Madeleka: Polisi wanaotekeleza maagizo yasiyo ya kisheria ni wahalifu hata kama wana magwanda na manyota

Madeleka: Polisi wanaotekeleza maagizo yasiyo ya kisheria ni wahalifu hata kama wana magwanda na manyota

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakili Peter Madeleka amesema kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na maofisa wote wa Jeshi la Polisi wanapaswa kutekeleza Katiba na sheria za nchi, badala ya kufuata maelekezo ya viongozi ambayo hayana msingi wa kisheria.

"Kile ambacho IGP au ofisa yeyote wa Jeshi la Polisi anapaswa kukitii ni katiba na sheria. Sio maelekezo ya waziri ambayo hayatokani na sheria."

"Yaani ukimwona mtendaji yeyote wa Jeshi la Polisi kainuka anatekeleza jambo fulani hivi kama sehemu ya wajibu wake, iwe hilo jambo limetamkwa na waziri au halijatamkwa, ujue huyo mtu atakuwa anatekeleza matakwa ya katiba au matakwa ya sheria. Sasa kama atakuwa anafanya hilo jambo alafu liko kinyume na sheria, hata kama angekuwa anavaa magwanda na manyota kila kitu mabegani, huyo mtu anakuwa anavunja sheria na anakuwa anavunja katiba, na anakuwa ni mhalifu tu kama walivyo wahalifu wengine."

 
CCM NI WAPUMBAVU SANA MKUU, LAKINI NITAKUJIBU KWA KIFUPI ANAEVUNJA UTULIVU/AMANI NI....

1. Anayeteka watanzania Wenzetu akina Soka, Polepole, Mdude, Chaula nk.

2. Anayepiga watu Risasi Akina TUNDU LISSU, SATIVA AKWILINA MAWAZO NK

3. Anayezuia haki ya Kikatiba ya Mikitano ya Vyama vya siasa.
(Kushiriki mikutano ya hadhara na Mikutano ya ndani.

4. Anayezuia Maandamano ambayo ni haki ya kikatiba ya Tanzania.

5. Anayezuia na Kupora Haki ya watanganyika ya kuchagua kiongozi wanaye mtaka.

6.Anayeficha Kila aina ya mikataba, Bandari, Ardhi, Dhahabu, Gesi nk.

7. Anayekandamiza uhuru wa vyombo vya Habari

CCM WAMETUONA WATANGANYIKA NI MALOFA SANA


AMKENI WATANGANYIKA.
 
Screenshot_20260616-173300~2.png
 
Ogopa sana mtu ambaye anakakamaa kukaza matako na kubana Miguu kama yupo parade akiskia nyimbo za sisiem.

Umeme Mdogo vichwani.
 
Back
Top Bottom