DOKEZO Madai ya matumizi mabaya ya kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Tarime

DOKEZO Madai ya matumizi mabaya ya kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Tarime

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna madai ya matumizi mabaya ya madaraka katika Shule ya Sekondari Tarime yanayohitaji uchunguzi wa mamlaka husika.

Inadaiwa kuwa Mkuu wa Shule alipendekeza mwalimu wa Fizikia ahamishiwe shule nyingine kwa madai kwamba utendaji wake darasani ulikuwa duni na alishindwa kumaliza mada. Hata hivyo, kinachozua maswali ni kwamba matokeo ya Kidato cha Sita ya mwaka 2026 katika somo la Fizikia yalikuwa mazuri. Aidha, muda mfupi baada ya shule kufunguliwa mwezi Julai, shule ilitangaza nafasi ya mwalimu wa muda wa somo hilo. Hali hii imeibua maswali kuhusu sababu halisi za uhamisho huo na iwapo Ofisi ya Elimu ilifanya uchunguzi wa kina kabla ya kufikia uamuzi huo au kama kulikuwa na maslahi binafsi.

Vilevile, kuna malalamiko kuhusu ukosefu wa uwazi katika usimamizi wa fedha za shule. Inadaiwa kuwa Mkuu wa Shule hasomi taarifa za mapato na matumizi kwa wadau. Kila mwanafunzi huchangia shilingi 60,000 kwa mwaka kwa ajili ya taaluma, lakini hakuna taarifa iliyowahi kutolewa kuhusu kiasi kilichokusanywa na namna fedha hizo zilivyotumika katika mwaka wa fedha 2025/26. Pia, kiasi cha fedha za ADA na Capitation kinachopokelewa na shule hakitangazwi kwenye mbao za matangazo kama inavyotarajiwa.

Wananchi na wadau wanaomba mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina kuhusu madai haya ili kubaini ukweli, kuwawajibisha watakaobainika na kurejesha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa shule.
 
Back
Top Bottom