Madai ya vifaa vya ujenzi kupanda bei: Mtaani kwako hali ikoje?

Madai ya vifaa vya ujenzi kupanda bei: Mtaani kwako hali ikoje?

Yaan ni balaa kubwa!
Kuna Tiles ndo usiseme
 
Bei ya nondo imepanda hadi kufikia 20,000 kwa mm 12 (DSM)
 
Bei zilizokuwepo mwezi june mwaka jana ukilinganisha na bei kuanzia dec.mpaka leo hii duuuuh ni hatari mfano cement ilikuwa 11500,mpaka 12000 leo hii 13500 simba cement na 14000 twiga unaweza kushangaa ukiamka imefika 15000
 
Huyu DANGOTE alikuja kwa mwembwe kweli tukadani ni mkombozi wa saruji sasa sijui kama anazalisha au azalishi na kama anazalisha anauza nchigani?
 
Mkuranga cement 14000 wakati kuna kiwanda cha rhino cement ndani ya wilaya
 
Kuna nini kinaendelea katika hii biashara ya vifaa vya ujenzi?

Mkuu hata Mimi sijafahamu bado !
Ila kiukweli kuna tatizo kubwa ktk vifaa vya ujenzi maana kila baada ya muda mfupi sana bei zinapanda!
Sijui wanajaribu kutaka kudiscourage watu wasijenge?!
Sasa maendeleo watayapima ktk vigezo gani ?!
Viwanja vyenyewe siku hizi kuwa navyo viwili vitatu ni shida maana itabidi kuvulipia kodi kila mwaka ambayo Mimi naina kuwa kubwa sana Kwa kweli! Ulipie ardhi na Kama kuna Nyumba kodi ya majengo pia!
 
Kodi Za viwanja wizara ya Ardhi wangeweka flat rate isiyozidi 10,000/- Walau watu wangeweza kuitikia na kulipa Kwa wakati na property tax vivyohivyo
 
Back
Top Bottom