Madaktari acheni kutuchanganya na hii kauli yenu tata ya Critical but Stable

Madaktari acheni kutuchanganya na hii kauli yenu tata ya Critical but Stable

Watu wanakaa ICU miezi mitatu nini hizi siku 14 tu. Critical but stable tuwaulize walioingia madarasani watueleze maana yake.
mimi nina mzee wangu alikaa kwa hiyo critical but stable akiwa ICU for about 3yrs na bado mpaka leo bado yuko not critical not stable lakini yuko hai unconscious for 10 yrs now
 
Sijui ni kwanini Madaktari wanapenda sana kusema kuwa Mgonjwa fulani yupo Critical but Stable lakini baadae ukija kuchunguza zaidi utakuta tayari huyo Mgonjwa ameshaonyesha dalili zote za Kukata roho / Kufa na mara nyingi wale Wagonjwa wengi ambao huwa tunaambiwa na Madaktari wetu kuwa wapo Critical but Stable huwa wanafariki dunia ndani ya ama muda mchache au siku chache tu zijazo.

Na kuna Daktari mmoja alinipa Siri kubwa ya wao kupenda kuitumia hii Kauli ya Critical but Stable kwamba huwa wanaitumia sana ili kuwaandaa Kisaikolojia wenye Mgonjwa wao ili hata baadae wakiwaambia ameshafariki basi wasiwe na mshtuko mkubwa lakini ukweli ni kwamba Kitabibu duniani kote hakuna kitu cha fulani ni Critical but Stable ila ukweli ni kwamba tayari huyo Mgonjwa anakuwa ameshafikia hatua ya mwisho kabisa ya kukata roho.

Sasa kama kumbe Mgonjwa kuwa Critical but Stable ni sawasawa tu na tayari ameshakata roho / amekufa nyie Madaktari huwa mnaogopa nini kutuambia Sisi tunaouguza kuwa Mpendwa Mgonjwa wetu ameshafariki dunia? Je hamuoni kwamba kuendelea kutuambia hii Kauli yenu ya Mgonjwa yupo Critical but Stable wakati kumbe ameshafariki dunia tayari mnatupa mzigo mwingine tu wa gharama na huenda mngesema tu ukweli mapema basi tungeokoa Pesa?

Kwa mfano Mimi binafsi nina Mgonjwa wangu Hospitali moja hapa Jijini ambaye alishambuliwa vibaya mno na Majambazi huku akiwa ameumizwa vibaya sana mkononi, mguuni, tumboni, kichwani na hadi wakaathiri na ini lake huku akiwa anapumulia mashine, lakini tokea tumkimbize hapo Hospitali leo ni siku kama si ya 15 basi ya 16 yupo ICU na hata haturuhusiwi kuingia kumuona ila ni Madaktari tu pekee ndiyo hutoka nje na kutupa taarifa zake za neno lao kubwa Kwetu sisi Wauguliwaji ni kwamba Mgonjwa wetu yupo Critical but Stable.

Madaktari acheni kutuchanganya tafadhalini huyu Critical but Stable anatutesa sana Sisi tunaouguza Wagonjwa wetu. Nawaomba pia Madaktari mliotukuka na mliopo humu JamiiForums mnipe ufafanuzi wa hii Kauli kwani inatuchanganya sana na hadi kuwafanya Ndugu, Jamaa na Marafiki zetu wengi wasijue la kufanya na huku wengine wasite pia hata kutaka kutoa msaada wao wa michango na huduma zingine kwa huyu Mgonjwa wetu Mpendwa ambaye ni Ndugu yangu aliyejeruhiwa vibaya sana na Majambazi huko Tarime Mkoani Mara ( Musoma ) akiwa anatoka Kazini na anaingia Nyumbani Kwake.

Nawasilisha.
Acha ujinga.

Unamuombea Lisu afe eehh!!
 
Wakuu acheni malumbano kwa maneno haya"critical but stable" kwa ufahamu wa kawaida mgonjwa hawezi kuwa CRITICAL at the same time awe STABLE, akiwa critical maana yake "he is fighting for his life" na akiwa stable maana yake "he is out of danger"
 
Back
Top Bottom