Madawa ya kulevya: Mtanzania afia Dubai, wengine wadaiwa kukamatwa China na Brazil

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
Kwa wiki iliyopita, tuilipekenyua maeneo yote muhimu na kukumbana na mambo mapya kuhusu habari za ‘unga' huku taarifa zikionesha kuwa, hali katika viwanja vye ndege duniani kote ni tete. Tuhuma za Watanzania kukamatwa au kufariki kutokana na madawa ya kulevya bado zinaendelea kuongezeka. Kwenye hii thread kuna tuhuma tatu zinazowahusu Watanzania, mmoja inadaiwa amefariki baada ya mzigo kupasukia tumboni na wengine wawili wanadaiwa kukamatwa kwenye nchi za watu wakiwa na mzigo.

Mtanzania afia Dubai akiwa na unga tumboni

Habari zilizotufikia juzi zinadai kwamba Mtanzania aliyejulikana kwa jina moja la Chambuso amefariki dunia katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kutokana na unga aliokuwa ameubeba tumboni kuyeyuka kabla ya kufika kwenye kituo husika. Habari za uhakika kutoka chanzo chetu jijini Dar zinasema kuwa marehemu Chambuso alikuwa na ‘mlinzi' wake ndani ya Ndege ya Emirate huku akiwa hamjui.

Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kushuka jijini Dubai, hali ya Chambuso ilianza kubadilika akilalamikia zaidi maumivu ya tumbo, ndipo ‘mlinzi' huyo alipombeba na kumpeleka hospitali (haikutajwa jina). "Baada ya kufariki dunia, jamaa (mlinzi) alijiweka mbele akitaka kufanya maarifa kwa madaktari ili tumbo la jamaa lipasuliwe atoe mzigo. Akashtukiwa, akakimbia na mpaka sasa maiti hiyo iko chini ya ulinzi wa serikali," kilisema chanzo hicho.

Mtanzania aliyekamatwa na unga China

Tukiachana na kifo cha Chambuso huko Dubai, Septemba 2, mwaka huu zilitufikia taarifa kwamba, mchumba wa mwigizaji Pendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus' aliyejulikana kwa jina moja la Tasha amedakwa na unga nchini China. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tasha alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing nchini humo akiwa na unga aina ya heroin (kiasi na thamani hakikutajwa).

Ili kupata uhakika wa madai hayo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta Pendo kwa njia ya simu ya mkononi na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri. "Yeah, ishu ni kweli. Mimi nilizipata hizo taarifa kutoka kule nikawaambia ndugu zake. Kwa mujibu wa mtu wake aliyekuwa naye kule (China) jamaa (Tasha) ameshapandishwa kortini," alisema Pendo huku akisema uchumba wake na Tasha ulishakufa.

Msanii wa Bongo Movie adaiwa kufungwa Brazil

Wiki mbili sasa, mapaparazi wetu wamekuwa wakifuatilia kwa undani kuhusu kusambaa kwa madai kwamba, staa wa filamu za Kibongo, Aisha Bui eti kafungwa miaka 5 jela katika gereza moja nchini Brazil baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye kibegi. Kwa mujibu wa madai ya habari hizo, eti Aisha alidakwa kwenye uwanja wa ndege wa jijini Brasilia akirejea Bongo kupitia Dubai.

Septemba 2 na 5, mwaka huu, waandishi wetu walifika nyumbani kwa baba wa Aisha, Kigamboni, Dar kutaka kujua ukweli. Septemba 2, mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema Aisha yupo Brazil lakini hakuna mawasiliano naye na alikwenda siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Julai mwaka huu. Septemba 5, hakukutwa mtu ila majirani walielekeza eneo analopatikana mzee huyo ambapo ni ufukweni. Hata hivyo, sehemu hiyo hakupatikana na waandiishi waliacha namba zao za simu.

Jioni, mzee Bui alizipata namba zilizoachwa, na saa 9:00 usiku wa kuamkia Septemba 6 alimpigia simu mwandishi wetu na kumvurumishia matusi huku akisema akome kumfuatafuata akidai yeye hana mawasiliano na binti yake tangu mwaka 2007. Mzee huyo alikwenda mbele zaidi kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwenye simu ya paparazi akitumia lugha ya Kiarabu ambapo kwa mujibu wa wataalam wa lugha hiyo ni dua ya kumwombea mabaya mwandishi huyo.

Mnaigeria aliyekamatwa na unga alitahadharishwa na wenyeji wake magomeni asipitie JNIA.

