Madee: Muziki wa hip hop bongo unapendwa na wahuni ambao hawawezi nunua kazi za wasanii

Madee: Muziki wa hip hop bongo unapendwa na wahuni ambao hawawezi nunua kazi za wasanii

Nimekumbuka miaka ya nyuma kuna mshikaji wangu alikuwa anataka kutoka kimuziki lakini alikuwa haimbi style ya hiphop sasa akaamua kumshirikisha msanii mmoja huyo msanii akamwambia kwenye mashairi yao waweke neno ganja ili kuwarusha masela, mshikaji akamwambia ata tukiitaja ganja kwenye mashairi yetu masela wenyewe hawatakuja kwenye show na hata wakija wataruka ukuta badala ya kulipa kiingilio.
 
Hakuna ukweli wowote huyo jamaa ajitambui...wenzie kina sugu umaarufu wao umeanzia kwenye mziki huo huo ananaosema ni wa kihuni na Leo hii wanawakilisha watu zaid ya million moja bungeni...wache yeye na mwenzie ney waendelee kujiita marais wa manzese.
Tukubali ukweli hapo Tanzania hiphop haiuzi.
 
Hajui anachozungumza uyu kiazi,utamaduni ni zaidi ya yeye anavyofikiria ndio maana tunasema wengi waki-rap wanajua ndio Hip Hop imeishia hapo na hawataki kujifunza wao wakivuta mibange,kutimua minywele na milegezo wanajikuta wanaishi kwenye huu utamaduni nyambafuuuuu hata Kitokololo wa Academia ana rap pia.
 
Hivi katika vyanzo vikubwa vinavyowaingizia wasanii wa Bongo hela, mauzo ya tapes/CDs yapo kweli? au dukani wanaenda kununua kazi gani?

Nadhani niliwahi kusikia wasanii wamegoma kuingiza albums sokoni. Walikuja kubadili msimamo, ama?
 
Wasanii wa kilingeni na Hip Hop yao ya kizamani wanatia huruma. Wachukue ushauri huu na waufanyie kazi
 
Madee kuwa mkweli. ..Media zinauwa hip hop bongo....hivi wewe Madee na Juma nature nani atajaza watu.makampuni yanadanganywa na watu"fulani"wasiopenda hip hop kuwanyima endorsement watu wa hip hop
 
Madee kuwa mkweli. ..Media zinauwa hip hop bongo....hivi wewe Madee na Juma nature nani atajaza watu.makampuni yanadanganywa na watu"fulani"wasiopenda hip hop kuwanyima endorsement watu wa hip hop
Nikuulize swali moja,
Nyumbani kwako una CD ngapi original za bongo rap ulizonunua?
 
Hakuna ukweli wowote huyo jamaa ajitambui...wenzie kina sugu umaarufu wao umeanzia kwenye mziki huo huo ananaosema ni wa kihuni na Leo hii wanawakilisha watu zaid ya million moja bungeni...wache yeye na mwenzie ney waendelee kujiita marais wa manzese.
madee ni kilaza sana
 
Nikuulize swali moja,
Nyumbani kwako una CD ngapi original za bongo rap ulizonunua?
Watanzania hatuna utamaduni wa kununua kazi za wasanii wetu iwe taarabu,dansi,bongo fleva,gospel au hip hop.Music wa sasa sio wa CD kina Diamond,Kiba,Yamoto Band lini walitoa CD?
 
Hivi katika vyanzo vikubwa vinavyowaingizia wasanii wa Bongo hela, mauzo ya tapes/CDs yapo kweli? au dukani wanaenda kununua kazi gani?

Nadhani niliwahi kusikia wasanii wamegoma kuingiza albums sokoni. Walikuja kubadili msimamo, ama?
Wasanii wengi siku hizi wamegoma kutoa album wamebaki Taarabu,dansi na gospel tu,mapato yao makubwa yanatokana na show wanazopata na wengi hupata show baada ya video muziki wao kuonekana kwenye TV au Youtube.Kenya wao wanatoa album na wanauza vizuri (King Kaka,Sauti Sol,Octopizo wametoa album hivi karibuni)
 
I'm sorry, hajaongelea umaarufu. Kaongelea mziki kulipa.
Soma vizuri, tafakari uelewe kabla hujani quote tena
ROMA,Prof J,FID Q hadi leo wanaimba Hip Hop ungekuwa haulipi wangekuwa wameshaacha
 
