Mkuu, nadhani hili tatizo lichukuliwe kama fursa na siyo kulalamika. Kuna wazungu wawili walienda India zamani waliporudi kwao wakaulizwa hali ya huko ikoje? Mmoja akasema ameona watu wengi wanaotembea pekupeku bila kujali maradhi na hana hamu ya kurudi tena huko kwani anaweza kuambukizwa ugonjwa. Mwingine akasema ameona soko kubwa la biashara ya yebo-yebo na akafungasha mzigo kwa ajili ya kwenda kuwauzia. Hivi Tanzania inakosa kikundi cha vijana waliosoma IT na wakaanzisha website ya uhakika na app kwa ajili ya watu wenye nyumba na viwanja kuweka matangazo yao na wao wakachukuwa fee ndogo? Hapa wenye nyumba watakuwa wana-deal na wanunuzi bila kupitia kwa dalali.