Anthonie Ojo, raia wa Nigeria aliyekamatwa Septemba 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar (JNIA), akijaribu kusafirisha kete 99 za unga na ndege ya Shirika la Ethiopian Airways alinaswa. Mwanamke huyo aliyevalia baibui akidai anakwenda kuhiji Maka, anadaiwa aliununua mzigo huo Magomeni-Mapipa jijini Dar. Aliziweka kete hizo kwenye makopo yaliyokuwa na poda ya Johnson.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, wenyeji waliomuuzia unga mwanamke huyo walimtahadharisha kuhusu hali ya ulinzi iliyopo sasa JNIA hasa baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kushikia bango udhibiti wa unga lakini mtuhumiwa huyo alidaiwa kusema atapita kwa anavyojua yeye.

Nzowa azungumzia

Ili kwenda mbele zaidi, mapaparazi wetu walikwenda ofisini kwa Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ili kutaka kujua kama amesikia lolote kuhusu Aisha Bui. Alisema: "Eee, kuna habari kama hiyo lakini si rasmi kwangu, bado nafuatilia Brazil ikiwa tayari nitawajulisha tu." Tulimtafuta Aisha kwenye mitandao, hasa Facebook, Instagram na Twitter bila mafanikio. Tumemwachia ujumbe kwa kuamini kwamba akirudi hewani ataukuta na kujibu lakini wapi!

Chanzo: TheChoice: MSANII WA BONGO MOVIE 'AISHA BUI' AFUNGWA BLAZIL,MCHUMBA WA PENDO WA MAISHA PLUS AKAMATWA CHINA NA MBWANA MATUMLA AKAMATWA NCHINI HISPANIA....
 
Ooooh mzigo ukiutia kwenye suitcase then ukaupaka mafuta ya simba eti mbwa anaukimbia na hataki kuunusa na unapeta. Mara sijui ukienda kufanyiwa makarama kwa waganga hutasumbuliwa kwenye airport yoyote.
Haya ndio matokeo yake haya
 
Tatizo ni kutaka maisha mazuri kwa njia za mkato
 
Ooooh mzigo ukiutia kwenye suitcase then ukaupaka mafuta ya simba eti mbwa anaukimbia na hataki kuunusa na unapeta. Mara sijui ukienda kufanyiwa makarama kwa waganga hutasumbuliwa kwenye airport yoyote.
Haya ndio matokeo yake haya

JF takuwa jukwaa la hovyo sana km mods wanaanza kushindana na wachangiaji kwa kuondoa threads na kuweka nyingine zenye ujumbe sawa...wengine huenda mbali kupiga ban kwa sababu za kuchekesha.Mengi sana nimetahadharisha humu ndani ila kuna mods wakiingia tuu...

Niliwahi andika humu ndani kuwa mara nyingi hawa punda km uchunguzi haujafanyika basi mashirika ya kimarekani huwa hayatibui , huwaashi ili waweze track mapapa..muda wote huo hawa punda huw ana impressive track records hadi mapapa kuwaamini sana,kuwa ni moto ktk kuruka vihunzi....na kwa nchi km zetu punda huamini vitu ulivyovitaja hapa....

Niliandika kuwa isku nchi fulani zikianza daka punda basi Mapapa bongo wajue wanakaribiwa, na hata km walidhani wanapiga issue na wamarekani, wajue wenzao walicheza ktk namna wakiingia mahakamani hawatashindwa na kuigharibu serikali yao...

Haha..sasa mbwa wa kizugu wamejifunza wapi simba?na km wanamjua ni wazi watakavyo jibehave mbele ya mshukiwa basi askari watajiuliza kwanini mbwa wao kawa mwoga....ila kuna ex-rays za siri ,zinawekwa kuepeusha raia kulia mionzi na privacy.
 
Madawa ya Kulevya:
Aisha Bui (mke mwenza
na Amina chifupa) nae
akamatwa Brazil .
kwenye katiba mpya tuweke ni ruksa raia kuuza sembe popote duniani
 
Kwa wiki iliyopita, tuilipekenyua maeneo yote muhimu na kukumbana na mambo mapya kuhusu habari za ‘unga' huku taarifa zikionesha kuwa, hali katika viwanja vye ndege duniani kote ni tete. Tuhuma za Watanzania kukamatwa au kufariki kutokana na madawa ya kulevya bado zinaendelea kuongezeka. Kwenye hii thread kuna tuhuma tatu zinazowahusu Watanzania, mmoja inadaiwa amefariki baada ya mzigo kupasukia tumboni na wengine wawili wanadaiwa kukamatwa kwenye nchi za watu wakiwa na mzigo.

