Madaktari mnapotuandikia dawa semeni kama inaendana au haendani na vitu vingine mfano pombe

Madaktari mnapotuandikia dawa semeni kama inaendana au haendani na vitu vingine mfano pombe

dyuteromaikota

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
5,929
Reaction score
8,327
Kuna pisi moja ya ukweli sana imepotea. Naskia ilichanganya pombe na dawa. Kwa nini hamsemi? Mnafurahi mtu akifa?

Haya ninyi madaktari mliomo humu hebu tusaidieni orodha ya dawa ambazo haziendani na pombe.

Msisubiri watu wafe ndo mjifanye kusikitika.

Ahsante.
 
unapaswa nawe usome maelekezo,mara nyingi nimepewa dawa nikasoma maelekezo yake zina mengi kuliko niliyoambiwa na daktari
 
Aah swala la kugida vipogo nikiwa natumia dawa nishakataza kabisa

Ikiwezekana acha kabisa kunywa pombe ukiwa unatumia dawa kwa matokeo mazuri zaidi
 
Dawa nyingi mara nyingi hazitakiwi utumie pamoja na pombe. Kwani ukiacha pombe mpaka umalizie dozi kuna shida gani. Pombe sio chakula kwamba Ukiacha urakufa
 
Dawa nyingi mara nyingi hazitakiwi utumie pamoja na pombe. Kwani ukiacha pombe mpaka umalizie dozi kuna shida gani. Pombe sio chakula kwamba Ukiacha urakufa
Doz zingine zinatumiwa hata miez m3 mkuu
 
Tangu siku ilipotaka kumuondoa mke wa jirani yangu aliyedanganywa baada ya masaa 6 inakuwa haina nguvu wala sidanganyiki eeeh!
Hilo nalo tatizo, kuna dawa unamaliza dozi wanakwambia ukae wiki mbele ndo uanze kula gambe
 
Hiyo itakuwa dawa gani tena au alichanganya flagyl na pombe nasikia huwa inaua
 
Hakuna dawa ambayo ukichanhanya na Pombe haitakuletea shida ila tu Utofauti upo kwenye madhara yake na ukubwa wake.. Kuna dawa kama Metronidazole na dawa za jamii hii ukinywa na Pombe umeishaaa. Zingine zitakupa changamoto tu ambazo zinaweza zisiwe mbaya.

SABABU KUBWA NI
Kila dawa huwa inachakatwa kwenye Ini ili iweze kufika hatua ya kutolewa nje lakini Pombe pia huchakatwa na maini so endapo Umekunywa pombe na dawa Ini linaweza kuchaka pombe itoke kwanza na kuacha dawa inazidi kuaccumulate ndani ya damu au zile product za dawa mpaka kufikia kiasi cha kuleta shida. USINYWE POMBE NA DAWA.
 
Back
Top Bottom