Madee: Siamini katika ubaguzi wa rangi

Madee: Siamini katika ubaguzi wa rangi

RAKI BIG

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2020
Posts
394
Reaction score
456
Rais wa Manzese Madee Ali amesema kuwa haamini kwenye ubaguzi wa Rangi unaotajwa kuendelea Duniani na hata George Floyd inawezekana alikuwa mhalifu.

Madee amezungumza hayo kupitia kipinfi cha XXL cha *CloudsFm. Nikimnukuu Madee "Siamini kwenye ubaguzi wa rangi, hata yule jamaa aliyekatishwa uhai wake Marekani inawezekana alikuwa Mhalifu".


101547100_1947642355375799_7367728788097990656_o.jpg
 
Nina uhakika hukusikiliza XXL jana ww umekimbilia kufungua uzi tu hujui aliongea nn juu ya hiyo kauli lakini alikuwa amaanishi kama ww unavyoaminisha watu hapa loh usizungumzie kitu ambacho hukijui mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kifo cha mwangosi kimenigusa zaidi kuliko huyo floyd



Wewe unashindwa kuelewa, swala hili la kifo cha George Floyd limeamsha upya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi. Hata kama hukuguswa na kifo chake moja kwa moja, lakini jina lake linatumika na wapigania haki za watu weusi Duniani.
 
Kama kweli kazungumza na kumaanisha hiki ninachokiona, basi ni wazi kabisa huyo Madee ni kiazi kikuu.
 
kuwepo au kutokuwepo kwa ubaguzi wa rangi hakutegemei IMANI ya madee, by the way, hii inshu iko complex beyond his capacities, aendelee kutuburudisha kwa nyimbo tu basi, inshu nzito kama hizi ziko juu ya uwezo wake
 
Kwakweli uyu ni anafaa kuwa RAIS wa dogo janja na mkewe
 
  • Thanks
Reactions: amu
yeye yuko manzese, anamaana kwamba waandamani wote, kutoka miji yote mikubwa ya marekani ni wapuuzi, yeye anauelewa na ubaguzi kuliko wao,,,anamaanisha ikibidi waje kwake awape kozi juu ya ubaguzi wa rangi, huku ye yuko manzese wao wako frontline na ubaguzi wa rangi
 
Naungana na madee, pale kilichotokea ni askari kutokufata misingi ya kazi yake naamini angeweza kumfanyia hata mzungu mwenzie, bongo hapa kila siku watuhumiwa wanapigwa na maaskari na wengine tunaambiwa wamejinyonga wakiwa selo

Mimi binafsi naendelea kutaka kujua majibu huo ubaguzi pale ulikua wapi? Suala la askari kutofata misingi ya kazi ni tatizo sugu ambalo lipo nchi nyingi. Lakini kugeuzwa kuwa ni tukio la kibaguzi bado mim nashindwa kufahamu, au kwa kuwa mtenda alikua white na mtendewa alikua black ndio tayari ndio ubaguzi?
Hii dunia siku hizi ina mambo ya ajabu sana, watu wengi wanaishi kwa mihemko tu
 
Mimi binafsi naendelea kutaka kujua majibu huo ubaguzi pale ulikua wapi? Suala la askari kutofata misingi ya kazi ni tatizo sugu ambalo lipo nchi nyingi. Lakini kugeuzwa kuwa ni tukio la kibaguzi bado mim nashindwa kufahamu, au kwa kuwa mtenda alikua white na mtendewa alikua black ndio tayari ndio ubaguzi?
Hii dunia siku hizi ina mambo ya ajabu sana, watu wengi wanaishi kwa mihemko tu


Mkuu wewe hujui kitu, kaa hukohuko Manzese na Rais wenu Madee.
 
kwani huyu Rais alichaguliwa na na wananchi wa wapi?!!
 
Back
Top Bottom