Mtanzania afia Dubai akiwa na unga tumboni

Habari zilizotufikia juzi zinadai kwamba Mtanzania aliyejulikana kwa jina moja la Chambuso amefariki dunia katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kutokana na unga aliokuwa ameubeba tumboni kuyeyuka kabla ya kufika kwenye kituo husika. Habari za uhakika kutoka chanzo chetu jijini Dar zinasema kuwa marehemu Chambuso alikuwa na ‘mlinzi' wake ndani ya Ndege ya Emirate huku akiwa hamjui.

Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kushuka jijini Dubai, hali ya Chambuso ilianza kubadilika akilalamikia zaidi maumivu ya tumbo, ndipo ‘mlinzi' huyo alipombeba na kumpeleka hospitali (haikutajwa jina). "Baada ya kufariki dunia, jamaa (mlinzi) alijiweka mbele akitaka kufanya maarifa kwa madaktari ili tumbo la jamaa lipasuliwe atoe mzigo. Akashtukiwa, akakimbia na mpaka sasa maiti hiyo iko chini ya ulinzi wa serikali," kilisema chanzo hicho.

Mtanzania aliyekamatwa na unga China

Tukiachana na kifo cha Chambuso huko Dubai, Septemba 2, mwaka huu zilitufikia taarifa kwamba, mchumba wa mwigizaji Pendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus' aliyejulikana kwa jina moja la Tasha amedakwa na unga nchini China. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tasha alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing nchini humo akiwa na unga aina ya heroin (kiasi na thamani hakikutajwa).

Ili kupata uhakika wa madai hayo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta Pendo kwa njia ya simu ya mkononi na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri. "Yeah, ishu ni kweli. Mimi nilizipata hizo taarifa kutoka kule nikawaambia ndugu zake. Kwa mujibu wa mtu wake aliyekuwa naye kule (China) jamaa (Tasha) ameshapandishwa kortini," alisema Pendo huku akisema uchumba wake na Tasha ulishakufa.

Msanii wa Bongo Movie adaiwa kufungwa Brazil

Wiki mbili sasa, mapaparazi wetu wamekuwa wakifuatilia kwa undani kuhusu kusambaa kwa madai kwamba, staa wa filamu za Kibongo, Aisha Bui eti kafungwa miaka 5 jela katika gereza moja nchini Brazil baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye kibegi. Kwa mujibu wa madai ya habari hizo, eti Aisha alidakwa kwenye uwanja wa ndege wa jijini Brasilia akirejea Bongo kupitia Dubai.

Septemba 2 na 5, mwaka huu, waandishi wetu walifika nyumbani kwa baba wa Aisha, Kigamboni, Dar kutaka kujua ukweli. Septemba 2, mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema Aisha yupo Brazil lakini hakuna mawasiliano naye na alikwenda siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Julai mwaka huu. Septemba 5, hakukutwa mtu ila majirani walielekeza eneo analopatikana mzee huyo ambapo ni ufukweni. Hata hivyo, sehemu hiyo hakupatikana na waandiishi waliacha namba zao za simu.

Jioni, mzee Bui alizipata namba zilizoachwa, na saa 9:00 usiku wa kuamkia Septemba 6 alimpigia simu mwandishi wetu na kumvurumishia matusi huku akisema akome kumfuatafuata akidai yeye hana mawasiliano na binti yake tangu mwaka 2007. Mzee huyo alikwenda mbele zaidi kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwenye simu ya paparazi akitumia lugha ya Kiarabu ambapo kwa mujibu wa wataalam wa lugha hiyo ni dua ya kumwombea mabaya mwandishi huyo.

Mnaigeria aliyekamatwa na unga alitahadharishwa na wenyeji wake magomeni asipitie JNIA.

Anthonie Ojo, raia wa Nigeria aliyekamatwa Septemba 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar (JNIA), akijaribu kusafirisha kete 99 za unga na ndege ya Shirika la Ethiopian Airways alinaswa. Mwanamke huyo aliyevalia baibui akidai anakwenda kuhiji Maka, anadaiwa aliununua mzigo huo Magomeni-Mapipa jijini Dar. Aliziweka kete hizo kwenye makopo yaliyokuwa na poda ya Johnson.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, wenyeji waliomuuzia unga mwanamke huyo walimtahadharisha kuhusu hali ya ulinzi iliyopo sasa JNIA hasa baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kushikia bango udhibiti wa unga lakini mtuhumiwa huyo alidaiwa kusema atapita kwa anavyojua yeye.

