PostGE2025 Madeleka: Deni la Taifa limefikia karibu Tsh. Trilioni 100, Miradi ya Kimkakati haionekani!

PostGE2025 Madeleka: Deni la Taifa limefikia karibu Tsh. Trilioni 100, Miradi ya Kimkakati haionekani!

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakili Peter Madeleka amesema anaona kuwa nchi inakopa kupita kiasi chini ya uongozi uliopo, huku akidai kuwa deni la taifa limefikia takribani trilioni 100 lakini hakuna ulinganifu wa miradi ya kimkakati inayoonekana kwa wananchi. Amedai kuwa licha ya mikopo hiyo, maisha ya wananchi bado ni magumu na huduma za msingi kama afya zimeendelea kudorora, akibainisha kuwa hospitalini mara nyingi hakuna dawa na hali ni ya kilio kila mara.

 
Wahuni siyo watu wazuri hata kidogo! Mtaani hali ya uchumi ni tete, na hakuna anayejali. Wananchi walio wengi wamekata tamaa! Wanaona kama vile serikali imewatelekeza! Chuki dhidi ya ccm na viongozi wake imeongezeka!

Nina imani ungefanyika uchaguzi huru na wa haki hata kesho halafu Tundu Lissu akagombea na kiongozi yeyote yule kutoka ccm, nina uhakika saa mbili tu asubuhi angetangazwa mshindi.
 
Wanakopa pesa nje kuwalipa watekaji. Ukiona watekaji wanakuwa na umiliki wa mali nyingi za gharama zisizoendana na mishahara yao ujue mikopo ndio inayowapa maisha ya anasa.
 
Back
Top Bottom