Made in Tanzania

Hauna kazi ya kufanya Nini?

Watu wenye akili nzuri ya kuweza kuendesha viwanda vya namna hiyo utawapata wapi hapa Tanzania??
 
Made in Tanzania ni aibu, mtu kaka chuo miaka mitatu . Kapigwa matheories kibao ya kina malthus sijui kina mafalsafa ya kina secretes. Anakuja kutengeneza kiatu cha plastiki mpaka kamba 😂
Kiatu ukivaa bila soksi kinakata kama kiwembe. Waafrika tuna lana wallahi
 
Interesting
 
Tanzania iliwahi kubahatika kuwa na Rais mmoja tu aliyekuwa na maono! Bahati mbaya na yeye aliamini kwenye sera moja tu, na ya kufikirika ya Ujamaa!!

Angechanganya mazuri machache ya Ujamaa na mazuri machache ya Ubepari kama walivyofanya China miaka ya 1970's; huenda na sisi leo hii tungekuwa kama China, Korea, au Singapore.
 
Sio kosa kutengeneza viatu vya plastic
 
Maono mazuri Dennis...

PIA,

Fanya mazoezi ya umodelishi wa viwanda vidogo vidogo halafu viwe ndani ya mtandao wa viwanda vya 'ukubwa wa kati' na 'ukubwa kabisa' halafu ushiriki mawazo.

Japo uadilifu na usanifu wako unajikita kwenye 'kutengeneza fedha na ajira kwa jamii ya Watanzania fanya mazoezi ya kuimajinisha sura ya namna ya 'uchumi wa kazi'.

Namna ya kuuona uchumi wa kazi: fikiria namna tofauti ya wanajamii kustawi pasipo dhana khasa za 'fedha ama kujenga ukwasi' bali kujishughulisha kwa ajili ya mahitaji yao ya karibu na muhimu ya kila siku--pesa inaweza kuwa ni matokeo tu; ama umiminishi wa hazina/pumzi/mtaji wa shughuli...

Mahitaji ya karibu na muhimu, ukiyaotea, yataelekea kwenye ujenzi/uboreshaji/uendelezaji wa makazi na uzashalishaji wa vyakula, bidhaa za chakula, madawa n.k -- pia mavazi.

Jenga ujuzi wa matumizi ya 'Akili Bandia' ili kuchungua mipangilio ya shughuli na mahitaji ya ujuzi ama/na kujengea ujuzi kwa wadau wa maendeleo--kwa hivyo hili linataka ujiandae kwa ujenzi wa mtandao wa mafundi wa mipango na mameneja wa miradi...

JITAHIDI KUJENGA MTANDAO WA JUHUDI NA UTENDAJI wa kutimiza maono--watu shughuli zao na maendeleo...

Unaweza, humu humu JF, kuibua mawazo, kufanya utunzi/ubunifu wa mbinu-kazi, na basi kuratibu vitendo kwa ajili ya uendelezi wa vipaji na uwezo wa kujisuka kitaasisi--kugema utayari wa wanajamii wenzako wanaoweza kuwa na dhamira na mapenzi ya kuleta mabadiliko katika jamii.

Unahitaji ujuzi na utundu wa kujipangilia na kujisukuma mbele kitaasisi; hili linakutaka uzingatie matumizi bora ya rasilimali zozote zilizopo na tena uwe na ujuzi na upeo kubaini vipaji, ujuzi na umahili wa wengine unaoweza kuwafikia/wakakufikia.

Chukulia kuwa JF inaweza kuwa ni sehemu mojawapo ya wewe kuweza kuwafikia/kuwapata wadau wa utekelezaji wa maono yaliyoko kwako. Livalie njuga hili suala hili, kinamna hii, ili upate wepesi kuibadilisha sura na mwenendo wa jamii yetu kwa 'Hamadi kibindoni...'

Hmmm​
 
Viwanda vidogo vitakua haraka kama kukiwa na viwanda vya awali mfano kama plastic raw material zitakua zinazalishwa hapa Tanzania itakua ni rahis kutengeneza bidhaa yeyote ya plastic kwa sababu raw material za plastic zipo

Kinachoipa wakati mgumu Tanzania ni raw material zote zinazotakiwa kiwandani tuna-import kutoka nje ya nchi
 
  • Viwanda vya magari
It is the maxim of a every prudent master of a family, never to attempt to make at home what it will cost him more to make than to buy.

Hayo ya viwanda vingine tuwaachie wachina na tununue huko (they are the industry of the World; cha maana let us try to be as sustainable as possible jambo ambalo vitu vidogo tu tunashindwa... Case Study ni sasa hivi tunawapa wana vijiji majiko ya gesi na kununua gesi kutoka nje wakati tuna umeme wa kutosha ambao kila mtanzania anaweza kuzalisha na hata kuuza nje....

Kwahio badala ya viwanda vya magari sijui ndege na ndoto kama hizo tuanze tu kuwauzia Afrika Umeme...

 
UMEKAZA NIA SANA KWENYE 'UZALISHAJI" na UZALISHAJI MALI' KULIKO WATU WENYEWE

Haudhani hivi?

Mdogo mdogo, fanya mazoezi ya 'Kuwaona watu'--watu na mawezekano; haya ya viwanda unaweza 'kuyaweka kiporo'--ama kuyarudia upya unapokuwa na mwangaza bora... Ama kuyasukuma kama 'mpango wa kando'.

