Madawa ya kienyeji yana athari yoyote katika afya ya uzazi?

Siyo kweli kuwa dawa za asili hazina kipimo maalumu kwa mtumiaji. Mtoaji wa dawa za asili ambaye siyo tapeli, lazima atakupa na maelezo ya kiasi gani utumie. Wengine kama umeenda kumchukulia mgonjwa dawa atakuuliza kama mgonjwa ni mtoto ama mtu mzima baada ya majibu anakuelekeza kiwango utakacho mpa.

Msukumo wa kibihashara kwenye dawa unaofanywa na makampuni ya kibepari ndiyo ambao unasababisha kudhalilisha na kudharau waganga wetu wa kiasili/kienyeji na tiba zao. Hawajari tena uhai wa mtu kama tunu bali wanajali uhai wa mtu kama mtaji ama kikuzio cha biahashara zao. Ni kweli baadhi ya dawa zao zina saidia lakini wao hawataki fair competition kwenye kutua huduma ya dawa ya kutibu. Wanataka wao wawe ndiyo wazalishaji na wauzaji pekee wa madawa. Na kwa sababu dawa zetu za asili ni rahisi sana kwenye gharama za uzalishaji basi wanaona hawawezi kushidana na sisi. Hivyo hujuma za namna zozote zitarajiwe kutoka kwao.

Ninachokiona hapa ni kuwa makini....na chanzo cha tiba zetu za asili (mimea) hawa jamaa si wema. Wanataka tuwe tegemezi kwa kila kitu...wamefanikiwa kuangamiza mimea yetu ya asili mfano migomba huko Uganda na Kagera ili tuwe tegemezi kwa chakula....na sasa watakuwa wako bize kutafuta aina ya mimea tunayotumia kama dawa asili ili waiharibu ili tutumie dawa zao tu...hasa baada ya kugundua tumeshtuka kuwa dawa zao sizote zinafaa kututibu magojwa yetu kama madawa yetu ya asili.
 
Mphamvu, Hawa matabibu haswa wanaotumia dawa za asili ku-attend wagonjwa, Dawa zao Si huwa Mpaka waoteshwe ndotoni kwanza?

Ni Tiba ya IMANI!

Kuna utapeli mwingi sana unaofanywa kwa jina la tiba za Kiafrika, iweni makini nao!

Mwanzo wafuasi wa tiba za Kizungu mmedai kuwa ni miti hii hii inayofanyiza dawa, sasa unadai inategemea imani na ni hadi uoteshwe, jambo ambalo sio kweli.

Kusema kuwa dawa hizi hufanya kazi kwa imani ni sawa na kusema nikila chakula bila imani sitashiba. Mambo ya kibaiolojia hayana uhusiano na imani mkuu.

Turejee kwenye mada, ambayo ni mchango wa dawa hizi katika afya ya uzazi.
 

Sababu za afya ya uzazi kudorora ni mtambuka, yaani sio jambo moja pekee linalosababisha.

Kuna mahali nchi hii suala la uzazi ni suala tukufu na huanza kupewa umakini tangu siku ya kwanza, kuanzia vyakula na tahadhari nyingine za madawa. Kwa hali ilivyo sasa, kwenda hospitali ndio namna salama kwa kina mama wetu, huko kuna waganga na vifaa tiba zaidi kuliko nyumbani ambako hata utaalamu wa tiba wa Kiafrika umeuwawa.
 

Wanaharakati fulani wa mifumo ya kisasa wanadai kuwa ulimwengu wa madawa ni industrial pharma complex, ni biashara zaidi kuliko tiba kama ulivyodai.

Shanga Serikali yetu kwa mfano, wana ushirikiano wa muda mrefu na manchi majizi kwenye yanayoitwa 'mapambano' dhidi ya Maleria, mapambano ambayo hayajawa na faida zaidi ya kutufanya kuwa wateja wa kudumu wa neti na madawa yao ambayo wanayabadilisha kila baada ya miaka kadhaa.

