Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
12/9/2009
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Udalali ya Majembe imesimamishwa kwa muda kuendelea na kazi ya kukamata daladala zinazokiuka sheria ya usafirishaji jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo imechukuliwa wakati ambapo kampuni hiyo imeleta mvutano mkali na madereva wa daladala jambo ambalo liliwafanya kugoma Jumatatu wiki hii na kusababisha adha kubwa ya usafiri jijini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi alinukuliwa jana na Redio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC-Taifa) akisema kwamba hatua hiyo ni ya muda tu.
Alieleza kwamba, lengo la kusimamisha kwa muda operesheni za Majembe ni kutoa fursa kwa wamiliki wa daladala kusahihisha kasoro zao na pengine kupata ufafanuzi zaidi juu ya mkakati huo.
Madereva wa daladala waliitisha mgomo kupinga kitendo cha Majembe kukamata mabasi yao na kuwatoza faini kati ya Sh100,000 hadi 300,000, kiwango wanachodai kuwa ni kikubwa ikilinganishwa na makosa wanayokamatwa nayo.
Majembe walikabidhiwa kazi hiyo baada ya kushinda zabuni iliyotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).
Majembe wanafanya kazi hiyo chini ya usimamazi wa Sumatra ambao ndio wanaosimamia leseni za usafirishaji jijini.
Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alipoulizwa na gazeti hili kuhusu hatua hiyo alisema ofisi yake haina taarifa za uamuzi huo.
Hata hivyo, alisema inawezekana yamefanywa kati ya Sumatra ofisi za kanda ya Mashariki na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kuona adha inayowapata wakazi jijini.
Juhudi za Mwananchi za kumpata Ofisa Mkuu wa Sumatra kanda ya Mashariki, Walukan Lihamba ziligonga ukuta baada ya kuwa nje ya ofisi yake na alipopigiwa simu yake ya mkononi hakupokea.
Hata hivyo, mmoja wa maofisa kwenye ofisi hizo alilithibitishia gazeti hili kwamba Majembe wamesimamishwa kwa muda lakini hakueleza wamesimamishwa kwa muda gani.
"Kinachoonekana ni kwamba hawa mabwana wakubwa wamekutana huko, wala sijui ni wapi, wakakubaliana. Hata maofisa wa Majembe waliofika hapa tumekubaliana wasiendelee kufanya kazi kwa sababu Mkuu wa Mkoa ameagiza." alisema ofisa huyo kwa sharti la kutotaja jina lake gazetini.
Mwananchi lilipowasiliana na Afisa Uhusiano wa Majembe, George Kyatika, alisema: "Hata sisi tumesikia taarifa hiyo redioni, lakini hatuna maelezo yoyote ya maandishi yanayotuamuru tusiendelee na kazi. Kama mpaka kesho hakutakuwa na taarifa ya maandishi, sisi tutaendelea na kazi".
Katika hatua nyingine, Kyatika alifafanua kuhusu utozaji wa faini ambazo wamiliki wengi wa daladala wanazilalamikia kuwa ni kubwa ikilinganishwa na makosa wanayokutwa nayo.
"Katika operesheni hii wajibu wa Majembe ni kusimamia zoezi, kupitia muongozo uliotolewa na Sumatra kwa lengo la kuhakikisha sheria za leseni na taratibu zilizowekwa kwa usafirishaji abiria nchini zinafuatwa kwa umakini".
Alitaja miongoni mwa faini zilizoorodheshwa kwenye kanuni za leseni za usafirishaji abiria za mwaka 2007, makosa ambayo yanatakiwa kutozwa faini ya Sh100,000 ni pamoja na kutumia lugha ya uhasama au matusi kwa abiria, kuwaziba au kuwazuia kwa makusudi wahudumiaji wengine wa usafiri na kuendesha gari zaidi ya vikomo vya spidi kwa kushindania abiria.
Alisema makosa ambayo yanatakiwa kutozwa Sh250,000, ni kufanya biashara ya kubeba abiria bila leseni au kibali maalumu.
Tangu Majembe ilipoanza operesheni hiyo Desemba Mosi, Kyatika alisema tayari imekamata magari zaidi ya 700 kwa makosa mbalimbali na kuyaagiza yalipe faini ofisi za Sumatra.
Alisema wameajiri vijana 200 ili kuboresha ufanisi wa operesheni hiyo, lakini wamebanwa kutokana na changamoto nyingi wanazokabiliana nazo.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ufinyu wa barabara na wingi wa foleni unaosababisha askari kusimamia uongozaji wa magari muda mrefu kuliko kufanya ukaguzi.