Katika hali inayotia hamasa katika elimu ya Tanzania wakati wakenya wakiendelea kubeza elimu ya Tanzania ,watanzania wajivunia elimu yao na kufanya maajabu
Madaktari Tanzania wafanya upasuaji wa kihistoria
Saa 4 zilizopita
Mshirikishe mwenzako
ImageMadaktari wamewafanyia upasuaji wagonjwa wawili
Madaktari wa Tanzania katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakishirikiana na wenzao wa India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa moyo wa aina yake Tanzania.
Upasuaji huo ujulikanao kama ‘bypass surgery’ ulishirikisha kupandikizwa kwa mishipa ya damu kutoka sehemu nyingine ya mwili moyoni bila kutumia mashine ya kusimamisha moyo na mapafu.
Kwa kawaida madaktari wanasema upasuaji wa moyo hufanyika baada ya moyo na mapafu kusimama, lakini upasuaji huo ulifanyika wakati moyo na mapafu vikifanya kazi.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa Bashir Nyangasa ameambia BBC kuwa upasuaji huo wa kupandikiza mishipa ya damu nje ya mshine ni wa kihistoria nchini Tanzania.
“Mgonjwa anaweza kutolewa mishipa ya damu kutoka miguuni au mikononi baada ya kupewa dawa ya usingizi na mishipa hiyo kupandikizwa kwenye mshipa wa moyo uliokuwa umeziba ili kuruhusu mzunguko wa damu wa moyo kama kawaida bila kutumia mashine,” amesema.
Upasuaji huo wa moyo kwa njia ya kupandikiza umefanyika kwa watu wawili, ambao umeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa hali zao zinaendelea vizuri .
Dkt Nyangasa amesema kwa sasa hakuna haja ya Watanzania wenye matatizo ya moyo kwenda nje ya nchi kwa kuwa wao kama wataalam wameweza kufanya upasuaji huo.
Anasema madaktari sasa wanaweza kuhudumia wagonjwa wengi zaidi wenye uhitaji na kupunguza gharama kwa serikali ya kusafirisha wagonjwa wa moyo nje ya nchi.
Mwandishi wa BBC aliyepo Dar es Salaam Esther Namuhisa anasema wengi wa wagonjwa wamekuwa wakisafiri hadi India ambapo wengi hukumbana na changamoto nyingi kupata huduma hiyo kifedha na hata kwenye upande wa lugha.
Source BBC SWAHILIView attachment 350990View attachment 350991
Jamani, naomba sana Watanzania acheni tabia ya kukimbila media ili kupata sifa.
Sijafahamu ni technolojia gani inayotoa assurance ya successful operation kabla hata mtu hajapata fahamu.
Lakini kingine, hakuna asiyejua ubingwa wa wahindi. Ninaona kwenye picha anayefanya procedures hapo ni kama mtu wa rangi. Au ndiye nyangasa? Wengine nawaona wanachunguilia kwa mbali ingawa wako kwenye plicha kama vile wanashuhudia. Tunajuaje wamefanya wao au walikuwa wanaonyeshwa inavyokuwaga?
Ninakumbuka uchunguliaji wa Ngeleja wakati akiwa kwenye msafara na vasco da gama eti kuonyesha naye alikuwa kwenye msfara wa raisi ulaya. Yasie kuwa yanajirudia.
Ninaobma mtotot apone, waendelee kufanya hizo operations bila ulazlima wa kuwa na wahindi, ndipo tushangilie .Kwa sasa tunaona ni wale wanaompa mgonjwa wa diabetes glucose halfu wanabadki wametoa mimacho na stethoscope kama wacheza sinema.
Tunaombea sana mabadiliko huduma za afya TAnzania na ndiyo sabbu tunahtaji waganga wetu wawe serious pamoja na serikali iwakumbuke Watnzania wanaokufa kama kuku wa kideli kwa kukosa huduma za afya. Usaanii wa kukimbila kwenye media kwa masuala ambayo hawajafanya wao, waache. Seriakli haiwezi kuwarubni wananchi kwa kutumia sinema na maigizo hatika kila jambo. La afya halpana. Tunahitaji uhalisia na ambao hauhitaji kupigiwa debe maana kila mtu atafahamu tu.