Lakini umewatoa muziki hao kina Sugu? Umaarufu sio pesa. Madee kachana ukweli usiopendeza lakini ni ukweli. Hip hop ina washabiki wengi lakini ni tabaka la wasio na pesa. Kimapato huwezi kuifananisha hata na taarab, kina Joh makini, bonta, fid nk wana nini?
Wasanii wengi hawana elimu ya kutosha na wanakosa management nzuri kuwasimamia kazi zao Prof J,ROMA ,FID Q bado wanafanya Hip Hop kumbuka Mr Nice,TID,MB Dogg ,Q Chief hawafanyi Hip Hop lakini wamechoka.Mfumo uliopo wasanii wengi wanaibiwa sana kazi zao wenzetu wakenya shule imewasaidia sana wasanii wao
 
hiphop ni msahafu kaka!!kanisani na msikitini ukweli unahubiriwa!!kamaisemavyo hiphop
 
Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection
Madee amefunguka na kueleza ni kwanini
wasanii wengi wa muziki wa Hip Hop nchini
wanashindwa kufanya vizuri licha ya nyimbo zao
kupendwa mitaani.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video
yake ya wimbo, Migulu Pande, ameiambia Times
Fm kuwa Hip Hop inapendwa na kundi la ‘wahuni’
wachache na machizi mtaani ambao ni ngumu
kwenda dukani kununua kazi anayoipenda.
Katika hatua nyingine, Mdee amesema kama
yeye angeendelea kudumu na staili yake ya
kurap kama zamani mpaka sasa, angekuwa
amekwisha potea kwenye ‘Game’ na ulimwengu
wa muziki.
“Watu wanataka changes, kama biashara
haikulipi kwanini uendelee kufanya inakuingizia
hasara kila kukicha, ningekuwa narap mpaka leo
nisingekuwepo kwenye game ningepotea, dunia
yenyewe inabadilika sasa kwa nini wewe
usibadilike” alisema Madee.
View attachment 348466

Daah Sasa Hip Hop nayo si mziki Kama miziki mingine , Kwa maana yake ni Kuwa Watu Waache kufanya Hip Hop na wote waimbe sasa Mbona diversity itakuwa hamna?
 
hii inaitwa factum probandum..... kama kuna mtu anammbishia madee aje na hoja sio viroja vya kusema malengo ya hiphop maana madee anazungumzia kulipa... kuanzia shows, deal za makampuni mbalimbali na vyanzo vingine vya pesa wasanii wa hiphop (bongo) wamekuwa nyuma sana .... na moja ya sababu ni kweli wengi wanaowasupport hawataki kugharamikia.... mfano tuwaweke prof j, sugu, nicky mmbishi na joh makini kwenye jukwaa moja halafu tukasema kiingilio ni 10000 huku upande wa pili tukasema Diamond na yamoto band waperform jukwaa moja kwa 30000.. watu watajaa sana huku kwa kina diamond hata kama kiingilio ni kirefu, upande wa pili wenye kiingilio cha elfu 10 kutahudhuriwa na watu wachache
 
Kwanza kabisa tambua Madee alikuwa haimbi Hip Hop bali alikuwa anarap kama wa fm academia tu...kwenye mafanikio
Unaukumbuka wimbo wa Nikusaidieje wa Prof J unajua ulimpa mafanikio gani? Kwanza unajua Mali za Joh Makini au kwakuwa hajitangazi??? Unatambua madee na nyimbo zake za mduara aimbe miaka buku hafikii utajiri wa Joh Makini achilia mbali Fid Q...
Hip hop sivyo anavyodhani yeye, mbona hao kina Mwana FA, ROMA, wanapiga hela na bado harakati zinaendelea??? Tatizo Babu Tale na Mkubwa na Wanae wanahitaji wabana pua ndio maana akabadili mfumo...
Wanaoimba wameshajifia kibaaaaao, wapo wapi hawa Mr Nice, TID, Mb Dog, Z Anton, Pingu na Deso n.k.... asikashifu kisa anabana pua moja Sasa hivi...Kwanza kwa mziki gani anaoimba haswa zaidi ya PUMBA TUPU
 
Back
Top Bottom