Nafikiri ingekuwa vizuri tungeungana na waislamu ili serikali ishike adabu. Walimu, madaktari, mgomo wa wafanyakazi wote pamoja na wote tusioipenda serikali ya kifisadi iliyoko madarakani tungegomea sensa kuonyesha msisitizo.Tuungane kama watanzania kugomea sensa ikiwa ni ishara ya kuchukia kutekwa kwa raia mwenzetu Dr Ulimboka.:spy:
Watanzania wenzangu, tujaribu kuishi wa upendo, na tuepukane na tabia ya kujadili mambo kwa hisia. Leo hii tunanyoosheana vidole eti fulani hampendi fulani kwa sababu ni dini fulani. Wengine tunaitana majina kadha wa kadha… hawa washenzi, hawa magaidi nk.
Naomba niwakumbushe haya, kama mnajisahau mkafikiri kwamba duniani vurugu ni za wakristo na waislam peke yake:
Japan kuitokea mauaji ya kidini, hayakufanywa na wakristo wala waislam;
Wakati wa vita ya Yugoslavia ya zamani, waliouliwa na askari wa ki-Serb walikua ni Wakristo na Waislam
North Ireland, wala haikua dini moja dhidi ya nyingine, ilikua ni waprotestanti na wakatoliki
Iraq, wanaouawa wala wakristo, ni Shia vs Sunni. Somalia wala haijulikani tatizo ni nini haswa… kama ni madhehebu au misimamo…!
India wakati mwingine nako mara budists, mara hindus, mara muslims…!!
Tunajua yaliyotokea kwa wayahudi wakati wa Hitler
Andrey Bravic wa Norway, alishasema hataki watu wa imani za mashariki ya kati na mashariki ya mbali Norway.
Sasa, sisi Watanzania tunaodhani kwamba ni upande mmoja tu ndio una maumivu kuliko mwingine – kwamba ni upande mmoja tu ndio "umetendwa" au "umetenda"- halafu tunaamua kutukanana bila sababu za msingi, tufikiri mara mbili.
Au niweke hivi: Wewe mtanzania ambaye unadhani labda Wakristo wote hawawapendi waislamu; au Waislamu wote hawawapendi Wakristo - Unayedhani kwamba waliodhulumiwa duniani ni Waislam pekee, au Wakristo pekee - tafadhali, fikiria mara mbili.
Vitabu vyetu vinasema tuishi kwa upendo, cha muhimu kila mtu aabudu kwa salama.
Sasa kama wewe unasali kanisani, adhana haikuhusu; na wewe unayesali msikitini, kengele haikuhusu. By the way, ili wewe uabudu kwani ni lazima mwenzako apate au akose kitu Fulani? Kuabudu kwako wewe, ama kanisani, au msikitini, kunahusiana nini na imani ya mwenzio?
Sasa haya masuala ya nani wengi nani wachache ni kwa ajili ya nini haswa? Kama serikali ingekua inajenga makanisa au misikiti, sawa, lakini kama si hivyo, whether kipengele cha dini kwenye sense kiwepo au kisiwepo, nani ata athirika au ata faidika nini. Kikiwepo Wakristo wataathirika au watafaidika nini? kisipokuwepo Waislam watafaidika au wataathirika nini?
Haya, na nyie wengine mnaohangaika kuhesabu waajiriwa, or viongozi wangapi ni wa imani ipi, sababu ni nini haswa? Kwani dini ndio inapima uwezo? Wawe wa dini ipi, wala sio hoja, hoja ni uwezo wao - wakiwa wana dini au hawana, hiyo ni juu yao. After all, hivi tunaanzia wapi kuuliza dini za viongozi? Hili nalo ni tatizo - hua tunaangalia tu majina ya kiarabu na kizungu? halafu hizo hisia za kuanza kusema juma atakua muislam, na john atakua mkristo tunazitoa wapi? Kwa nini tusiwe na hisia tu kwamba juma au john ni watanzania.. basi!!
Hivi, ukiamka asubuhi ukaenda kazini, huko kote unapopita, unafikiri wanaokuhudumia wote ni dini yako peke yako? Hua unauliza dereva wa dala dala au kondakta au muuza chakula ni dini gani? Hua unauliza dini ya daktari anayekutibia au polisi anayekusaidia? Dereva texi anaye kuendesha? Mwalimu anayekufundisha? Wanajeshi wanaolinda nchi yako?
Kwa sisi tunaotoa matamshi ya kuudhi dhidi ya dini nyingine, hivi tunajisikiaje, baada ya kukashifu dini ya mwenzio mtandaoni, kesho asubuhi unamtolea tabasamu rafiki yako ambaye naye ana imani hiyo hiyo uliyoikashifu?
Kama kuna mtu kwenye nafsi yake anaona raha kuudidimiza upande mwingine, ajifikirie mara mbili, kwa sababu katika mazingira ya Tanzania, mitazamo hiyo haitotuacha salama, iwe inatoka makanisani au misikitini! Unaposema hupendi udini, badi na itoke moyoni, na kama huwezi fanya hivyo, fanya ibada zaidi. Vitabu vyote vinatuonyesha Bw Yesu na Mtume Mohammad walivyokua wakiishi kwa upendo licha ya kufanyiwa vitimbwi kadha wa kadha.
Labda nimalizie moja tu, haya yasiishie hapa – ukimuona kiongozi wako wa kiimani anatoa matamshi yanayokera kwa upande wa pili, basi na wewe uwe wa kwanza kumkosoa. Usimuonee aibu ati kwa sababu tu ni Sheikh wako, au Mchungaji wako, au Father wako.
Mungu ibariki Tanzania