Pre GE2025 Madeleka: Kama Lissu hafai, CHADEMA haifai kuaminiwa pia

Pre GE2025 Madeleka: Kama Lissu hafai, CHADEMA haifai kuaminiwa pia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
"Unaposema leo kuwa Lissu hafai, mtu mliyemuamini nyinyi (CHADEMA) wenyewe, kama Lissu hafai basi CHADEMA haifai. Kama Tundu Lissu wanamuona hafai kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, CHADEMA haifai kuendelea kuaminiwa na Watanzania"

Soma, Pia:

Tundu Lissu achukua rasmi Fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA

Tundu Lissu: Haikuwa rahisi kwangu kuamua kugombea Uenyekiti

CHADEMA watoa tamko zito, John Mnyika aanika gharama za fomu za kugombea na kutoa mwongozo
 
"Unaposema leo kuwa Lissu hafai, mtu mliyemuamini nyinyi (CHADEMA) wenyewe..kama Lissu hafai basi CHADEMA haifai. Kama Tundu Lissu wanamuona hafai kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, CHADEMA haifai kuendelea kuaminiwa na Watanzania"
Kuhusu Lissu hahitaji kupigiwa Kampeni.....yeye mwenyewe ni Ushahidi wa kutosha
 
"Unaposema leo kuwa Lissu hafai, mtu mliyemuamini nyinyi (CHADEMA) wenyewe..kama Lissu hafai basi CHADEMA haifai. Kama Tundu Lissu wanamuona hafai kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, CHADEMA haifai kuendelea kuaminiwa na Watanzania"
Ni wapi Madeleka amesema hivyo? Dunia hii bado unataka kuwalisha watu upotoshaji usio na kichwa wala miguu? Weka clip kuondoa shaka ya huu upotoshaji wako.
 
CHADEMA ni zaidi ya Lissu.

Lissu sio mtu pekee aliyepata fursa ya kugombea urais kupitia CHADEMA, Mbowe, Slaa na Lowassa pia walipata fursa hiyo; cha ajabu nini?

Lissu siyo standard gauge ya kutumika kupima mtu kama anafaa su hafai.

Kuaminiwq kwa CHADEMA hakufungamanishwi na kufaa kwa Lissu.
 
Ni wapi Madeleka amesema hivyo? Dunia hii bado unataka kuwalisha watu upotoshaji usio na kichwa wala miguu? Weka clip kuondoa shaka ya huu upotoshaji wako.
image.jpeg
 
"Unaposema leo kuwa Lissu hafai, mtu mliyemuamini nyinyi (CHADEMA) wenyewe, kama Lissu hafai basi CHADEMA haifai. Kama Tundu Lissu wanamuona hafai kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, CHADEMA haifai kuendelea kuaminiwa na Watanzania"
View attachment 3187267
nadhani madeleka ndiyo hafai zaidi,
alimtelekeza kijana wa kuingizwa chupa kule babati hivi hivi kwa mdomo, makelele na mbwembwe 🐒k
 
"Unaposema leo kuwa Lissu hafai, mtu mliyemuamini nyinyi (CHADEMA) wenyewe, kama Lissu hafai basi CHADEMA haifai. Kama Tundu Lissu wanamuona hafai kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, CHADEMA haifai kuendelea kuaminiwa na Watanzania"
View attachment 3187267
Soma, Pia:

Tundu Lissu achukua rasmi Fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA

Tundu Lissu: Haikuwa rahisi kwangu kuamua kugombea Uenyekiti

CHADEMA watoa tamko zito, John Mnyika aanika gharama za fomu za kugombea na kutoa mwongozo
Propaganda za kitt za chawa wa mbowe
 
Katika muktadha wa uchaguzi wa mwenyekiti wa Chadema Taifa, wajumbe wa mkutano mkuu wanakabiliwa na maamuzi muhimu yanayoweza kuathiri mustakabali wa chama hiki. Hivi karibuni, kumekuwa na mjadala mzito kuhusu aina ya kiongozi anayefaa kuongoza chama katika kipindi hiki cha changamoto. Wajumbe wanahitaji mgombea ambaye ni mwasiasa, si mwanaharakati, ili kuweza kuimarisha siasa za chama na kukabiliana na matatizo ya kisiasa yanayolikabili taifa.