Chochote ukifikiriacho, weka watu kama ndiyo 'Taa na Dira' ya maisha na kujichagulia...

Ulimwengu wa leo hili, hutafundishwa hili 'Shuleni' ama 'Chuoni'--huko sana sana mtu/mwanajamm anaweza kugeuzwa 'mtumika' wa 'mifumo ya mali' na 'uzalishaji mali'....

Hili lina mazuri na mabaya yake wakati mmoja hata mwingine--japo kwa ujumla, SI JAMBO BORA kwa maana hili ni shauri rahisi lenye nasibu ya kutweza 'heshima ya utu wa mtu/mwanajamii'...

Mambo ya 'Mnyonge hana Haki' ni tunda bovu la mfumo wa biashara wa jamii; kuna namna yake ya ubayana wenye kuleta hata muktadha akilifu wa kana kwamba: hata wewe unaweza kuwa 'umeathirika na unyonge' -- ndiyo basi maana ya mapelekeo ya dhana rahisi ya kuibuka na madhumuni ya 'made in Tanzania'... hili lawa ni 'shauri la faraja'/kuwazia Tanzania Imara kwa msingi wa viwanda kama vya 'mabeberu'...

Hakuna ubaya kuhusu kudhamiria 'Ubeberu'; sema huu huja kwa utundu na ujuzi wa kuruhusu mifumo ya 'wenyekuwa nacho' na 'wasio nacho' wakati wote... Ni vema kuwa na akili kama beberu, lakini jiongeze ili kujiangazia mawezekano ya Ujamaa.

Ulimwengu ulipo sasa, Ujamaa unawezakana--unahitaji tu 'wanajamii na taasisi zao' kujiongeza--kujua ilivyobora.

Inawezekana kuthubutu kufikiri tofauti...

Kwa hivyo unaweza kuimarisha upeo na uelewa wako juu ya wanajamii na jamii... Maendeleo ni watu halafu vitu; mtaji mkubwa wa jamii ni 'akili zao' kwa hivyo kadiri unanyoshikiri yale yaliyo ndani ya wanajamii wenyewe 'kujiongeza' basi unakuwa umeonesha njia khasa...

Hmmm
 
Hilo ni wazo lako na una-uhuru wa kufikiri hivyo
Ila kwa kupitia wazo lako ni ngumu sana kuondoka kwenye umaskini
Tanzania ni maskini sana
 
Hivyo viwanda labda una-uelewa navyo ila ungekua na uelewa navyo usingeongea ulichoongea

Viwanda vyote hivyo vitagusa watu kwa asilimia mia moja sababu hata mtu wa kawaida anaweza fungua kiwanda sababu raw material zitakua nyingi na zinapatikana hapa hapa na sio kama sahivi raw material zinatoka nje ya nchi
 
Ni wazo zuri, ila matatizo mengi katika nchi za kiafrica yanafanana. Kabla hatujaenda mbali, ni nchi zipi za kiafrika zimefanikiwa kwenye hilo?​
 
Hilo ni wazo lako na una-uhuru wa kufikiri hivyo
Ila kwa kupitia wazo lako ni ngumu sana kuondoka kwenye umaskini
Tanzania ni maskini sana
Haya ya kwanza sio maneno yangu ni maneno aliyosema Adam Smith the father of Modern Economy..., kwamba sio busara kujaribu kutengeneza kitu kwa gharama wakati unaweza kukinunua kwa bei nafuu..., ndio maana niweka magari (kutengeneza magari hata nchi kama UK zimeshindwa na kuacha kutokana na comparative advantages walizonazo nchi nyingine) na hata mkisema mfanye assembling plant ya magari kama Toyota ili yaweze kuuzwa East Africa nadhani nchi zilizotuzunguka zipo more poised kufanya hivyo (South Africa being one)

Haya ya pili nikakuonyesha jambo dogo tu kama la ku-assemble majiko ya umeme na kushusha umeme ili watu wapikie (soko / uhitaji /need) ipo kubwa tu wala hatufanyi hivyo na tunauza product ambayo kuna alternative lakini tunaagiza kutoka nje...

In short kuusu viwanda vya kama nguo sio kwamba havipo..., ila quality na production costs as well as cultural / fashion watu wananunua mitumba (cheaper and more quality) than anything which can be manufactured by the likes of Mwatex et al....
 
Viwanda vya nguo Tanzania sababu hatuna msingi wa viwanda
Mfano hatuna viwanda vikubwa vya spinning ambavyo vitakua vinatengeneza nyuzi (yarn) both za kisasa na za asili zitokanazo na cotton

Tungekua na viwanda imara vya nguo watu wasingeenda china

Ili utengeneze majiko unahitaji uweze kununua steel au chuma kwa bei nafuu sasa Tanzania hatuna smelter za pog iron, aluminium na copper
Matokeo yake chuma (steel) aluminium na copper tunaagiza nje mwisho wa siku gharama za kutengeneza bidhaa jamii ya steel au aluminium zinakua juu matokeo yake hatuwezi shindana na wazalishaji wa nje
Ndo maana kwenye post yangu ya kwanza kuna proposal naandika ya kutengeneza
Pig iron smelter
Aluminium smelter
Copper smelter
Spinning plant
Na nyinginezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…