voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
Mifano iko mingi sana!
Marehemu Sankara wa Burkina Faso alipinduliwa na kuuwawa na aliekiwa Rafikie wa karibu na msiri wake Bless Compaore. Marehemu Patrce Emely Lumumba alipinduliwa na mtu wake wa karibu Joseph Kasavubu kwa ushirikiano wa wabelgiji na Mobutu Sese Seko.
Na mfano wa hivi karibuni kabisa ni pale kiongozi wa Korea kaskazini Kim Ill Jong alipomuuwa mjomba wake Jang Song Thaek, kaka wa kuzaliwa tumbo moja na mama yake mzazi Kim Ill Jong.
Hakuishia hapo tu, bali pia kwa kuhofia kupoteza kiti chake cha urais. Kim Jong Ill alimuuwa kaka yake wa kizaliwa tumbo moja aliyejulikana kwa jina la Kim Jong Nam, mauaji yaliyotekelezwa huko Malaysia kwa vikosi maalumu vya kikachero wakati akiwasili Airport jijini Kuala Lumpur!
Kuna watu Mashuhuri Duniani na Africa kwa ujumla waliopoteza maisha yao sababu ya kitu inaitwa Madaraka ya uongozi hususan wa dola kuu.
Watu kama Chris Hani, Steve Biko(s'Africa), Thom Mboya, Robert Ouko, (Kenya)Samora Machel(Mozambique)na hata askofu Jaral luwum kule Uganda. Kwa uchache tu.
Nimetoa mifano hiyo michache huku nikiacha kutaja historia za wafalme waliokuwa wakiuwa kaka zao na kujisimika ufalme badala yao.
HITIMISHO langu!
Kwa wanasiasa wengi Duniani, kwao madaraka huwa ni maktamu na wako tayari kuwaondoa hata wale waliokuwa wakiwaamini sana, ili mradi tu wakalie kiti cha enzi.
Kwa sababu tunashuhudia watu wakiwaua ndugu zao wa damu ili tu washike nafasi zao za uongozi.
Kwa hiyo Madaraka ni kama kitu kilicholaaniwa kuliko vitu vyote. Sababu mtu akishanogewa na madaraka anageuka kuwa adui wa kila mtu anayedhania kwamba anaweza kuhatarisha nafasi yake ya Madaraka.
Mfano mwingine ni Paul Kagame wa Rwanda ambaye amewaweka ndani au kuwaua wale wote anadhani wanahatarisha utawala wake.
Akiwemo aliyewahi kuwa Waziri mkuu wa Rwanda Pastor Bizimungu. Anayetumikia kifungo cha nyumbani kisicho na ukomo.