Madee: Ferouz alizingua kufanya chorus kwenye wimbo wangu

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
1,982
Reaction score
2,931
Kama kuna wimbo ambao madee anaupa heshima ya pekee ni wimbo wa Yote maisha aliomashirikisha Pfunk.
Wimbo huo anadai ulimtambulisha kwa mara ya pili na pia kumfanya watu waamini kuwa hakubahatisha baada ya kutambulishwa na wimbo wa kazi yake Mola.
Madee anasema ilikuwa 2006 mwishoni na kwamba ule wimbo ilitokea kwamba alikuwa amekwenda Bongo records kurekodi wimbo wake wa Cheza kidogo aliomshirikisha CP.
Baada ya kurekodi na kumaliza Pfunk akaweka beat, madee akaielewa sana Pfunk akamuuliza umeipenda, madee akakubari akamwambia basi chukua ukaiandikie ngoma.
Anadai kipindi hicho uliokuwa waweza pewa beat ukae nalo hata mwezi unaandika ngoma tu (huenda hii ndiyo ilikuwa sababu walikuwa wanaimba nyimbo zenye maana).
Baada ya muda akarudi studio akiwa ashaandika mashairi na kuanza kumchania Pfunk ambapo aliipenda akamwambia hii ngoma kwa jinsi ulivyoandika ina feeling za kusikitisha sasa hapa akae Ferouz kwenye chorus ambaye kipindi hicho alikuwa katisha sana kwa michorus.
Basi kutokana na kwamba Ferouz alikuwa chini ya Bongo records chini ya Boss Majani, Majani akamtafuta ila kila mara Ferouz akawa hatokei. Madee anasema hajui ni kwanini alikuwa anazingua japokuwa Pfunk alikuwa ni boss wake kwa maana Ferouz alikuwa chini ya Bongo records.
Pfunk alivyoona muda unakwenda akaamua atie Chorus na back Vocal mwenyewe maana alitokea kuifeel kwakuwa ilikuwa kwa namna moja ama nyingine inamgusa kutokana na kwamba kwa kipindi hicho alikuwa amekorofishana na mzazi mwenzie ambaye alikuwa bado anampenda Kajala Masanja.
Pfunk aliipendezesha ngoma huenda hata Ferouz asingeweza kufanya kile alichofanya majani humo ndani.
Ngoma ilikuwa hit sana na iliwagusa wengi na nina imani wengi mpaka leo wakiusikia huu wimbo unawarudisha enzi hizo za Bongo Records
 
Kila kitu hutokea kwa sababu flani yani bora ata Ferooz hakuwepo kwenye hiyo ngoma mana nahisi asingefanya vizuri akama alivyofanya Majani...

Yote ni ni Maisha ngoma bora kabisa ya muda wote kutoka kwa Madee Ally
 
Kazi yake Mola by Madee lile pini si mchezo!!...Hiyo nyimbo Yote Maisha utaiona nzuri ukiisikiliza huku umecatch feelings!. Zaidi ya hapo Kazi Yake Mola ni pini hasaa!!..
 
Madee nyimbo zake kali mbili tu:
1. Kazi yake Mola.
2. Yote Maisha.

Alipofiwa na Pendo akachanganyikiwa hadi leo anachoimba sikielewi.
 
Yote maisha nasikiliza kila siku na haichuji,inahamasisha kuzisaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…