NIMEKUSOMA, NIMEPATA PICHA
Ahsante,
Ni kweli uholela wa
mabepari na vyombo vyao vya kibiashara, ilivyo pia ni 'watu binafsi'--watu binafsi kitafsiri ya kisheria na mifumo ya kileo, ni mtambo wa kufarakanisha wanajamii kupitia utaasisi wa biashara na maslahi yake ya ubinafsi...
Sasa biashara ni kuuza na kununua, kwa vigezo na masharti vya 'maridhiano ya kimkataba' -- mkataba ilivyo ni makubaliano ya mabadilishano ya bidhaa/kazi/huduma/fedha ili kunufaika na matunda ya kazi, huduma, na umiliki wa mali.
Kiuono na ufikirifu mifumo, biashara ni mahusiano ya kuhamishiana sifa na hadhi za mahitaji ya kimazingira ya 'watu' kwa dhana ya fasili ya '
kiumbe halali cha utendaji wa kibiashara'. Masoko ni muktadha akilifu wa 'makutano ya muuzaji na mnunuzi' katika mapana ya utendaji wa kibiashara.
Inaweza kushangaza, lakini ndiyo ukweli wenyewe wa mambo, utendaji wa kibiashara si lazima uhusishe fedha ama/na uhalali wa '
mali binafsi' kama kiini cha msingi;
matumizi ya fedha na utaasisi wote mzima wa mambo ya fedha ni zao ya wanajamii wenyewe 'kujichagulia' msingi wa maisha, vipewavyo thamani na ustawi wao...
Taasisi zote hupata marefu ya uzima wake na basi mifumo yake kulingana na wastani wa upeo na uwezo wa wanajamii wenyewe kujiamulia hatma za maendeleo, uthamani wa mambo yao na basi ustawi wao...
Ndivyo basi Ubepari hata sasa, kweli, upo kitandani--karibuni kukata roho;
ni kwa utundu na uhuni ubepari unadumishwa katika mapana ya ustawi na uhai wa mataifa.
Ndivyo basi dhana ya
usoshalisti wa kimasoko, kiufundi, ni utundu na maarifa ya kubayanisha mazingira huru ya masoko kama mapana muafaka ya jamii yenyewe kujitosheleza kijamii, maendeleo na ustawi na kumbe 'uholela' wa kusaka faida unashiriki kusudi la fedha na mitaji ili kufaa '
maslahi mapana ya jamii/umma kupitia mashirika yenye hisa za serikali'. Fedha kuwa aseti kimiminika cha ukwasi... Kwa kuwa, kipi kinaweza kuwa ni kizio cha uthamani wa mali ama huduma?
Hili linatukumbusha jambo moja adhimu, ukiondoa hitaji na umuhimu wa sera na vipaumbele vinavyolinda 'maslahi ya jamii', kupitia utendaji wa serikali na dola, wanajamii wenyewe wanahitaji 'kujielewa' na kuwa mstari wa mbele kujisuka kitaasisi kwa ajili ya ustawi na maendeleo yake na tunu zake za thamani kama taifa.
Kwa Tanzania udhamirifu wa ustawi na maendeleo ni fanusi ya tunu za Uhuru, Udugu, Haki na Amani...
Japo mchakato wa kujisuka na kujifuma kitaasisi, kwa jamii ya tuseme watu wapatao milioni sitini (60) yaweza kuchukua muda mrefu; uhitaji wa wanajamii wanaojielewa kulisukuma jahazi la utaasisi bora wa sura ya nchi na tawala uko pale pale...
Uongozi ni kuonesha njia, kuongoza njia ni Utaasisi...
Hili kwa jamii yetu wa watanzania linatukumbusha 'kutokulala na kuwa macho'--kwa maana bado kuna 'mapambano'....
Nchi yetu kuwa na msingi ya Ujamaa na Kujitegemea,
jambo hili linatutaka sana wanajamii tuwe mstari wa mbele kuzitawala 'siasa za nchi'; kufanya hivi kwa kushirikiana na wale tunaowapa madaraka katika jamii.
Watu wa madaraka ni vitovu vyetu vya mienendo ya maisha na kujichagulia; Ujamaa ni mwenendo wa maisha na si 'Utaasisi wa Miundo-utendaji-Jamii ya namna za watoa Amri na Wapokea Amri'...
Kwa minajili ya hivi,
demokrasi na ujamaa tukiwa na uono na ufikirifu mifumo, yawezakuwa jambo hili ni muktadha akilifu wa ufanyaji maamuzi juu ya taasisi zetu za umma na tena ustawi wa jamii ili kuleta hata 'Mapinduzi'--mapinduzi ya mifumo ya biashara huria inayotawala biashara globali...
Kwa hivyo
tunaweza sisi kwa sisi, kama wananchi wenyenchi, tukapeana mwangaza kwamba muktadha wetu wa masoko na biashara vifuate utoshelezaji wa mahitaji na stara ya jamii kiuchumi na mazingira. Kila mtu awe na cha kufanya ili kuifikia ndoto ya maisha bora kwa kila mtanzania.
Katika ulimwengu wa leo, uwezekano upo wa kupangilia kishughuli/biashara na masoko kwa ajili ya manufaa ya wanajamii wote!
Matumizi ya akili bandia yanaweza kurahisisha hili, mtu yeyote asijidanganye ama kujipotosha kana kwamba kujifikirsha: mbona nchi zilizoendelea na hata kuleta maendeleo ya tekinolojia za Akili Bandia yenyewe hawawi 'Wasoshalisti'(?)
Akili Bandia inaweza kuchochea Ujamaa na kuleta mapinduzi makubwa duniani--
hili la kukwamisha uwezekano huu LINARATIBIWA na 'wanaojijua' ili lisichukue upesi mkondo huu.
Kwa hivyo
iko namna tunaweza kulimulika hili na kuonesha mawekano hata ya 'Mapinduzi' kwa matumizi ya Akili Bandia na Utengeneaji wa Kijamii. Hili linatutaka sana tuwe na uono na ufikirifu mifumo, kwa kuwa Akili Bandia nayo hutenda kwa Uono na Ufikirifu Mifumo....
Akili Bandia inaweza kubadilisha mfumo dume wa kiuchumi kuwa '
Mfumo mama wa Uchumi'...
Uchumi wa kazi ni muktadha akilifu wa 'Uchumi Mama' na hali Ubepari ni mfumo dume wa 'Uchumi Biashara'...
SASA, kamwe tusidhani tunahitaji kuona mahala huo uchumi mama halafu 'tudese...'
Wasomi wetu mashudu, hapa ndipo wanapotuangusha kwa kadiri ya wao kuwa ni watumishi wenyedhamana ya utendaji--utendaji wa hata kiserikali; na huku hawathubutu 'kulivumbua gurudumu jipya la maendeleo ya watu--watu na vitu'...
Kwa hivyo
usanifu miundo ya utendaji wa kijamii kwa kutumia akili bandia unaweza kuwa unakamia kuvunja utendaji mpana kuwa utendaji wa kimafungu madogo madogo mengi yanayohodhiwa na utendanji wa wanajamii inaweza kuwa ni suluhu ya kuondokana na mifumo dume ya uchumi mauti wa kibepari wa leo...
Jamii yetu na dunia yetu inahitaji kuhama kiparadaimu ya utu na maendeleo ya kweli...
Fedha si msingi wa maendeleo, akili na watu wenyekujielewa wanaweza kuifumua na pia kuufuma mfumo wowote pale ule wa awali unaoishiwa pumzi ya uhai ya manufaa yake kwa jamii pana...
Tuthubutu kufikiria tofauti!
Hmmmm