msimamia kucha
JF-Expert Member
- Dec 1, 2013
- 683
- 551
Ni wazi mwanadada huyu anapitia kipindi kigumu na si ajabu hakujua ugumu wa kazi kabla ya kukubali kufanya ya kondoo katikati ya kundi la mbwa mwitu.
Pengine angejua tabia na desturi za watu wa nchi hii wanaojiita watu wa mpira asingekubali kuajiriwa kufanya kazi anayoifanya.
Naamini yeye aliamini anakwenda kufanya kazi na sio vita. Anachokutana nacho sasa ni vita na sio kazi za mpira wa miguu.
Na kibaya zaidi vita hiyo anapigwa na wale wanaojifanya wamevaa ngozi ya kondoo ila ndani mbwa mwitu wanaowaza kumrarua na kula nyama yake.
Vita hii anayokutana nayo inatokana na chuki ya yeye kuamua kuwa mkweli na kuitetea taasisi iliyomwajiri na kumlipa mshahara. Kwangu huyu dada mwenye msimamo wa kukisimamia kile anachokimini na kukitete ndiocho kinachomtesa. Watesi wake wameamua kumtangazia vita na kuapa ama zake ama zao.
Wanatumia nguvu kubea mno kutaka kumdhoofisha ili tu watimize malengo yao na asiwepo wa kusema hili hapana.
Wapo tayari hata kushawishi wanachama na wapenzi wa Simba ili walaghaike na kuwa upande wao kwa nia ya malengo yao.
Kabla hujaja kunishawishi kutaka niungane na wewe itabidi kwanza uje na majibu ya maswali yafuatayo.
1. Kosa lake ni lipi?
2. Wapi amekiuka miiko ya kazi yake?
3. Kanuni ipi ya mbwa mwitu au ya Simba amevunja?
4. Kosa lake ni kusema ukweli na kufichua dhambi?
Kwa karne hii bado tunaeneza majungu na fitna ili tu kumfanya mtu ajione mnyonge kwa manufaa ya malengo ya giza?
Tumefika mahali mtu akiwa ni mtumishi anayefuata ueledi na kufuata taratibu za kazi basi huyo anakuwa adui?
Badala tuitumie elimu na utendaji mzuri wa kazi wa huyu dada kwa manufaa ya kulisogeza soka mbele tunamjengea majungu na kutaka aondeke ili tutimize majungu na janja janja.
Kwa mwenye mapenzi ya kweli na mpira wetu bila kujali itikadi ya klabu yake. Atasimama na Babra. Ila wenye kutaka njia za mkato na janja janja watapambana mpaka wahakikishe anaondoka ofisini.
Hatukatai kwamba kama binadamu na yeye ana mapungufu yake ila hayatoshi kuondoa yale mazuri anayolifanyia soka letu.
Babra anatakiwa kwa sasa kumtia moyo na kumuhakikishia wapenda soka wa ukweli na maendeleo ya kweli tuna macho na tunaona kila analofanya kwa klabu yake na soka kwa ujumla.
MIMI NIMEAMUA KUSIMAMA NA BABRA