Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Kabisa, ikipostiwa nyumba moja, say inauzwa milioni 50, madalali wote wanaiposti , kila mmoja anaweka bei yake, wa mwisho anaweka milioni 100.Madalali ni watu ambao hawana professionalism lakini ndio wanao run real estate ya bongo.
Well saidKosa hapo ni wizara ha ardhi wameshindwa kuwasimamia hao madalali.Wizara hii inauozo sana.nina mwaka wa nane nabangaikia tu hati na sijapata
Achani ubinafsi kwa hiyo hamtaki watu wenye vipato vya chini wapate sehemu za kujihifadhi na familia zao??MADALALI ndio wavunjifu wakuu wa sheria , makampuni ya kuuza viwanja wamekwenda mpaka huko kigamboni puna becha , mbuutu na kigamboni nzima wameikata viwanja vya 20 kwa 20, serikali inatoa hati , sasa hapa waziri anaongea nin na watendaji wake wanafanya nini?
Kujenga nyumba kwenye kiwanja cha mita 20 kwa 20 (kinachotoa jumla ya mita za mraba 400 - 400 SQM) kuna changamoto zake kitaalamu. Serikali ya Tanzania ilipiga marufuku upimaji na uuzaji wa viwanja vya uwiano wa 1:1 kama 20 kwa 20, ikisisitiza kuwa kitaalamu viwanja vinatakiwa kuwa na uwiano wa urefu na upana wa kuanzia 1:2 hadi 1:2.5 (kama mita 16 kwa 25).
Hapa kuna ufafanuzi wa kina kuhusu hasara za kiwanja hiki, msimamo wa sheria, na sababu zinazofanya watu waendelee kupata vibali au kujenga kwenye maeneo hayo.
Hasara za Kujenga Kwenye Kiwanja cha 20 kwa 20 Ingawa mita za mraba 400 (400 SQM) zinatosha kutoa nyumba nzuri ya familia ya vyumba 3, muundo wake wa mraba uliosawa (Square) unaleta changamoto zifuatazo:
Kuvunjwa kwa Sheria za Nafasi (Setbacks): Sheria za ujenzi Tanzania zinataka uache umbali wa mita 3 kutoka kwenye njia/barabara na mita 1.5 hadi mita 2 pande za majirani. Ukitoa mita hizi pande zote nne za kiwanja cha 20x20, eneo linalobaki katikati la kujengea linakuwa finyu sana, jambo linalowalazimu watu wengi kusogeza nyumba hadi mpakani mwa majirani na kuhatarisha usalama wa moto.
Kukosekana kwa Faragha (Privacy): Kwa sababu kiwanja hakina urefu wa kutosha kurudisha nyumba nyuma, madirisha yako na ya jirani yanakuwa karibu mno. Sauti na shughuli za ndani zinasikika kirahisi kwa jirani.
Ufinyu wa Miundombinu ya Ndani: Ni ngumu kupanga kwa ufasaha miundombinu kama shimo la choo (septic tank), kisima cha maji, na mfumo wa maji ya mvua bila kuingiliana au kuhatarisha afya (kwa mfano, shimo la choo kuwa karibu sana na kisima cha maji).
Kukosa Sehemu ya Kupumzikia na Maegesho: Ukishajenga nyumba, nafasi inayobaki ya bustani (garden), parking ya magari, au eneo la watoto kuchezea inakuwa ndogo au haipo kabisa ikilinganishwa na kiwanja chenye urefu
View attachment 3700596
Kibaya zaidi ni pale watakatishaji fedha wanaupenda mchezo wa madalali.Kabisa, ikipostiwa nyumba moja, say inauzwa milioni 50, madalali wote wanaiposti , kila mmoja anaweka bei yake, wa mwisho anaweka milioni 100.
Hawana akaunti wala EFD. receipt, ila wanautajiri mkubwa , haram maana hawalipimkodi.
Acheni kupotosha watu. Mikocheni ushuani kuna viwanja vingi tu vya 20*20Kuvunjwa kwa Sheria za Nafasi (Setbacks): Sheria za ujenzi Tanzania zinataka uache umbali wa mita 3 kutoka kwenye njia/barabara na mita 1.5 hadi mita 2 pande za majirani. Ukitoa mita hizi pande zote nne za kiwanja cha 20x20, eneo linalobaki katikati la kujengea linakuwa finyu sana, jambo linalowalazimu watu wengi kusogeza nyumba hadi mpakani mwa majirani na kuhatarisha usalama wa moto.
Hao hata hawajui ukubwa wa 400sqm wanasema vidogo tu kulinganisha na 1000sqm.Achani ubinafsi kwa hiyo hamtaki watu wenye vipato vya chini wapate sehemu za kujihifadhi na familia zao??
Mama muuza mihogo ataweza kununua kiwanja Cha 40x40 Dar hii??
walipe kodi kwenye mamlaka ipi? maana sidhani kama wanatambulika rasmiHivi madalali wanalipa kodi
Aiseee hawa jamaa wanapiga hela sana kwani wizara ya ardhi inasemaje?walipe kodi kwenye mamlaka ipi? maana sidhani kama wanatambulika rasmi
wale real estate wakubwa wanajulika, ila kuna hawa madalali wa mitaa ambao ni wengi ,sijui wizara ina mpango ganiAiseee hawa jamaa wanapiga hela sana kwani wizara ya ardhi inasemaje?
Ukiingia kwenye mfumo wa tausi sasahivi kuna viwanja vinauzwa na serikali imevipimaSerikali ndo wanauza hivyo viwanja. Ingia kwenye mfumo wa tausi ujionee
anapaswa kuishi kiwanja kikubwa kwa bei nafuu, unataka akiwa anafanya mapenzi na mume wake majirani waskie miguno?Achani ubinafsi kwa hiyo hamtaki watu wenye vipato vya chini wapate sehemu za kujihifadhi na familia zao??
Mama muuza mihogo ataweza kununua kiwanja Cha 40x40 Dar hii??
Hao real estate wakubwa kama knight frank,remax nk,hao nao nao wanategemea connection za madalali wa mtaani mzeewale real estate wakubwa wanajulika, ila kuna hawa madalali wa mitaa ambao ni wengi ,sijui wizara ina mpango gani