Digirii za kuhenya:
Kuna wenye shahada kutoka vyuo stahiki (k.m., PhD, MD, DDS, DPT, JD, n.k.) ambao wanastahili kuheshimiwa kwa kuitwa ma-Dr. Kama chuo alichopatia hii shahada kina utata basi tuchunguze lakini anastahili kupewa
title yake mpaka hapo tutakapothibitisha kuwa hastahili.
Digirii za kutunukiwa (heshma):
Sasa kuna hizi digrii za kutunukiwa kama Ph.D.
honoris causa (latin: for the sake of the honor). Hizi shahada za heshima zinatolewa na vyuo vikuu kwa mtu katika kutambua mchango wa kazi yake maishani. Hii shahada ina uzito sawa na ile aliohenyea mtu kwa kufanya research, kuandika desertation, na kui-defend kwenye kamati yake. Hivyo basi mtu aliepewa Ph.D.
honoris causa anastahili kuitwa Dr.
Dr. Kikwete, Dr. Mengi, late Dr. Nyerere wote wanastahili kupewa heshima hiyo. Wengi wanaopewa hizi Ph.D.
honoris causa hawapendi kuitwa hadharani Dr. kama alivyokuwa mwalimu Nyerere. Lakini mara nyingi hii michango inayomfanya mtu apewe
honorary degree ni mikubwa sana kuliko hata a simple written desertation ilioandikwa kwa miaka 3 au 4. (my humble opinion, as a holder of a non-honorary Ph.D.)
Nani mwengine ni Dr.?
Katika safu yangu, wa kwanza kuitwa Dr. ni marehemu babu yangu aliekuwa mganga mashuhuri sana wa kienyeji kijijini kwetu who never saw the inside of a formal classroom. Watu wote wengine wanaotoa michango au ushauri mzuri kama ya
tiba mbadala (
Dr. MziziMkavu),
mapenzi/mahusiano (
Dr. Love - hivi nani hapa JF anapaswa kupewa hii heshima?), n.k. Kwa maoni yangu mtu yeyote anaejihisi ana ujuzi zamilifu kwenye fani yake anaweza tu kujiita Dr. Udaktari uchwara utajulikana haraka sana.
Nawasilisha.