Mimi hutibu maleria kwa ufanisi kwa kutumia dawa rahisi kabisa za nyumbani, juisi ya aloe vera na wakati mwingine mbegu za limao. Tiba ni haraka, haipandishi homa na haiachi sumu/athari mwilini kama zilivyo dawa-sumu za Maleria.

Kuendelea kuwa wategemezi kwa wazungu kwenye tiba sio jambo la bahati mbaya, ni makusudi na linasimamiwa ili liendelee kuwepo kwa faida yao, laanakum!
 

Serikali inatumia pesa nyingi kwenye ruzuku za madawa ya kizungu huku tafiti za tiba za Kiafrika zikizimwa kwa makusudi.

Kitengo cha Tiba Asili Muhimbili kipo kama kilivyokuwa miaka kumi nyuma, hakuna jitihada za kukitanua ama walau kushirikiana na matabibu wa Kiafrika wanaopatikana karibu nchi nzima kwa manufaa ya watu wa nchi hii.

Ipo taasisi moja nchini Afrika Kusini, inatengeneza dawa za asili lakini huwa ghali sana kwa kuwa hakuna ruzuku wala usaidizi kutoka kwa Serikali zao. Kuna jamaa wapo Vingunguti wanaweza kutibu mifupa iliyovunjika kwa muda mfupi sana, hawajasoma utabibu popote na walipojaribu kuwaona hao pumbavu wa Muhimbili unajua waliwajibu nini? Eti waje na makaratasi ya tafiti zao zoote hadi wakafikia hitimishi kuwa dawa zao zinatibu mifupa, waona walakini huu?
 
Wazee wetu wa Afrika walitumia, baadhi tumezaliwa na wazazi wametumia dawa za kienyeji. Hazitolewi hovyo hovyo wana vipimo vyao na namna zao za kutoa dose na watu walipona na wanapona.
Eneo lile la hospital ya Muhimbili lilikua shamba la dawa za kienyeji-zingine zipo pale hata leo. Wazungu waliua teknolojia yetu ya tiba. Sasa hivi wala hatuamini tena zile dawa zetu.
Kwa kawaida hata hospitl za wazungu/wakoloni dose huwa inabadilika kulingana na tafiti na uzoefu na jamii husika.
Dawa zetu za asili leo ishu ya dose inaweza kuwa shida maana watumiaji sio wengi kuweza kupata data za kutosha ili kutoa dosw sahihi.

Nasikitika sana, wakoloni wametuharibia maisha
 
Mimi nakuunga mkono kabisa, haya matibabu ya wazungu hayakua ya kwetu-sisi tunaiga tu na kujitahidi kufanana nao. Tunasahau kwmb lengo ni mtu mgonjwa apone.
Kama njia zetu za tiba za kiafrika zinaponya ya nini kujitahidi kujua ya wazungu kiasi cha kudharau yetu?
Mashine zote tunanunua kwao. Vidonge kwao, standard za kwao. Tafiti zifanane na za kwao. Sio utumwa huu ni nini?
 
Ufadhili wa project za kuhudumia wagonjwa waukimwi ni mkubwa sana kutoka kwa hao wa 'kisasa' na mashirika yao why! Wao ndo wanatuuzia dawa za ARV. ukimwi ukipata dawa ni msiba mkubwa sana kwao.

Wewe nawe wamekufundisha kwa vitabu vyao na standard zao mpaka umefundishika. Hujui kwmb kitu kuwa kibaya au kizuri inategemeana na vigezo ulivoeka ktk judgement yako?
Standard zao wakoloni usizitumie ivo. Kwani wao wanvobadilisha mti kuwa kidonge cheupe wanaweka nini?
 
