Madaktari Hospitali Binafsi Mnatulazimisha Magonjwa!

Omutwale

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2008
Posts
1,429
Reaction score
1,047
Suala la Hospitali Binafsi kuwaruzuku Madaktari Bingwa na Wa-kawaida kulingana na mapato au Bill ambazo wamesaini kwa mwaka/mwezi kunachangia ongezeko la sumu ya madawa kwa Wagonjwa na kunasababisha watu kujikusanyia magonjwa makubwa ya kudumu wakati wa matibabu. Saa nyingine katika kukuza bill hawa Madaktari wanasababisha wagonjwa kuchanganyikiwa.

Yamemkuta ndugu yangu wiki hii huko Dar. Jamaa alibaini uvimbe usio na maumivu mwilini mwake. Akaamua kwenda kuchunguza katika Hospitali binafsi yenye asili ya Kenya inayotoa hudumia za Bima ya Afya kwa mashirika mengi makubwa katika Mikoa ya Dar, Arusha na sasa wameingia Mwanza. Hapa akakutwa kila kitu kiko sawa. Walichofanya ni kuhakikisha mteja wao anafanya vipimo vya kila kifaa walichonacho kwenye Lab yao na mwisho wakampa magunia ya madawa japo walisema hakukutwa na ugonjwa wowote! Kampuni hii haina vifaa vya operation na uchunguzi mkubwa hivyo inapolazimika upate vipimo au huduma ya operation kubwa, wao hukupeleka kwenye Hospitali zingine. Wakifanya hivi, wao hulipa huko na hivyo hawapati faida sana. Mara nyingi unapoonekana hauna tatizo, hawawezi kukupa rufaa ya kwenda kufanya uchunguzi zaidi kwa watoa huduma wengine.

Jamaa yangu baada ya kupata majibu ya mtoa huduma ya Bima za afya wa kwanza akaamua kwenda kwenye hospitali nyingine binafsi ili alinganishe na awe na uhakika wa afya yake. Zamu hii akaenda katika moja ya Hospitali iliyo katika Mtandao wa Mahospitali makubwa sana katika ukanda wetu. Hospitali hii iko pembeni mwa ufukwe wa Bahari ya Hindi na barabara inayopita mbele yake Jumatatu ijayo itazawadiwa kwa Rais Barak Obama! Alipokutana na Daktari Bingwa kwenye hii hospitali akamuulezea hisia zake na vipimo alivyokwishapima. Daktari akamwambia lazima aanze upya. Vipimo vikachukuliwa, majibu yakaja sare na Hospitali ya kwanza. Daktari baada ya kuyasoma akamtaka afanye vipimo vingine zamu hii vikiwa ni vipimo vikubwa vikubwa. Navyo vikaja na majibu mazuri lakini kukawa na viashiria vya thyroid gland kutanuka. Mgonjwa akaambiwa atapingwa sindano kwenye shingo na pia afanye vipimo vingine vikiwemo vya vya cancer! Baada ya kupata mrejesho huu nikazama mtandaoni na nikajaribu kupata ushauri wa marafiki-Madaktari waliosoma enzi za Mwalimu. Nilichokifahamu na Waliponichambulia Madaktari wa zamani kimenistua sana. Biashara ya huduma ya afya sasa imevuka mipaka. Daktari bingwa anapombambikizia mteja vipimo vikubwa, magonjwa sugu na matibabu feki haina tofauti na askari anayembambikia mwananchi kesi! Ingekuwa amri yangu, afya na elimu zingekuwa huduma za Kikatiba, zingetolewa bure na zingetolewa na hospitali za umma tu. Sekta binafsi isingeruhusiwa kabisa kutoa huduma hizi.
 
Aiisee mkuu umenena kitu cha ukweli,hii kitu inagharimu afya zetu na kutishia uhai wetu.
 
Omutwale una hoja kabisa hapa....ila nina shaka kama serikali ingeweza kubeba mzigo huu kama hatujatua kwanza mzigo wa ufisadi ili pesa za kufanya vipimo genuine na kuwalipa hao wataalam na kununua vifaa tiba zipatikane!
 
Last edited by a moderator:
Biashara kwenye huduma muhimu ni janga na kifo!! Ilinitokea last month Morogoro, nikiwa mapumzikoni nikajichoma na mti kichwani damu zikatoka na kidonda kidogo kikawepo nikaenda hospital. kufunga kidonda na sindano ya kuzuia tetenasi ilinitoka 40000Tsh. Hio ni hospital binafsi! Nilijua tu hapa nimefanyiwa biashara nikawa najiuliza inakuaje kwa maralia Kali au mguu uvunjike kwa Mtu asie na kipato si mauti inamkuta!? Naungana na wewe kuna ulanguzi mkubwa kwenye Afya hii biashara iangaliwe vzr na serikali vinginevo watu wataendelea kubebeshwa magonjwa na gharama ZisiZo stahili!
 
Omutwale una hoja kabisa hapa....ila nina shaka kama serikali ingeweza kubeba mzigo huu kama hatujatua kwanza mzigo wa ufisadi ili pesa za kufanya vipimo genuine na kuwalipa hao wataalam na kununua vifaa tiba zipatikane!

