A
Anonymous
Guest
Mimi ni daktari tarajali (intern doctor) katika Morogoro Regional Hospital, na tunakumbana na changamoto kubwa ya kutolipwa posho zetu kwa wakati. Hadi sasa tumekaa takribani miezi miwili bila malipo, jambo linalotuweka kwenye hali ngumu ya maisha.
Hakuna malipo ya extra duty, hakuna nyumba za kuishi, na wengi wetu tunalazimika kutumia nauli binafsi pamoja na kulipa kodi za nyumba. Pamoja na gharama hizi zote, bado posho hazitolewi kwa wakati, hali inayotuathiri kiuchumi na hata katika utendaji wetu wa kazi.
Tunaendelea kuhudumia wagonjwa kwa kujitolea, lakini hali hii si endelevu. Tunaomba mamlaka husika ziangalie suala hili kwa haraka ili kuhakikisha haki na ustawi wa madaktari tarajali unalindwa.