...

Matokea yake wamenikalisha masaa, mwishoni wananiambia nije kesho sijui report haikutumwa vizuri, mara sijui kuna vitu havijabalance..

Nimechoka na hizi porojo zao...

Hivi wakuu hakuna namna naweza kuwashitaki nilipwe fidia kwa usumbufu wanaonifanyia ?
Screenshot_20220818-171032_Messages.jpg
 
Back
Top Bottom