Madee: Ni ushamba kupiga mwizi

Madee: Ni ushamba kupiga mwizi

Hivi wale wanaoiba mabilion kwa matrilion wananchi wanaweza kuwafata

Ova
Sio kazi rahisi kwa sababu hakuna uthibitisho na Dola inawalinda sana. Lakini Wananchi (Mob)wanaangalia mwizi wa papo kwa hapo au Red handed. Na wanatoa hukumu ya papo hapo - hakuna longolongo. Ndani ya robo saa tu mchezo umeisha.
 
Kwenda hata ukiibiwa ñdo uue.
Bado hayajakukuta, nakumbuka siku moja alfajiri kabisa naikuta kesi sehemu mwanamama analia hajiwezi, vibaka wamemuotea wamemuibia pesa, simu na kila kitu, kibaya zaidi wamemkata kata na viwembe, maumivu ya viwembe hayahisi kilio chake ni zile hela, ni milioni na ushehe zilikuwa kwa ajili ya operation ya mama yake mzazi na mpaka kaipata hiyo hela ni kakopa kopa saana, atazitolea wapi, sipati picha yule mama akimoata mwizi atamtendea nini.

Nilikuwa nina pikipiki nyepe, haijafikisha hata wiki 3, wezi wakapita nayo,dogo anarudi hoi hana chombo, unadhani nikimkamata mwizi wa pikipiki nitamtemda nini?
 
asilimia kubwa wanaoua wezi hawana self control ndani yao ndo haohao wanapiga wake zao majumbani pindi wakiwa na hasira yaani swala la kujizuia kwao ni changamoto, mtu akisikia kelele za mwizi tu basi anatoka na silaha akaue huyo mwizi anaekimbizwa bila hata kujua kaiba kweli au anasingiziwa.kuna vifo vingi sana vya watu kuchomwa moto na hawakuwa wezi...sasa ukiletewa taarifa mtu muliyemuua mchana kama mwizi kumbe alisingiziwa tu utajisikiaje na amani ya kuishi kwa furaha huku unajua ulishiriki kukatisha uhai wa mtu tena asiye na hatia itatoka wapi.mimi binafsi siui mwizi hata kama kaiba kweli
 
Nimeiba sana samaki WA rangi kwa kuweka mdomoni halafu naenda kutema kwenye kweramu langu Enzi hizo

[emoji23][emoji23][emoji23]umenikumbusha enzi za kufuga magapi, tambala, kitenge, gold, zebra, na kwenda baharini kutafuta mapango
 
Kuna watu walisema hivyo hivyo ila yalipowakuta wao ndio washika vibiriti.
 
"Nilikuwa mafya ninja, nikikukuta na mazaga lazima nikombe" Haya ni moja ya maneno katika wimbo wake.
 
Sio kazi rahisi kwa sababu hakuna uthibitisho na Dola inawalinda sana. Lakini Wananchi (Mob)wanaangalia mwizi wa papo kwa hapo au Red handed. Na wanatoa hukumu ya papo hapo - hakuna longolongo. Ndani ya robo saa tu mchezo umeisha.
Na hao wezi,mafisadi,wanaoiba Mali pesa za umma wanaweza pia wakaibiwa na kuporwa fedha
Kimafia tu,ni kundi maalum lowepo liwafanyie umafia huo

Ova
 
Na hao wezi,mafisadi,wanaoiba Mali pesa za umma wanaweza pia wakaibiwa na kuporwa fedha
Kimafia tu,ni kundi maalum lowepo liwafanyie umafia huo

Ova
Kama nilivodokeza hapo; Hao Mafia watakuwa wanapambana na dola inayowalinda hao wezi, mafisadi na wanaoiba mali na pesa za umma kwa mwamvuli wa tuhuma za Kujichukulia Sheria mkononi. Kwani broo, kuna waliofikishwa mbele ya Mahakama ya mafisadi tangu ianzishwe?
 
Binadamu wa kawaida unamchoma vipi mwenzio moto? Ni ukatili tu, kuibiwa kisingizio.
 
Back
Top Bottom