Madam Rita ateseka siku 365 Muhimbili

TANMO

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
11,763
Reaction score
11,873


Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Productions inayoendesha shindano la kusaka vipaji vya muziki, Bongo Star Search (BSS), Rita Paulsen ‘Madam' amesimulia mateso aliyopitia takriban mwaka sasa (siku 365) baada kuvunjika mguu mwaka jana alipopata ajali ya gari katikati ya Jiji la Dar.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwenye mahojiano maalum hivi karibuni aliponaswa na gongo linalomsaidia kutembea, Madam Rita alisema kwa kusikitisha kwamba, baada ya kupata ajali alitibiwa kwenye Hospitali ya Muhimbili lakini madaktari walimwambia aliteguka tu kumbe alikuwa amevunjika mfupa.


"Nimepitia mateso makubwa. Mwaka jana baada ya kupata ajali na kuvunjika mguu nilipopelekwa Muhimbili waliniambia nimeteguka tu, na wakaamua kunifunga hogo ambalo baadaye walinifungua na kuniambia nimepona," alisimulia Madam Rita na kuongeza:


"Baada ya pale nilianza kujiachia hata niliposikia maumivu na kuwaambia walisema niukanyagie tu kwamba hali hiyo ingebadilika kwa sababu ulielekea kupona, kumbe nilikuwa nimevunjika kabisa mfupa na kama ningejua siku nyingi hata nisingejiumiza kiasi hicho.


"Ujue baada ya kuambiwa hivyo, nilishangaa kuona maumivu yanazidi, nikaamua kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuuangalia zaidi mguu wangu kwa sababu maumivu yalikuwa yakiongezeka kila siku.

"Nilikwenda kwenye Hospitali ya Morning Site ya Afrika Kusini ambapo nilifanyiwa upasuaji na kugundulika nilivunjika mfupa na kwamba tayari nilipokuwa nikitembea ilikuwa ikipandiana.

"Ona sasa nilivyoteswa na mguu huu maana ajali nilipata mwaka jana na huu upasuaji nimefanyiwa mwaka huu Afrika Kusini.


"Kiukweli hospitali zetu saa nyingine zinatusababishia shida ambazo siyo za lazima maana kama awali wangenifanyia upasuaji wakati nawaambia ninaumia baada ya kunitoa hogo, basi leo ningekuwa nafanya shughuli zangu.


"Naona bora pale Fame Centre (Dar) maana wao waligundua tatizo na kunishauri kwenda Sauzi ambapo nimefanyiwa upasuaji na mguu unaelekea kupona kwa sababu mwanzo nilikuwa natumia magongo mawili lakini ona leo ninajikongoja kwa gongo moja ambalo nalo si muhimu sana sasa."



Habari ya Hisani ya GLobal Publishers TZ

MY TAKE:
Huyu Mama alikuwa na uwezo wa kwenda Afrika ya Kusini kwa Uchunguzi zaidi na ikabainika kuwa Madaktari wa Muhimbili walikosea. Mtanzania masikini asiye na uwezo wa kwenda kuhakiki afya yake nje ya nchi ana wakati mgumu sana.

Mungu Ibariki Tanzania.

Mapendo,
TANMO.
 

Attachments

  • IMG_0009.jpg
    68.6 KB · Views: 8,518
  • IMG_0015.jpg
    77.1 KB · Views: 8,445
Pole sana Madame Rita!

Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
 
Duh kwa kweli inasikitisha mpaka mtu unaona hakuna haja ya kujivunia Tanzania.
 
Mbatia Akiwaambia Ubovu Wa Elimu YETU Watabisha Mpaka Basi Ila Sisi Tunaoishi Hapa MUHIMBILI Ndo Tunapajua.
 
Sasa madam hawakukupiga xray,ungelitambua mapema kama umevunjika au laa.Ukivunjika, mfupa unaonekana kwa macho.
 
Afya na Elimu ni majanga makubwa sana hapa nchini zaidi ya serikali mbili au tatu. Inanipa HASIRA sana jinsi watu tunavyokubali kuishi maisha haya. AAAARGGH!!
 
Rais atakaeweza tz lazima aangalie vitu viwili muhimu sana Elimu na Afya
 
Type yako ni wale wanaofikiri kwa kutumia makalio lol kweli tuna watu nchi hii na wanamichango. Haya kamchukue wewe hana mtu kwa sasa.
nan anamla huyu madam?
 
Pole Madam, kwa engine hapo ndio unakuwa umepata ulemavu hivi hivi!
 
Sasa hapo wenzangu na mimi tusio na hela ya kukwea pipa, mbona tungekuja kushtuka mguu ushakuwa na more complications. Sometimes hizi hospitali za serikali zinaweka maisha yetu rehani.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mungu atuepushe na majanga ,maskini sie.
 
hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania. serikali sikivu inaboresha maisha yako.
 
With all due respect Siamini/Sidhani kama "kuvunjika" kwa mguu kunashindwa kugunduliwa hapa Muhimbili tena ukifuata hatua/njia elekezi husika, unless kuna shida nyingine kuhusu Muhimbili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…