Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 70
Leo katika gazeti la Mwananchi , kuna taarifa ya Makamu wa Rais wa Chama cha madaktari Tanzania (MAT), Primus Saidia kwamba Majibu toka kwa mwakilishi wa ofisi ya Waziri Mkuu yamewakatisha tamaa. Aidha kuna taarifa kwamba huduma katika hospitali ya muhimbili imedorora na kwamba kuna dalili kwamba kuna uwezekano wa kuwepo mgomo siku ya Jumatatu yaani kesho.
Pamoja na taarifa hiyo ya Dk Saidia , sikuona aya iliyotamka majibu walioyapata toka kwa Waziri Mkuu. Je majibu hayo ni siri?
Najiuliza swali hilo kwa vile ninakuwa na wasiwasi sana kwamba, isije ikawa Madaktari nao wanalihusisha tatizo hilo na mambo ya siasa na kujisahau kwamba wao ni wataalamu. Watuambie ni majibu gani wamepewa toka ofisi ya waziri Mkuu ili watanzania tujue ukweli. Mimi naamini Serikali inatambua umuhimu watumishi wake wote na siyo Madaktari pekee. Busara zaidi zinahitajika toka kwa wataalam wetu hawa. Wapime, wakumbuke pia kuwa Serikali haijishughulishi na Madaktari tu. Ni wazi kabisa kwamba madai yao ni halali, lakini kutokana na ukweli kwamba siyo wao peke yao wanaohitaji kuhudumiwa na Serikali , wanaowajibu wa kuangalia ukweli wa viwango wanavyovidai kwa kutambua kwamba ni watumishi wa umma kama watumishi wengine kama mwalimu, mhandisi, askari na wengine wengi. Zaidi wajiulize na kutafakari juu ya nafasi zao na jinsi ambavyo sasa wagonjwa wanapata shida pale. Muhimbili.