Madam Ritta na team yote ya BSS pigeni moyo konde yote yatapita

Madam Ritta na team yote ya BSS pigeni moyo konde yote yatapita

evart

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2016
Posts
2,838
Reaction score
2,772
Habarini wana JF ni matumaini yangu mpo wazima kabisa katika kipindi hiki cha karantini tuendelee kuchukua tahadhari.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada. Kwenu madam Ritta na timu nzima ya BSS kwanza niwapongeze kwa kazi kubwa mliofanya na mnayoendelea kufanya ya kuinua vipaji vya watanzania hususan katika muziki.

Hivi majuzi mmepata changamoto kubwa kutoka kwa wasanii na Mashabiki wenu kila mtu akiongea lake wengine wakitoa matusi, kashfa na madukuduku mbalimbali .

Nawasihi kazeni moyo, vumilieni msiyumbishwe sana na maneno ya watu maana wengi wao ni wanafiki wamesahau mema yote mliyowatendea kwa baya moja ambalo hawana uhakika nalo na hii ndio tabia ya wengi wetu.

Nawatakia kila la heri katika kazi yenu njema.
 
Hakuna cha wema haiwezekani watu watangaziwe watapewa pesa ambayo hawatoi wakati wadhamini washatoa pesa.

Huenda wote wakiongea itajulikana walikuwa hawapewi pesa yao maana mpaka Kayumba kathibitisha naye hakupewa pesa. Sasa si utapeli huo.
 
Kayumba alihojiwa TBC alisema amepewa hela na kumjengea baba yake nyumba ,kajenga nyumba yake ,kanunua gari na anafanya biashara
Hakuna cha wema haiwezekani watu watangaziwe watapewa pesa ambayo hawatoi wakati wadhamini washatoa pesa.

Huenda wote wakiongea itajulikana walikuwa hawapewi pesa yao maana mpaka Kayumba kathibitisha naye hakupewa pesa. Sasa si utapeli huo...
 
Wamelipa deni au ndio unawafariji ili shindano linalokuja nawewe wakufikirie
 
Kuna sehemu haujelewa,watu hawaisemi BSS vibaya kwa sababu inaendeleza vipaji, BSS inasemwa vibaya kwa sababu washindi wake wanadai kutokupewa hela ya ushindi ambayo waliahidiwa.

kumbuka kwamba mtu haendi BSS peke yake kuimba, watu wanaenda pale kushinda ili wapate pesa, kwa sababu kama ingekua ni kuimba leo washindi wake wote wangekuwa masuper star wakubwa nchi hii. wengine ndo kwanza hata hawajulikani ni wana muziki au mashabiki (hili tuliache).

Waambie BSS wawape washindi pesa yao halafu uje hapa usifie.
 
Kayumba alihojiwa tbc alisema amepewa hela na kumjengea baba yake nyumba ,kajenga nyumba yake ,kanunua gari na anafanya biashara

Latest interview yake aliyohojiwa kama weeks mbili nyuma akiwa na meneja wake alisema alipewa milion moja mama yake na baba yake nao wakapewa milion moja, akapewa na gari bovu ambalo lilikuwa linaharibika lilichukuliwa garage moja Temeke na baada ya miezi waliliuza kama scraper kwa wakata magari.

Kisha kakabidhiwa kwa akina said fella ambapo fella akampeleka kwenye kati ya zile nyumba za ya moto band, akaambiwa moja ya kwake na zilikuwa hazijaisha, hakuwahi hata pewa hati yani alionyeshwa nyumba tu. Kisha kaambiwa milion 30 itatumiaka wenye promotion yake.

Akasema hakuwahi yasema hayo alikuwa yeye anahisi akisema italeta mtafaruku na atashindwa penya kimziki hivyo yeye aliamua apige kimya kwakuwa watu washamfahamu yeye ni nani apambanie tu mziki wake.

Na siku anafanyiwa hiyo interview ilikuwa siku ya pili baada ya Shonza kutoa agizo na akasema Madam Rita amempgia ila akagoma kusema alimwambia nini
 
Kwamba hawana jema hata moja?
Kwasasa tunaongelea utapeli wao wa kutowapa walichoahidi maana vijana wengi wanafuata hiyo pesa na ndiyo maana asilimia kubwa ya waliopita pale hawakufanikiwa kuwa wasanii wakubwa
 
Kuwapa u famous ni bora kuliko pesa
Ufamous wakati wao wamefuata pesa, tuache unafiki kama hawajapewa pesa walioahidiwa huo ni utapeli hakuna neno mbadara zaidi.
 
Back
Top Bottom