Madaraja mapya kwa Mitihani ya Kidato cha nne ndo haya hapa!!!.

Tunahitaji mjadala na tume ya kina ya kuchunguza mustakabali wa Elimu yetu. Elimu ya Tanzania ipo njia panda, inayumbayumba. Mungu saidia watawala wetu wazinduke usingizini.

Hata siamini hayo madaraja mapya bado, je kidato cha Sita yamebadilika?? Dahhh... Namshukuru Mungu nimesoma hapo kabla. Haki ya Mungu nawaambieni, hapo mwakani kutakuwa na msiba mzito kielimu, tujiandae kuomboleza mapema. Ni hari. Naona giza nene mno. Hakuna haja ya kurudia mitihani.
 
Kama kweli serikali imechakachua viwango vya kufaulu, basi hii itakuwa ni pekee kabisa.

Kwahio inamaanisha kwamba kama mtu alifeli mtihani wa form IV mwaka huu, bado anapewa nafasi ya kuendelea na masomo ya juu ya form V na VI au tu kuridhishwa kwamba angalau alipata alama kadhaa za D.

Hili ni janga jamani!
 
tunataka mjadala wa mustakabali wa elimu yetu,sio kila kukicha mabadiliko yasiyokua na tija

hapa NECTA na serikali kwa ujumla wanatakiwa watoe sababu ya mabadiliko haya. la sivyo madaraja haya yatazidi kuichafua serikali kwa matokeo mabaya ya mitihani yetu macho!!!!!!!!!!!
 
kama ni kweli. kuna haja ya kupima uwezo wa kifikra wa viongozi wanaosimamia elimu. kama nusu wanafeli kwa 21 je 35?
 
kama ndivyo mwaka huu zero zitakuwa 90% ..shule za kata mpaka wakafikishe hyo D..
 
Hizi ni propaganda za chadema ili kuwalaghai watu waende kwenye maandamano yao kesho.
 
Sasa significance ya kufanya hizo marginal changes (kama habari ni ya kweli) ni nini?
 
Necta wameshndwa moja wanatka mia wataweza waboreshe kwnz mfumo wa elimu bora kw kila mwanafnz
 
Yaani hapo tutegemee viwanda vya zero kibao sana...hasa shule za kata wataweza kweli kufika 35%?sidhani hilo nalo janga jipya la taifa...vijana hawasomi kabisa uwezo kukariri nyimbo na mambo starehe haya ingekuwa sawa na kukariri notes za masomo...sidhani kama angefeli kijana wa kileo na simu zao masikioni full time...suruali chini makalio...na wasichana wanavaa skeli mlegezo pia!
 
Fanyen hvyo hta kwenye divisions angalau III ianzie point 28..lasivyo elimu ya Tanzania itaelekea shmon...
 
Isijekuwa hizi alama ndizo zilizotumika kumark mitihan ya mwaka 2012 !!!
 
Fanyen hvyo hta kwenye divisions angalau III ianzie point 28..lasivyo elimu ya Tanzania itaelekea shmon...

Big up Mkuu. Mie nashangaa watu wanavyotaka wanafunzi wenye alama ndogo waambiwe tu wamefaulu, Ninavyojua mie Kidato cha Pili mtahiniwa anatakiwa awe amepata wastani wa Alama 30. Je Wizara inaweza kusema Alama 30 F2 halafu kwa wahitimu F4 iwe alama 21?
Naomba mwenye waraka unaoonesha Alama ya ufaulu F4 inatakiwa iwe 21 auweke hapa ili tuuchambue vizuri. Je hizo Alama 21 anatakiwa apate kwenye mtihani wa NECTA au zimejumuisha na Alama za Maendeleo za kila siku? Tupeni huo waraka tuweze kuchangia ipasavyo
 

Kati ya F na D kuna kuanzia 21% mpaka 34% ni Barajas gani? August hizo points zinapelekwa wapi?
 
hakuna page ya necta ya kiharali facebook.officialy si taalifa ya kweli.futa thread ka vip au usirudie kuchukua facebook habari huwa hazna ukwel ni udaku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…