Hakuna dawa isiyo na madhara (be it side effect or contraindication), tatizo la fani ya kienyeji kwasasa inaingiliwa na waganga feki wasio na utafiti. Nakuambia ukweli, mganga wa zamani alikuwa akirithi dawa iliyotafitiwa na babu au bibi yake na kuonekana kwanza haina madhara makubwa kwa mtumiaji lakini pili inasaidia kumaliza tatizo lake. Nalaumu kitengo cha tiba asili Muhimbili kusubiri waganga wa kienyeji wapeleke dawa zao pale badala ya kuwafuata waliko ili ijionee maajabu ya dawa za kienyeji. by the way, dawa zote karibu zinatokana na miti shamba....ila ilyotafitiwa...maana hata sumu nyingi pia zinatokana na miti shamba...na ndiyo dawa za kienyeji.
 
Wazungu wameleta kamtindo ka kuwapumbaza weusi ili muamini kila cha kwao ni bora kuliko chenu lakini nataka nikuhakikishie wamama wa vijijini kama masuala ya msosi yuko vizuri kwanza mda wote wa ujauzito huwezi mkuta eti kachoka,mara homa wala nini,wanapiga jembe,wanatembea kama hana mzigo wowote ule mpaka anajifungua na siku akijifungua kesho yake utamkuta anaendelea na shughuri zao poa ..wako strong sana na afya,na hata wakati anajifungua ni safe zaidi kuliko mijini make siku hiyo mama kazungukwa na mabibi kama 4 na akina mama ambao wamewahi kuzaa vizazi 7 kwahiyo wanaelewa A-Z na hata mjamzito unahisi uko salama kuliko mijini manesi2 na hata kuzaa wao hawajawahi alafu ndo kwanza wana miezi6 kazini,ndo maana wanashindwa kuzalisha salama sababu hawana uzoefu wa complications za kuzalisha watu tofauti na mazingira tofauti
 
Akina mama wenye ujauzito nendeni Kagera ama waagizeni ndugu zenu kipindi hiki cha X-mas walioko huko wakirejea wawajie na dawa za kienyeji zipo maalumu na miezi yote 9 unajifungua salama kabisa tena mwanao anakuwa na brain nzuri kwani maziwa ya mama yake yanakuwa hayajachanganyikana sana na sumu za madawa ya kizungu ..aliye tayari afanye hivyo!
 

Sawa wao ndio wanatuletea ARV, je unafahamu kuwa vifo vingi vya ukimwi vimepungua kutokana na matumizi ya ARV hizo hizo zinazotoka kwa wazungu? Au kwa vigezo vyako kupungua kwa vifo ni jambo baya?
Hayo madawa ya kienyeji ya kubahatisha bahatisha, kutoka huko Bukoba, yalishindwaje kuzuia vifo vya ukimwi miaka ya 1980 na 90? Unafahamu familia zilivyopukutika kule Muleba, biharamulo na Bukoba? kutokana na HIV? Acheni kukaririshwa na junk science za akina Ndodi. Wewe mwenyewe hapo kichwa kikiuma sana utakimbilia panado/ na aspirin. Kwanini usinywe mamizizi yenu hayo yasiyo na dose?
 

Hizo ni myth tu.
Hata huko Kagera pamoja na hizo dawa bado kuna vifo vya wazazi wakati wa kujifungua. Maternal deaths zipo dunia nzima.
Na hata sehemu zingine hapa nchini na duniani, kuna wazazi wanajifungua salama na watoto wanakuwa na brain safi bila kutumia madawa yoyote. Ushahidi wa "kagera" hutoshelezi kuthibitisha kuwa madawa ya kienyeji hayana madhara.
 
tulifanywa soko na wazungu mbaya zaidi ni soko la fikra ambalo walituamnisha ya kuwa chochote chetu ni dhambi na duni ili vyao vya viwandani vipate soko, nilipata vidonda vya tumbo kutokana na dawa hizohizo za viwandani nilizo andikiwa na aoao madaktari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…