Mtangazaji (Rausath Sued):"Tumeona Rais amezindua tume ikachunguze wale waliohusika na yale matukio yaliyotokea tarehe 29. Kwa unavyona, hii tume iliyoundwa na Rais ni tume ya kijaji kama ilivyokuwa ikipendekezwa na tutakuwa tunatelekea sehemu nzuri ya kuweza kuiponya taifa?"
Peter Madeleka:"Kilinachosumbua wengi hapa tangu mwanzo, hii tume inadhahiri kweli ya kuja kutatua tatizo ambalo lilitokea? Hiyo ndiyo dhamira iliyopo kwa mazingira ambayo nchi imefikia. Kwa sababu inawezekana Rais Samia anadhahiri njema sana, anatamani Tanzania... yaani kwa kumwangalia atamani Tanzania itoke hapa ilipo. Lakini dhamira inabaki moyoni na inatakiwa ionekane kwa matendo. Yaani matendo ndiyo yanaweza yakasema zaidi kwamba ah, bwana yule fulani anadhahiri ya kweli.
Sasa hivi tunasema waende wakachunguze wale waliochochea na wale waliofadhili, yaani adhabu za sheria ni mbili: waliochochea na waliofadhili. Walioua je? Kikweli kuna watu waliuawa, na Jaji Mkuu amesema kabisa wazi hata kama alikosea kutamka, ninajua kesi ya mtu wa Lilla alijumlisha zile namba akasema ni 518. Lakini ukisumbusha kihalisia, ni 2518. Lakini bahati nzuri alisema ile idadi inaweza ikaongezeka mara duafu. Kwa hiyo tunakubaliana kwamba watu waliuawa.
Hao watu waliouawa watachunguzwa na tume gani? Au kikimaliza hii tume ya kijaji ya kuchunguza waliochochea na waliofadhili, tutakuja kuunda tume nyingine sasa ya walioua? Kwa sababu ni jambo ambalo unajiuliza, unawezaje sasa kuwapata watu na ukawahukumu kwa kuchochea halafu usituonyeshe waliochochewa ni nani? Maana lazima aliyechochewa sasa na yeye tumjue. Tukishamjua baada ya kuchochewa atuambie alichukua hatua gani. Kwa hiyo lazima atakuwepo mtu atakayesema 'mimi bwana, Juma Abdallah, nilichochewa na Hamisi Jumanne niende nikachukue bunduki nikamwue MTI ambaye ndiyo MTI alisema waliua. Kwa hiyo mimi ndiyo nilipaua, lakini sikua hivi hivi, nilichochewa.'
Kwa hiyo mimi naasi Watanzania, kama Rais alivyosema, tusiisumbue hii tume. Kwamba tuiache ifanye kazi yake. Kuiacha tume ifanye kazi yake ni sawa, lakini tume ije ituambie pia watu waliochochewa ni kina nani. Kama tume haitakuja na majina ya watu waliochochewa, watu waliochochea hawawezi kuwa na msaada wowote katika jitihada hizi za kutatua huu mkwamo tulionao, kwa sababu sasa watu watakuwa walimchochea nani?"
Pia soma: Rais Samia: Tumeamua kuwashirikisha wenzetu kutoka Uganda na Namibia kupata muono mpana. Tume inakwenda kutafuta nani walichochea, waliotoa fedha