mimi ni kijana ambaye nina miaka 39! tatizo langu ni kwamba joint za vidole vya miguuni na mikononi pamoja na vidole vyenyewe vinaniuma sana kama vile nimekimbia sana na kufanya mazoezi na ninakua mchovu sana hasa usiku nikilala! tangu hali hii inianze ninashindwa hata kumridhisha mke wangu kwan nguvu zinakua hazipo, lakin hamu ya kufanya mapenzi ninakua nayo.naombeni msaada wenu ninateseka sana hata kazi za kunipatia mlo wa kila siku nashindwa kufanya kwa ukamilifu kutokana na tatizo hili.