The Businessman
JF-Expert Member
- Jan 9, 2014
- 7,397
- 9,255
Duh.... wonders shall never end in this country .....tuna safari ndefu sana kuwafikia wenzetuNaandika uzi huu kwa niaba ya Watanzania, kumhusu Madam Wema Sepetu, mlimbwende wa zamani wa Tanzania, akishinda Taji hilo mwaka 2006 mbele ya Jokate Mwegelo, mjasiriamali, msanii wa filamu, muziki na mwanaharakati na Lisa Jensen, mwanamitindo.
View attachment 330138
Wema Abraham Sepetu, alipotawazwa kuwa Malkia wa Urembo Tanzania mwaka 2006
Kwa muda mrefu Madam amekuwa kwenye vichwa vya habari kwa wema na kwa ubaya, kama lilivyo jina lake, Wema Sepetu a.k.a Mama Ubaya, lakini ubaya ukionekana kuzidi wema wake machoni pa kundi la 'Watanzania Wastaarabu'.
Wema, kama washindi wengine wa taji hilo la Umiss, amelitendea haki kwa kufanya kazi zinazotakiwa, na walau kuka nalo vema hadi alipolikabidhi kwa mrithi wake, Richa Adhia mwaka 2007.
View attachment 330108
Wema Abraham Sepetu akiwa na Diamond Platinumz, msanii wa kimataifa wa Tanzania, enzi za mapenzi yao, kwenye Tuzo za MTV Afrika.
Licha ya ushindi huo, madam amekuwa na 'kismati', kama wenyewe wanavyodai. Wachumba aliokuwa anatembea nao walipata mafanikio makubwa kwenye kazi zao, iwe muziki, uzalishaji au uigizaji wa filamu na pengine hata biashara zisizohusisha sanaa.
Ukikaa na Waridi utanukia, bila shaka mada amekuwa waridi kwa watu wengi, akiwaangazia nyota na kuwatangaza kimataifa. Madam akiwa upande wako, nani aliye juu yako? Kwa hili tuna deni kwake...
Madam amemsaidia sana msanii Diamond Platinumz, licha ya kuwa pumziko lake kwa miaka kadhaa, alimfundisha mambo mengi ya msingi ikiwemo lugha ya Kiingereza, nyenzo muhimu kwenye utandawazi.
Madam alimtoa Diamond kutoka uselebriti kunuka na kumfanya kuwa wa kisasa, msanii wa kimataifa. Popote tunapomsifia Chibu, tujue tuna deni kwa Madam Wema Sepetu.
View attachment 330110
Rangi za midomo za Kiss, kazi ya ubunifu wa Wema Abraham Sepetu
Licha ya umaarufu wa magazeti na Blogu, madam ana juhudi binafsi za kimaisha, uzinduzi wa Kampuni ya Endeless Fame (inayomsimamia msanii Mirror), brand yake ya ' Kiss Lipstick' na maajabu mengine kibao.
Madam ni msanii, NDIO, mmoja wa wasanii wakubwa kabisa wa Bongo Movie... Tunapoona mafanikio yoyote kwenye tasnia, madam ana mchango wake mkubwa sana, kwa kweli anatudai.
Madam amewahi kushiriki kwenye Siasa ngazi ya kitaifa, kwa kugombea Ubunge Viti Maalum ndani ya Chama cha Mapinduzi. Licha ya kuwepo kwa dalili za ushindi wake kuchakachuliwa, alionesha uungwana wa hali ya juu kwa kukubali matokeo na kushiriki kikamilifu kwenye kampeni za Uchaguzi 2015.
View attachment 330117
Wema Abraham Sepetu akihutubia hadhara kwenye moja ya mikutano yake ya kisiasa.
Madam ni Celeb pekee kuwahi kuwa na Timu yake, timu inayojitambulisha kama #TeamMadam na ikijumuisha watu wakubwa na maarufu; Kajala, Petit Man, Aunt Ezekiel, DJ Rommie Jones (DJ wa Diamond Platinumz) na wengine wengi... Huu ni umaarufu wa Kiwango cha Kimataifa.
View attachment 330116
Kava la filamu ya Madame, moja ya kazi maarufu na bora za Wema Abraham Sepetu
Licha ya kupumzika kidogo shughuli za filamu, bado hayuko nyuma kuwaunga mkono wasanii wenzake. Juzi alienda na gari lake kumpokea Elizabeth Michael Lulu, huu ni upendo uliopitiliza.
Madam ni mshiriki mzuri wa matukio ya kijamii na kindugu. Anahudhuria misiba, sherehe na matukio mengine kwa ukamilifu.Hata uhusiano wake na washabiki wake sio wa kunata wala kujidai, kama wadada wengine maarufu.
Sijasahau alivyojitolea kumtoa jela Kajala Masanja, wakati ambao wasanii wengine maarufu walipomsusa. Huu ni wema usio na kipimo...
Licha ya utu wake huu, madam amesakamwa na magazeti, blogu, mitandao na watanzania kwa ujumla. Wakimtusi, wakimkejeli, wakitengeneza picha za uongo, wakimuita malaya na wakati huo wakinufaika na kuuza habari zake.