Wakati wa uchaguzi huu, ni muhimu kuelewa tofauti kati ya mwanasiasa na mwanaharakati. Mwanasiasa anajitahidi kutafuta mbinu na mikakati ya kisiasa inayoweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii, huku akitafuta njia za kushirikiana na wadau mbalimbali katika uwanja wa siasa. Kwa upande mwingine, mwanaharakati anajikita zaidi katika harakati za ukombozi, akilenga kuleta mabadiliko kupitia mapambano ya moja kwa moja dhidi ya mfumo uliopo. Hii ni tofauti kubwa ambayo wajumbe wa mkutano wanapaswa kuzingatia katika uchaguzi wao.

Tukichunguza majina mawili yanayojitokeza katika uchaguzi huu, Tundu Lissu na Freeman Mbowe, ni wazi kwamba kila mmoja anawakilisha aina tofauti ya uongozi. Lissu amejijengea sifa ya kuwa mwanaharakati mwenye msimamo thabiti katika masuala ya haki za binadamu na demokrasia. Hata hivyo, siasa za mwanaharakati mara nyingi zinaweza kuonekana kama za kukabiliana na mfumo, badala ya kujaribu kuujenga na kuuboresha. Wakati huu, wanachama wa Chadema wanahitaji mtu ambaye anaweza kuhamasisha umoja na ushirikiano, si mtu anayepigana vita vya kisiasa pekee.

Katika upande wa Mbowe, yeye anajulikana kama mwanasiasa mwenye uzoefu wa muda mrefu katika siasa za Tanzania. Mbowe anajua jinsi ya kuendesha siasa na kuujenga chama katika mazingira magumu. Kuweka kando tofauti za kisiasa, Mbowe anaweza kuwa kiongozi ambaye anaweza kuleta umoja na kuelekeza chama katika njia sahihi ya kisiasa. Katika wakati wa mgawanyiko na changamoto za kisiasa, ni muhimu kuwa na kiongozi ambaye anaweza kuleta ushirikiano na kuelekeza juhudi za chama katika kujenga mustakabali bora.

Wajumbe wa mkutano mkuu wanapaswa kuelewa kwamba wakati huu wa uchaguzi, siasa zinazohitajika ni zile zinazoweza kuleta maendeleo kwa chama na kwa jamii nzima. Wanachama wanahitaji siasa zinazoweza kuleta mafanikio na siasa ambazo zinaweza kuimarisha ushawishi wa chama katika jamii. Kiongozi anayejikita katika siasa atakuwa na uwezo wa kujenga na kudumisha uhusiano mzuri na wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na jamii kwa ujumla.

Aidha, ni muhimu kufahamu kwamba siasa si tu kuhusu kushinda uchaguzi, bali pia ni kuhusu kujenga mazingira bora ya kuishi na kufanya kazi. Wanachama wanahitaji kiongozi ambaye ataweza kuangalia maslahi ya chama kwa ujumla, badala ya kujikita katika masuala binafsi au ya kikundi fulani. Mbowe, akiwa na uzoefu wa kisiasa, anaweza kuwa na uwezo wa kujenga mazingira hayo na kuimarisha nafasi ya chama katika siasa za nchi.

Katika hali hii, wajumbe wa mkutano wanapaswa kuzingatia umuhimu wa kuwa na kiongozi ambaye ataweza kuhimiza siasa za maendeleo, badala ya siasa za ukombozi pekee. Wanachama wanahitaji mtu ambaye ataweza kubuni mikakati ya kisiasa itakayowezesha chama kuendelea kuwa na mvuto katika jamii na kuongeza ushawishi wake katika masuala ya kitaifa. Hii itasaidia Chadema kuwa na nafasi imara katika siasa za Tanzania na kuweza kushiriki katika maamuzi yanayohusu mustakabali wa nchi.

Kwa kumalizia, wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema wanahitaji kufikiria kwa makini kuhusu uchaguzi wa mwenyekiti. Wanahitaji kiongozi ambaye ni mwasiasa, sio mwanaharakati, ili kuweza kuimarisha siasa za chama na kukabiliana na changamoto za kisiasa.

Wakati huu, Mbowe anaonekana kuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya na kujenga umoja katika chama, wakati Lissu anahitaji kuzingatia zaidi harakati za ukombozi. Chaguo sahihi litasaidia Chadema kuendelea kuimarika na kuwa na sauti yenye nguvu katika siasa za Tanzania.
 
Poor perception kwahiyo mtu mmoja asipofaa chama chenye wanachama zaidi ya elf 10 wote hawafai, kama hii ni conclusion ya msomi basi na yeye hafai kuitwa wakili msomi.
 
Back
Top Bottom