Madawa ya Kulevya

Madawa ya Kulevya

kizaizai

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
5,651
Reaction score
6,966
Wana JF naomba msaada wenu nifanyenini? Ndugu yangu miaka 27 (male) anatumia Bangi na Unga(heroin au cocaine). kama familia tumejitahidi sana kumsaidia naona tunashindwa, sasa amefikia hatua ya kutembea bila viatu barabarani na kulala chini ya madaraja Ubungo. Tunahisi anaelekea kwenye ukichaa. Please Bandungu naomba ushauri wenu ili nduguyangu aweze kupona.
 
kama cash ipo kidogo jaribu kumpleka kwenye vituo vya counselling vinavyohusika na madawa ya kulevya,kule atapata msaada,ilasifahamu vipo wapi.
 
Nikupe ujanja? Mkamatisheni kwa kesi halafu ongea na mwendesha mashtaka na hakimu...........wampige jela miezi kama sita, huko hatavuta huo unga na hata kama atapata bangi ni kwa kiasi kidoogo.Akitoka hamu ya unga imepungua halafu mnampeleka kwenye kituo cha ukarabati.

Ni kama masikhara lakini inasaidia sana!
 
Mkuu platozoom Umezungumza Point huku nje hivyo hivyo Wavuta Unga huwa wanafungwa kiasi cha mwaka mmoja kisha ndio wanapelekwa hospitali kwa matibabu.Hiyo ndio njia nyepesi kuliko kumpeleka hospitali watatumia pesa zao bure wazazi na hata acha kuvuta Unga.
 
Last edited by a moderator:
Wana JF naomba msaada wenu nifanyenini? Ndugu yangu miaka 27 (male) anatumia Bangi na Unga(heroin au cocaine). kama familia tumejitahidi sana kumsaidia naona tunashindwa, sasa amefikia hatua ya kutembea bila viatu barabarani na kulala chini ya madaraja Ubungo. Tunahisi anaelekea kwenye ukichaa. Please Bandungu naomba ushauri wenu ili nduguyangu aweze kupona.

Mkuu kizaizai, Pole.

Yuko mkoa gani, shughuli yake ...na kwa muda gani amekuwa akitumia vilevi?
-Je, amekuwa akitumia kiasi gani cha vilevi/vileo?
-Ni muda gani(mrefu) alikwisha wahi kukaa bila kutumia dawa?
-Na je, mtazamo wake ni upi baada ushauri wenu?
 
Last edited by a moderator:
Waulize wale wote waliotoka hizo jela watakwambia kitu wanachokosa huko ni uhuru tu!,lakini vitu vyote vipo mle ndani,hata huo unga umejaa tele,Watu wanasema mtu akikudhulumu muombee kwa muumba awe mla unga,yaani mateso atayapata yeye na ndugu zake wote.Ndio hili tunaloliona hapa.
 
Mkuu platozoom Umezungumza Point huku nje hivyo hivyo Wavuta Unga huwa wanafungwa kiasi cha mwaka mmoja kisha ndio wanapelekwa hospitali kwa matibabu.Hiyo ndio njia nyepesi kuliko kumpeleka hospitali watatumia pesa zao bure wazazi na hata acha kuvuta Unga.

Wakuu MziziMkavu, platozoom,

Just to remind you, nje si sawa na huku...i think you underestimate the power ya addiction or drug withdrawal by physical measures!
-Pili, Ulinzi uko mzuri and esp. maximum security penitentiaries..tofauti na huku kwetu, "deal" kuchezwa na maaskari na madawa kupatikana ndani humo humo!
 
Nimeshuhudia hili lilimsaidia mtu, kumbuka hapa hatusemi kwamba hatapata kabisa unga, hata akipata ni kidogo sana (na ofcourse hata huko kwenye rehab siku za mwanzo hawawanyimi kabisa).

lakini pia tofauti na bangi unga kuingizwa magerezani ni kwa wale wenye kipato kizuri kiasi ndio wanapata lakini kwa hyu ambaye ndugu zake watakuwwa wanamcheki mara kwa mara itakuwa ngumu!
 
Kama uko DSM pale kinondoni mkwajuni upande wa kushoto kama unatokea Manyanya au kulia kama unatole amagomeni kuna kituo kimoja ambacho pia kinafanya maombi na counselling kwa hawa waathirika wa madawa. Kinasaidia sana.
 
Thanks...!

Karibu nime edit na post na kueleza jinsi ya kufika ni kituo cha Kinondoni mkwajuni kama unatokea Manyanya ni kushoto au kama unatokea magomeni ni kulia. Wengi wamesaidika sana pale.Pole sana. Ile list yetu ilitua kwa Rais iliishia wapi? Kweli mafisadi hawana huruma na watanzania, watoto wanazidi kuangamia kila siku.
 
Nimeshuhudia hili lilimsaidia mtu, kumbuka hapa hatusemi kwamba hatapata kabisa unga, hata akipata ni kidogo sana (na ofcourse hata huko kwenye rehab siku za mwanzo hawawanyimi kabisa).

lakini pia tofauti na bangi unga kuingizwa magerezani ni kwa wale wenye kipato kizuri kiasi ndio wanapata lakini kwa hyu ambaye ndugu zake watakuwwa wanamcheki mara kwa mara itakuwa ngumu!

Mkuu, nadhani issue kubwa ni motive...yaani kwa nini anaenda Rehab na kwa nini anaenda gerezani!!
In Rehab..kunakitu tunaita psyche orientation na ndio maana kuuliza maswali hapo juu kwa mtoa thread(hayajibiwa bado).

Mara nyingi tunasahau kuwa with drugs adiction, someone is "compelled" to do anything ili apate dawa..and i literally mean ANYTHING..sasa kwa gerezani( forget abt the motive) unaongeza matatizo mengine zaidi(hasa kama mtu hajiwezi)..vitendo vya ulawiti n.k hutokea!
 
Mkuu platozoom Umezungumza Point huku nje hivyo hivyo Wavuta Unga huwa wanafungwa kiasi cha mwaka mmoja kisha ndio wanapelekwa hospitali kwa matibabu.Hiyo ndio njia nyepesi kuliko kumpeleka hospitali watatumia pesa zao bure wazazi na hata acha kuvuta Unga.

bila undava kutumika kwanza basi kwa kiwango hichi huyo jamaa haponi ni lazima undava wa namna hiyo utumuke kwanza then akitoka ndo apigwe rehab.
 
Back
Top Bottom