Nzowa azungumzia

Ili kwenda mbele zaidi, mapaparazi wetu walikwenda ofisini kwa Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ili kutaka kujua kama amesikia lolote kuhusu Aisha Bui. Alisema: "Eee, kuna habari kama hiyo lakini si rasmi kwangu, bado nafuatilia Brazil ikiwa tayari nitawajulisha tu." Tulimtafuta Aisha kwenye mitandao, hasa Facebook, Instagram na Twitter bila mafanikio. Tumemwachia ujumbe kwa kuamini kwamba akirudi hewani ataukuta na kujibu lakini wapi!

Chanzo: TheChoice: MSANII WA BONGO MOVIE 'AISHA BUI' AFUNGWA BLAZIL,MCHUMBA WA PENDO WA MAISHA PLUS AKAMATWA CHINA NA MBWANA MATUMLA AKAMATWA NCHINI HISPANIA....
Naona hili suala linakuwa siku zinavyozidi kwenda ,ila ndio madhara ya kuwa na serekali legelege
 
Hivi kwani big deal ya hayo madawa ni nini hasa?

Kwa nini yana bei hivyo? Kwani ni mazuri sana ukiyatumia?

Manake sielewi kabisa....
 
.
Kwa spidi hii ... itabidi nchi yetu imteue Balozi maalum wa kushughulikia madawa ya kulevya.

Huyu Balozi itabidi awe anafuatilia huko nchi za nje kujua watanzania wangapi wamekamatwa, waliokufa kwa kupasukiwa na madawa, je maiti zao zitarudi au, waliofungwa ni wangapi n.k

Maana serikali inaonekana haipo serious katika mapambano ya madawa ya kulevya! ... basi mteueni Balozi wa Madawa ya kulevya .. then tujue moja!
 
Aisha BUI.jpg
Masikini Aisha Bui kwa nini uliamua kuendeleza Biashara aliyokuwa akifanya Mpakanjia ona sasa yaliyokukuta.
 
Kwa wiki iliyopita, tuilipekenyua maeneo yote muhimu na kukumbana na mambo mapya kuhusu habari za ‘unga’ huku taarifa zikionesha kuwa, hali katika viwanja vye ndege duniani kote ni tete. Tuhuma za Watanzania kukamatwa au kufariki kutokana na madawa ya kulevya bado zinaendelea kuongezeka. Kwenye hii thread kuna tuhuma tatu zinazowahusu Watanzania, mmoja inadaiwa amefariki baada ya mzigo kupasukia tumboni na wengine wawili wanadaiwa kukamatwa kwenye nchi za watu wakiwa na mzigo.

Mtanzania afia Dubai akiwa na unga tumboni

Habari zilizotufikia juzi zinadai kwamba Mtanzania aliyejulikana kwa jina moja la Chambuso amefariki dunia katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kutokana na unga aliokuwa ameubeba tumboni kuyeyuka kabla ya kufika kwenye kituo husika. Habari za uhakika kutoka chanzo chetu jijini Dar zinasema kuwa marehemu Chambuso alikuwa na ‘mlinzi’ wake ndani ya Ndege ya Emirate huku akiwa hamjui.

Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kushuka jijini Dubai, hali ya Chambuso ilianza kubadilika akilalamikia zaidi maumivu ya tumbo, ndipo ‘mlinzi’ huyo alipombeba na kumpeleka hospitali (haikutajwa jina). “Baada ya kufariki dunia, jamaa (mlinzi) alijiweka mbele akitaka kufanya maarifa kwa madaktari ili tumbo la jamaa lipasuliwe atoe mzigo. Akashtukiwa, akakimbia na mpaka sasa maiti hiyo iko chini ya ulinzi wa serikali,” kilisema chanzo hicho.

Mtanzania aliyekamatwa na unga China

Tukiachana na kifo cha Chambuso huko Dubai, Septemba 2, mwaka huu zilitufikia taarifa kwamba, mchumba wa mwigizaji Pendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’ aliyejulikana kwa jina moja la Tasha amedakwa na unga nchini China. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tasha alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing nchini humo akiwa na unga aina ya heroin (kiasi na thamani hakikutajwa).

Ili kupata uhakika wa madai hayo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta Pendo kwa njia ya simu ya mkononi na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri. “Yeah, ishu ni kweli. Mimi nilizipata hizo taarifa kutoka kule nikawaambia ndugu zake. Kwa mujibu wa mtu wake aliyekuwa naye kule (China) jamaa (Tasha) ameshapandishwa kortini,” alisema Pendo huku akisema uchumba wake na Tasha ulishakufa.