Hivi serikali yetu inaweza nini na nini majukumu yake basi? Biashara sawa imebinafsisha. Huduma za jamii nazo partially zimebinafsishwa na zilizobaki mikononi mwake ni sawa na hazipo. Elimu mashuleni na vyuoni vimegeuka nyenzo za kuzalisha wajinga, Ulinzi na Usalama wa raia nao sasa ni mateso na mauti ya wananchi. Kukusanya kodi nako haifanyi ipasavyo na badala yake inakamua vidagaa. Sasa basi nini sababu ya kuwa nayo?

Nakuhakikishia tungekuwa na Serikali imara, kodi zetu zingetosha kabisa na kubaki ziada ya kufadhili utoaji wa huduma bora za Jamii zingine. Angalia huu mfano halisi; Tanzania ilikuwa ya kwanza miongoni mwa nchi za Afrika kuunda mfuko wa bima ya afya. Nchi kama Rwanda imekopi mpango wetu miaka kama mitatu tu iliyopita lakini leo hii coverage yake ni 75% ya Wananchi wake wakati sisi waasisi wa huo mfuko tuko below 25% ya population! Rwanda wana rasilimali gani za kuidhihaki Tanzania kiasi hiki?
 
Safi kabisa.
Wakati ule madaktari wamegoma na kudai haki zao tulikuwa tunawanyooshea vidole na kujifanya kusimama upande mmoja na serikali.
Sasa madaktari wameamua kuwa wajasiriamali
hakuna mgomo,ni kuchakachua kwenda mbele.
Sasa ni zamu yetu kupiga kelele juu ya madaktari,sijui hii serikali tuliyokuwa pamoja nayo wakati wa mgomo, iko pamoja nasi au imeamua kukaa kimya ikishirikiana na madaktari.
 
Wapo waliosimama kufa na kupona na serikali na wapo pia waliokubali kuwatetea madaktari kikamilifu. Mimi nilisimama na kundi la pili.

Rafiki Maubero tusiwe kama panya aliyefurahi kwamba paka kamkuta kanisani anasali na hivyo hatamla! Usiombe zamu yako ifike upate mgonjwa au wewe mwenyewe uugue. Kama huna pesa au bima ya afya, kicheko chako cha leo kitageuka kilio cha kusaga meno
 
Yameshanikuta!
na nimejifunza jinsi ya ku-handle situation za namna hii.
Usidhani kwamba nafurahia haya yaliyotokea, ila ushabiki wetu wa kisiasa ndiyo utakaondelea kutugharimu kila siku.
Wakati ule wa mgomo wa madaktari hata wananchi walitakiwa kuandamana ili kuishinikiza serikali yao kuboresha huduma za afya, lakini matokeo yalikuwa tofauti, wengine tuliwalaani madaktari, na wapo walioshinikiza madaktari waende kumuomba msamaha Rais.
Simchekli mtu ila kulalamika hatutatusaidia chochote bila kuchukua hatua.
 
Omitwale!
Hayo yote uliyosema ni sahihi sana. Kuanzia zahanati za mitaani hadi Hospitali binafsi, sera zao ni kupata faida zaidi bila kujali maslahi ya mgonjwa. Mapungufu makubwa yapo katika usimamizi; HAKUNA. Kila mmoja anafanya atakavyo ili kujilimbikizia faida na kuwaumiza Wagonjwa kwa kuwabambikia bili kubwa na kuwapa madawa wasio yahitaji.
Mimi nina mfano mwingine.
Kuna Mama mjamzito alianza kliniki katika Hospitali binafsi akiwa na Ujauzito wa miezi 6. Baada ya kufanyiwa Ultra Sound scan ya kwanza majibu aliyopewa ni kuwa ana Placenta Previa hivyo inabidi aonane na Madaktari Bingwa tu"Specialisty" na Itabidi azalishwe kwa upasuaji; Yule Mama alipata hofu na akapata shinikizo na Damu (HBP). Lakini alipopata ushauri aonane na Daktari mwingine na vipimo vingine, akaenda kuonana na Daktari mwingine Mwananyamala Hospitali akaonekana ujauzito wake ni wa kawaida na hatimaye akajifungua salama kwa njia ya kawaida.
Hii ndio Bongo!!!
 
na watu wameipuuza hii mada sana ingekuwa ya wakina nchemba zingekuwa kurasa 200
 
hili suala nilikuwa nalijadili na familia yangu jana jioni ,naenda kupima malaria na dawa 15,000/= hahaahahahah
 
na watu wameipuuza hii mada sana ingekuwa ya wakina nchemba zingekuwa kurasa 200
Wacha tuangamie. Mtu asiyejua haki yake, hawezi kuipigania.
 
Au nafikiri kungeanzishwa vituo vya upimaji tu (maabara), na huko leseni zake ziwe na kutoa huduma ya kupima tu nafikiri
hili tatizo lingepungua.

Hii ishu umekuwa kubwa sana, kuna ndugu yangu alitiwa msukosuko na haya mahospitali binafsi mpaka wakafikia hatua ya kuambia ana tatizo kubwa kwenye figo na ini kumbe ni typhoid tu.....alipotibiwa mpaka leo yuko buheri wa afya.
 
Wakati wa mgomo wa madaktari nilieleza wazi umuhimu wa kuwaunga mkono....Hivi mashine ya CT scan inauzwa shilingi ngapi hadi serikali ishindwe kununua hata kwenye hospital kama Muhimbili ila Regency na Agha Khan zipo????????????? Kuna mchezo tunafanyiwa na viongozi wetu ndg watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…