Tatizo la Madaktari ni kama la wabunge; Wala haina ubishi.
Kosa kubwa hapa ni la ubaguzi kama alivyosema Nyerere. Hebu fikiria Daktari mwenye Digrii moja na mhasibu wenye digrii moja eti Dr. 960,000 harafu mhasibu 300,000/-TZS. Makosa haya yamefanyika na serikali na sasa yanawatesa. Tumesome tulichosome kwa vile ni interest tu, sio kwamba daktari aliombwa na watz asome vile yeye anaakili sana, no ni mgawanyiko tu wa kazi ili wengine tufanye kazi zingine, sasa isije ikawa wanadhani ni bora kuliko kila mtu, hakuna. Wote tupo sawa, kama umesoma udaktari ni vile ulipenda, kama nimesoma uhasibu, kompyuta, uhandishi au fani yoyote ni vile tumependa wenyewe sio ombi la waTZ au serikali.
Sikubaliani kabisa na madaktari wa TZ, wanapenda masilahi kuliko hata kuchambua hali ya uchumi wa nchi ukoje, kwanza wangejiunga kukomboa uchumi, kudai vifaa bora vya matibabu na hali nzuri kwa wagonjwa ndipo waongelee mishahara na maposho yao; mbona tangu nipate akili sijawahi sikia dr. amegome kwa vile kina mama wanalala wawili kitanda kimoja, amegome vile hospitali hakuna vifaa vya kisasa, amegoma vile hospitali zipo chake angependa huduma ifike vijiji??? wao ndo wakwanza kutotaka kwenda hata vijijini.
Madaktari ni wataluma wa kwanza kuonesha kuwa wali ni limbukeni kwelikweli; Kwa kuungana na wabunge kudai posho zaidi ya % 100 pamoja na nyongeza ya mshahara kutoka 960,000/- hadi 3,500,000/- hivi hawa madaktari walisoma hata hesabu zile za BAM wakajua hizo % ni ngapi, je kada zingine nazo wakigoma nchi itakuwaje au tukitaka hilo ongezeko itakuwaje.
Nawasihi madaktari kama wanania ya dhati, basi tuungane kupinga posho za wabunge na sio kudai kama wabunge.