Madalali waiponza yanga

Mr Alpha

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
273
Reaction score
765
Niliwahi kuonya habari ya madalali kwenye soka letu, nikaonya tabia ya kupenda vitu vya bei nafuu hatimaye naona Yanga wameingia kwenye mtego, wameenda kuchukua kocha wa bei nafuu, kocha wa viwango vya baba levo

Nashauri aliyewapa Yanga wazo la kumtimua Gamondi na kumleta huyu kanjanja akamatwe

Yanga ilishaingia kwenye ramani ya vilabu bora Afrika ila sasa inaenda kwenye anguko kwa kasi ya 5G

Huyu kocha mfumo wake ni wa ovyo ovyo hana game plan wala hajui namna ya kuset kikosi kulingana na uchezaji wa adui anapigwa mipira mingi ya akili timu imepoteana imekuwa kama nanyumbu fc

Inasikitisha sana aisee 😭😭😭
 
Your browser is not able to display this video.
 
 
Naunga mkono hoja waliyochangia kumuondoa Gamond wakakatwe haraka sana
 
Simjui ila hebu tuwe wa kweli. Mtu hana hata mwezi ulitegemea afanye maajabu gani?
Timu na wachezaji bado hajawajua vizuri, kama kuna uzembe kwa kipindi kifuoi anafix vipi?
Soka halina mwamposa, ni mchezo wa kisayansi na uwekezaji bahati ni nadra.
 
Simjui ila hebu tuwe wa kweli. Mtu hana hata mwezi ulitegemea afanye maajabu gani?
Timu na wachezaji bado hajawajua vizuri, kama kuna uzembe kwa kipindi kifuoi anafix vipi?
Soka halina mwamposa, ni mchezo wa kisayansi na uwekezaji bahati ni nadra.
Ile game ilihitaji akili za kawaida tu kushinda. Hawa Wasudan hawana mpira mkubwa ila wana defend vizuri sana. Kwa muda mfupi angeweza kuboresha namna ya kupasua ngome za timu inayolinda au kutumia mipira mirefu ya counter attack. Alichoboresha ni upigaji wa back pass nyingi zaidi.
 
Nyie kocha wenu aliyeishusha timu daraja akafukuzwa alikuwa ni wa Bei Gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…