Madaraja ya mserereko na msawazo wa madaraja umekwama wapi? Tusilete siasa ili kujizolea umaarufu bungeni na vyombo vya habari

Madaraja ya mserereko na msawazo wa madaraja umekwama wapi? Tusilete siasa ili kujizolea umaarufu bungeni na vyombo vya habari

bahatibahati

Member
Joined
Jul 4, 2023
Posts
44
Reaction score
84
Hivi karibuni yametolewa matamko mengi kwa watumishi kwamba KATIKA MWAKA huu wa fedha 2023/2024 unaoishia June hii 2024 watumishi wote watawekwa kundi Rika Ili wasitofautiane Madaraja kwa kuzingatia seniority.

Ndiyo maana maafisa utumishi kutoka HALMASHAURI zote nchini walielekezwa na mh. Waziri wa Tamisemi kupitia taarifa za watumishi wote na walikaa kwa muda wa wiki mbili DODOMA. Wakipitia taarifa za mtumishi Mmoja hadi mwengine kama walielekezwa na mamlaka.

Hali imekuwa tofauti kwani miongozo inayopelekwa kwa watumishi haitoe tafsiri ya msawazo au mserereko.
Hii inaumiza sana mfano Anita ya 2014 awe sawa na aliyeajiriwa 2005?

Waziri waambieni watumishi ukweli kama bajeti imekwama wafahamu Hilo na nilitolewe taarifa.
 
Jana hapa wilayani kwetu,Moja ya wilaya ya mkoa wa pwani wamepita watu wa tamisemi na kusema yote hayo mwezi July yatafanyika
 
Unaharaka ganj,mama yuko kazini ,subiri mshahara wa juni na july hutaamini macho yako kama una vigezo vya kupata haki hiyo
 
Kuna waraka umetoka hauzungumzii habari hizo
Weee ni mtumishi wa umma,unajua kuwa kupanda daraja ni hakiya mtumishi?,huo waraka uliozungumzia kupanda madaraja wewe umeuona?
 
Baadhi ya watumishi hawajapanda Madaraja kwa zaidi ya miaka 12 , kwa Hali hiyo utendaji kazi uliotukuka utakuwepo?
Serikali inatakiwa kundi Rika lote wapande Madaraja , unakuta watumishi wameanza kazi pamoja na elimu yao inafanana lakikini wanatofauti kubwa ya Madaraja yao. Ifike mahali Hili suala lifanyiwe kazi kwa vitendo na isiwe propaganda tu.
 
na sidhan kama watapanda vyeo,maana waraka uliotoka tarehe 28/05/2024 hauzungumzii chochote ,na Naibu katibu mkuu anayeshughulikia Elimu Charles Msonde amepita kila halmashauri anaongelea habari ya harmonization(msawazisho)wa madaraja lakin waraka unawazungumzia walionyanganywa vyeo 2016
 
Wewe ajira ya ualimu ya mwaka gani?
 
Back
Top Bottom