Madaktari acheni kutuchanganya na hii kauli yenu tata ya Critical but Stable

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Sijui ni kwanini Madaktari wanapenda sana kusema kuwa Mgonjwa fulani yupo Critical but Stable lakini baadae ukija kuchunguza zaidi utakuta tayari huyo Mgonjwa ameshaonyesha dalili zote za Kukata roho / Kufa na mara nyingi wale Wagonjwa wengi ambao huwa tunaambiwa na Madaktari wetu kuwa wapo Critical but Stable huwa wanafariki dunia ndani ya ama muda mchache au siku chache tu zijazo.

Na kuna Daktari mmoja alinipa Siri kubwa ya wao kupenda kuitumia hii Kauli ya Critical but Stable kwamba huwa wanaitumia sana ili kuwaandaa Kisaikolojia wenye Mgonjwa wao ili hata baadae wakiwaambia ameshafariki basi wasiwe na mshtuko mkubwa lakini ukweli ni kwamba Kitabibu duniani kote hakuna kitu cha fulani ni Critical but Stable ila ukweli ni kwamba tayari huyo Mgonjwa anakuwa ameshafikia hatua ya mwisho kabisa ya kukata roho.

Sasa kama kumbe Mgonjwa kuwa Critical but Stable ni sawasawa tu na tayari ameshakata roho / amekufa nyie Madaktari huwa mnaogopa nini kutuambia Sisi tunaouguza kuwa Mpendwa Mgonjwa wetu ameshafariki dunia? Je hamuoni kwamba kuendelea kutuambia hii Kauli yenu ya Mgonjwa yupo Critical but Stable wakati kumbe ameshafariki dunia tayari mnatupa mzigo mwingine tu wa gharama na huenda mngesema tu ukweli mapema basi tungeokoa Pesa?

Kwa mfano Mimi binafsi nina Mgonjwa wangu Hospitali moja hapa Jijini ambaye alishambuliwa vibaya mno na Majambazi huku akiwa ameumizwa vibaya sana mkononi, mguuni, tumboni, kichwani na hadi wakaathiri na ini lake huku akiwa anapumulia mashine, lakini tokea tumkimbize hapo Hospitali leo ni siku kama si ya 15 basi ya 16 yupo ICU na hata haturuhusiwi kuingia kumuona ila ni Madaktari tu pekee ndiyo hutoka nje na kutupa taarifa zake za neno lao kubwa Kwetu sisi Wauguliwaji ni kwamba Mgonjwa wetu yupo Critical but Stable.

Madaktari acheni kutuchanganya tafadhalini huyu Critical but Stable anatutesa sana Sisi tunaouguza Wagonjwa wetu. Nawaomba pia Madaktari mliotukuka na mliopo humu JamiiForums mnipe ufafanuzi wa hii Kauli kwani inatuchanganya sana na hadi kuwafanya Ndugu, Jamaa na Marafiki zetu wengi wasijue la kufanya na huku wengine wasite pia hata kutaka kutoa msaada wao wa michango na huduma zingine kwa huyu Mgonjwa wetu Mpendwa ambaye ni Ndugu yangu aliyejeruhiwa vibaya sana na Majambazi huko Tarime Mkoani Mara ( Musoma ) akiwa anatoka Kazini na anaingia Nyumbani Kwake.

Nawasilisha.
 

Rudi shule.

Tumia akili.
 
Critical but Stable
 
mhhh kama sikuelewi kama unawish jambo baya litokee vile !haya !

Hoja yangu ni hiyo Kauli ya Critical but Stable tu na hakuna jingine tafadhali. Kwahiyo unataka kumaanisha kuwa Mimi GENTAMYCINE nina hamu huyu Mgonjwa wangu afariki dunia? Mkuu hebu tengua upesi kauli yako na nitake radhi sasa hivi.
 
Hoja yangu ni hiyo Kauli ya Critical but Stable tu na hakuna jingine tafadhali. Kwahiyo unataka kumaanisha kuwa Mimi GENTAMYCINE nina hamu huyu Mgonjwa wangu afariki dunia? Mkuu hebu tengua upesi kauli yako na nitake radhi sasa hivi.

Go back to school kama neno jepesi hivyo linakutoa kwenye reli.
 
GENTAMYCINE kama unavyojiita. Mungu akupe hekima...................................................... Na uendelee na hiyo shida yako. Lakini letu moja Lissu atapona na utashudhudia ukuu wa Mungu.....
 
Hivi mkuu wangu uliyetoa huu uzi, huwa unafikiria kwa kutumia kiungo gani cha mwili?
 
tangu jana huyu punguani analazimisha tumuamini kuwa eti Lissu atakufa hata baada ya miezi 3.

Nadhani aliyekuhifadhi tumboni mwake kwa miezi Kenda / Tisa Yeye ndiyo anaweza akawa Punguani mkubwa wa kunizidi. Hivi katika uzi wangu nimetaja mahala popote jina la Tundu Lissu? Kwahiyo GENTAMYCINE sina uhuru wangu na haki yangu ya kuhoji Jambo la Kitaalam na kupata ufafanuzi wake? Kwani ni Wagonjwa wangapi humu Mahospitalini huwa tunaambiwa na Madaktari kuwa wapo Critical but Stable?

Utundu Lissu katika huu uzi wangu umekukaje? Umepimaje kama Mimi siuguzi huyo Mgonjwa wangu? Naona unanitafuta Mkuu hivyo endelea tu utakipata unachokitafuta kutoka Kwangu kwani unaonekana unajifanya Kunijua sana halafu unawashwawashwa na Mimi.

Na nilitaka ufafanuzi wa Kitaalam na Kiueledi kabisa kutoka kwa Madaktari humu JF na sikuhitaji maoni ya Wapumbavu wachache wa mfano wako ambao akili zenu zote na muda wote zimekaa tu Kiitikadi za Kisiasa. Nauguliwa je ni dhambi kuhoji juu ya jambo fulani ambalo linanitatiza?

Uvumilivu wangu Kwako unaanza kufikia Kikomo.
 
Tasnia ya udaktari ni sawa na muuza ice cream.
Daima utapewa matumaini na kukufurahisha wewe unayemuuguza jamaa yako.

Hata Nyerere baba wa Taifa, Mwl. Nyerere, inajulikana alikata roho siku kama 7 kabla ya kutangaziwa kifo chake ili mipango yote iwekwe sawa kwa ajili ya kuhimili changamoto na mihemuko serikali na wananchi.

Ila hilo neno la critical but stable lilitumika sana. Though, kifo kikifika ndiyo hakuna zuio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…