Madeleka: Paul Chacha ana kesi ya kujibu kuhusu dada aliyemtongoza, ametoa taarifa bila ridhaa

Madeleka: Paul Chacha ana kesi ya kujibu kuhusu dada aliyemtongoza, ametoa taarifa bila ridhaa

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Wakili Peter Madeleka amesema anafunga safari kuelekea Tabora kwa ajili ya kusimamia kesi ya mwanamke aitwaye Sophia ambaye anatuhumiwa kumtongoza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha, ambaye aliteuliwa Katibu wa Oganaizesheni Ya CCM.

SOPHIA.webp

Taarifa hizo zimeibuka kufuatia mahojiano maalum yaliyosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, ambapo Wakili Madeleka ameweka wazi msimamo wake wa kisheria huku akipinga vikali hatua yoyote ya kisheria inayoweza kuchukuliwa dhidi ya mwanamke huyo.

Soma>> Madeleka: Nitakwenda Tabora kumtetea Sophia, kumtongoza Mkuu wa Mkoa siyo Jinai

Kwa muujibu wa Madeleka amesema hilo sio kosa bali Paul Chacha ndiye mwenye kosa la kutoa taarifa binafsi za mtu bila ridhaa yake.

Wakili huyo amesisitiza kuwa hisia za kibinadamu au jaribio la kutongoza haviwezi kuhesabiwa kama utaratibu wa kijinai unaostahili kumkamata au kumkushtaki raia.

Wakili huyo amebainisha kuwa hatua ya kiongozi huyo kutoa, kusambaza, au kuweka wazi taarifa na mawasiliano binafsi ya mwanamke huyo bila ridhaa yake ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za ulinzi wa taarifa binafsi (Data Protection) na haki ya faragha inayolindwa na Katiba ya Nchi.

Tukio hili limeendelea kuibua mjadala mzito kati ya wanasheria, wanaharakati, na wananchi kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakiohoji mipaka ya maadili ya viongozi, ulinzi wa faragha za raia, na matumizi sahihi ya vyombo vya dola katika mambo binafsi.
 
kuna ile Mitongozo ya
siiiii........ watongwozwaji wakiisikia tu wamesha geuka, ila kama unajielewa huna mda wa kugeuka!
 
Back
Top Bottom