Wakili Peter Madeleka anaeleza kuwa kwa misingi ya kisheria kama Alute Mughwai Lissu(kaka wa Tundu Lissu) angetakiwa kuzikwa kabla ya Novemba 6, 2026 basi Lissu angeshindwa kuhudhuria mazishi hayo.
Madeleka akizungumza kwenye kipindi cha Jambo TV leo Novemba 2, 2026 ameeleza kuwa kesi inayomkabili Lissu ya uhaini haina dhamana hivyo pia anakosa nafuu zingine kama kuwa nje.
Hata hivyo ameeleza kuwa ndiyo sababu ya familia ya Lissu imepanga kufanya mazishi baada ya Novemba 6, 2026 siku ambayo hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Lissu inatoka.