Msanii wa Bongo Movie adaiwa kufungwa Brazil

Wiki mbili sasa, mapaparazi wetu wamekuwa wakifuatilia kwa undani kuhusu kusambaa kwa madai kwamba, staa wa filamu za Kibongo, Aisha Bui eti kafungwa miaka 5 jela katika gereza moja nchini Brazil baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye kibegi. Kwa mujibu wa madai ya habari hizo, eti Aisha alidakwa kwenye uwanja wa ndege wa jijini Brasilia akirejea Bongo kupitia Dubai.

Septemba 2 na 5, mwaka huu, waandishi wetu walifika nyumbani kwa baba wa Aisha, Kigamboni, Dar kutaka kujua ukweli. Septemba 2, mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema Aisha yupo Brazil lakini hakuna mawasiliano naye na alikwenda siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Julai mwaka huu. Septemba 5, hakukutwa mtu ila majirani walielekeza eneo analopatikana mzee huyo ambapo ni ufukweni. Hata hivyo, sehemu hiyo hakupatikana na waandiishi waliacha namba zao za simu.

Jioni, mzee Bui alizipata namba zilizoachwa, na saa 9:00 usiku wa kuamkia Septemba 6 alimpigia simu mwandishi wetu na kumvurumishia matusi huku akisema akome kumfuatafuata akidai yeye hana mawasiliano na binti yake tangu mwaka 2007. Mzee huyo alikwenda mbele zaidi kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwenye simu ya paparazi akitumia lugha ya Kiarabu ambapo kwa mujibu wa wataalam wa lugha hiyo ni dua ya kumwombea mabaya mwandishi huyo.

Mnaigeria aliyekamatwa na unga alitahadharishwa na wenyeji wake magomeni asipitie JNIA.

Anthonie Ojo, raia wa Nigeria aliyekamatwa Septemba 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar (JNIA), akijaribu kusafirisha kete 99 za unga na ndege ya Shirika la Ethiopian Airways alinaswa. Mwanamke huyo aliyevalia baibui akidai anakwenda kuhiji Maka, anadaiwa aliununua mzigo huo Magomeni-Mapipa jijini Dar. Aliziweka kete hizo kwenye makopo yaliyokuwa na poda ya Johnson.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, wenyeji waliomuuzia unga mwanamke huyo walimtahadharisha kuhusu hali ya ulinzi iliyopo sasa JNIA hasa baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kushikia bango udhibiti wa unga lakini mtuhumiwa huyo alidaiwa kusema atapita kwa anavyojua yeye.

Nzowa azungumzia

Ili kwenda mbele zaidi, mapaparazi wetu walikwenda ofisini kwa Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ili kutaka kujua kama amesikia lolote kuhusu Aisha Bui. Alisema: "Eee, kuna habari kama hiyo lakini si rasmi kwangu, bado nafuatilia Brazil ikiwa tayari nitawajulisha tu." Tulimtafuta Aisha kwenye mitandao, hasa Facebook, Instagram na Twitter bila mafanikio. Tumemwachia ujumbe kwa kuamini kwamba akirudi hewani ataukuta na kujibu lakini wapi!

Chanzo: TheChoice: MSANII WA BONGO MOVIE 'AISHA BUI' AFUNGWA BLAZIL,MCHUMBA WA PENDO WA MAISHA PLUS AKAMATWA CHINA NA MBWANA MATUMLA AKAMATWA NCHINI HISPANIA....

Watanzania wanapenda sana magendo!! Yaani hata kama madawa ya kulevya yangekuwa legal bado wangetafuta biashara yoyote ya kuibia!! Kukwepa kodi kunaicost nchi jamani na wanaoathirika ni wanajamii wenzetu
 
Nchi ikipuuza tu ELIMU. Au kutoa elimu isiyo sahihi matokeo yake ndo haya. Hili tunalo.. naona bora serikali isimamishe yote iwekeze KIUKWELI kwenye ELIMU.
Bila hivyo.. mtaniambia.
 
Huu sasa ni udhalilishaji wa nchi yetu na hata watu wasafi watakuwa wanakaguliwa sasa kana kwamba ni walewale wasafirishaji.

Hebu acheni hizo, hata kama ni pesa jaribuni kufikiria ishu nyingine ya kufanya kupata pesa wandugu.
 
wamemkosea nini Mungu mbona wanamikosi hivyo
 
Back
Top Bottom