Licha ya ubaya huu tuliomlipa, bado Wema ameendelea kuwa mzalendo, na mtu anayejitolea kwa taifa, kwa wasanii wenzake na jamii kwa ujumla. Kwa ambao wamewahi kuroll na Mama Lao, watakubaliana na mimi kuwa hayuko namna ambavyo watu wanamchukulia.
Kwa kweli wema wa Madam ungekuwa unaandikwa, vitabu vya dunia hii visingetosha kuuelezea wote.
Natoa wito kwa sisi kama taifa, kutafakari ubaya huu tuliomvika madame, na tumuombe radhi kwa ujumla wetu... Ikiwezekana tumjengee na mnara wa kumbukumbu.
Mimi ninachojua pamoja na lugha, Madam Wema Kamfundisha Diamond kuogelea. Huyu Madame Mungu azidi kumbariki hadi ashangae.Aliyemfundisha lugha diamond ni WEMA au PENNY?? mbona mwanafunzi mwenyewe anasema ajafundishwa na WEMA!!!
Hii nchi kuwa houseboy wa Madame Wema Abraham Sepetu ni zaidi ya kuwa na Degree ya Kwanza ya chuo cha umma, ni zaidi ya kada nyingi sana Serikalini. In fakt ikitokea madam akataka niwe hausiboi wake nitabarikiwa sana.Houseboy wa Wema Sepetu nae Una mume? Kweli watanzania lazima waombe samahani
Diamond ni msanii wa Afrika, Ali Kiba ni Balozi wa Kimataifa wa kupinga ujangili. Rose Muhando, Belle 9, Navy Kenzo na wengine wana mikataba na makampuni ya kimataifa ya muziki. Hot Lulu na Richie wamekwala tuzo juzi, Bongo Movie inaenda kimataifa na wewe upo hapa unahubiri safari ndefu.Duh.... wonders shall never end in this country .....tuna safari ndefu sana kuwafikia wenzetu
Umeona eeeeh, kuna jambo si bureKuna nini kinafuatia hapa?
Thread nzuri sana hii.
Natumia nafasi hii kumuomba msamaha madam pia. Nimekua nikichekelea pindi watanzania Wenzangu wanapomchafua bila kujali Umuhimu wake. Watu wametajirika kwa kuuza magazeti ya kumchafua wala hajawa na kinyongo na Mtu.
Wema Sepetu sio malaya tena hana tabia chafu. Hajui kubadilisha mabwana hadi labda mabwana wamuumize na kumuacha bila sababu. Kwenye mapenzi Wema hajui kuchanganya mabwana, akipenda amependa na yupo wazi si sawa na Wasanii wengine ambao hujui mumewe ni nani kwani wanao wengi.
Madam Wema Sepetu anafaa kuwa Mke na Mama wa Familia kwani kapitia mikimikiki mingi ya maisha na ana uvumilivu wa hali ya juu. Kama kuumizwa kaumizwa sana.
Wema Sepetu tusamehe Sisi Watanzania, tumekukosea sana. Sijawahi sikia Wema kagonganisha mabwana, kafumaniwa wala kachukua mume wa Mtu.
Tusamehe Madam Wema, tupo chini ya Miguu yako
Juzi kamkana mkongo kuwa hamjui na wala hafikirii kuwa na mkongo. Ajabu mkongo kaamua kumwaga mboga. Huyu mama ubaya ni tatizo anahitaji canceling chibu amemuathiri Sana kisaikolojia hatulii na mwanaume mmoja.unamtetea, basi watu wasio maarufu waliopita hapo ni zaidi ya hao maarufu unaowajua, take it or leave it!
Sijawahi kumuona huyo madame akiwa amevaa hizo nguo za kuogelea. Au anaogeleaga na dera hata picha akiwa swimming pool sijawahi iona.Mimi ninachojua pamoja na lugha, Madam Wema Kamfundisha Diamond kuogelea. Huyu Madame Mungu azidi kumbariki hadi ashangae.
Pool Table tumecheza Embasy Hotel kabla Magufuli na Makonda hawajaja mjini, token buku enzi hizo...Mkikatazwa kucheza pool asubuhi mnaanzisha ujinga mpya
Diamond sio mtu wa kumsikiliza sana, alishasema anarekodi wimbo na Ne-Yo...Aliyemfundisha lugha diamond ni WEMA au PENNY?? mbona mwanafunzi mwenyewe anasema ajafundishwa na WEMA!!!
Kwa mujibu wako. Mimi nawajua viongozi wa makahaba ambao ni wakuu wa mashirika ya Umma na wanasiasa wakubwa, bila kusahau mashoga. Madam Wema Sepetu ni mwanamke jasiri, malkia wa nguvu... Kila sekta ana mafanikio, hadi siasa ambayo amethubutu kugombea Ubunge wakati akina nyie mkibwabwaja majukwaani nyuma ya keyboard.hahahahahahah
sasa na wewe nawe uko too low
Huyu ni kiongozi wa makahaba
mfano mbovu kabisa katika jamii yetu ...asiyefaa kuigwa kabisa
unamtetea, basi watu wasio maarufu waliopita hapo ni zaidi ya hao maarufu unaowajua, take it or leave it!