Madeleka: Si kosa wakili kuongea na wanahabari mahakamani

Madeleka: Si kosa wakili kuongea na wanahabari mahakamani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakili Peter Madeleka amesema si kosa la kimaadili au la jinai kwa mtu yeyote, wakiwemo mawakili, kuongea na vyombo vya habari kwenye viunga vya mahakama baada ya ahirisho la kesi.

Mahakama kuu ya Tanzania iliwakumbusha mawakili wote wanaohudhuria mashauri mahakamani kuzingatia na kuheshimu maelekezo ya chama cha wanasheria tanganyika (TLS) pamoja na maelekezo ya mahakama, kwa lengo la kuhakikisha mwenendo wa mashauri unafanyika kwa ufanisi, heshima na kwa kuzingatia misingi ya haki.

Soma: Mahakama Kuu: Marufuku Mawakili kuongea na Vyombo vya Habari nje ya Mahakama baada ya mashauri kuahirishwa

Kauli hiyo imetolewa kwa kuzingatia matakwa ya kanuni ya 137 ya kanuni za maadili ya mawakili na ibara ya 30 (1) (2) (d) ya katiba ya jamhuri ya muungano waTanzania.

Soma: Dkt. Nshala: Mawakili kuzuiwa kutoa muhtasari kwa waandishi ndani ya viunga vya mahakama si sawa, TLS ichukue hatua
 
Back
Top Bottom