MADAKTARI: Vipimo vya UTI kama ni hivi ni balaa

Kwani chief ,maabara wanaripoti kwamba patient ana UTI ? Or wanaripoti presence of pus cells in urine na ku-quantify only?

Nan humwambia patient ana UTI?

Mimi nafikiri kote kuna matatizo .....msomaji na mtafsiri wa majibu.
Chukulia mfano,
Urinalysis ripoti ambayo iko mfano wa picha hapo chini (zingatia leucocyte esterase + nitrite).

Most likely daktari ata suspect mgonjwa yuko na UTI. Kwa hospital ambazo hazina uwezo wa kufanya urine culture & sensitivity, daktari atafanya empirical treatment kwa kuprescribe antibiotic ampe mgonjwa.

Kama hayo majibu kila kitu kingekua normal, daktari asingetoa antibiotic ya aina yoyote kumpa mgonjwa.

Daktari hawezi kususpect UTI kwa kumuangalia mgonjwa kwa macho, lazima kuwe na report flani kutoka maabara itakayompa alert kwamba huyu mgonjwa kwa ripoti hii ya mkojo anaweza kuwa na UTI ndio maana wakati anamsikiliza mgonjwa mwanzo hakumpa dawa za UTI ila akasema nenda lab kapime urine. Ripoti ilipokuja alipoiona ndio akaandika dawa.

Kama mtaalamu wa maabara kafanya makosa katoa ripoti fyongo basi itaharibu mlolongo mzima wa matibabu.
 
Kila anayekwenda zahanati binafsi kama ana homa ni lazima ataambiwa ana UTI au malaria tena katika malaria wanaongezea na msemo wa malaria ringi 5 au ringi 7 😂nilimsikia aliyekuwa naibu waziri wa afya mbunge wa kigamboni alipokuwa akihojiwa kipindi hicho akiwa bado ni naibu waziri , alisema kwanza katika vipimo vya malaria hakuna kitu kinaitwa Ringi !! Na pia haiwezekani kipimo cha UTI kipatikane siku hiyo hiyo ulipopeleka mkojo !! Ni lazima vile vimelea vioteshwe kitaalamu ndio majibu yapatikane labda mpaka baada ya masaa 36 kwa uchache!! Hatari sana !!
 
1. Kwanza ieleweke hakuna ‘Daktari wa maabara’ bali kuna ‘mteknolojia maabara’
2. Kuna ombwe kubwa la maarifa na elimu kwa wataalamu wetu. Kwa maana ya madaktari, tabibu na wataalamu wa maabara. Kiufupi elimu yetu katika kuwaandaa wataalamu hawa kwasasa ipo chini.

3. ‘Conflict of Interest’ kati ya dhumuni la kituo (kuingiza mapato) vs taaluma.
4. Ujuaji wa wagonjwa hata wakipewa ushauri katika matatizo yao. Wengi siku hizi wamekuwa wabishi hususani wakirelate dalili zao na vile walivyoona mtandaoni. Huwalazimishi madaktari kufanya kile wanachokijua wao na sio anachokijua daktari.
 
Kwa anaefahamu kipimo cha hepatitis B kinachukua muda gani, Maana rafiki yangu alipewa majibu baada ya dkk 20 nikashangaa.
 
Kwa anaefahamu kipimo cha hepatitis B kinachukua muda gani, Maana rafiki yangu alipewa majibu baada ya dkk 20 nikashangaa.
Hepatitis B ipi alipima

Hepatitis B surface antigen?
Hepatitis B surface antibody?
Hep B core antigen/antibody?
Hep B viral load?
.
.
 
Me mwenyewe Kila nikienda hospital kupima.nikipima mkojo lazima niambiwe Nina UTI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…