Wakili Peter Madeleka amesema si kosa la kimaadili au la jinai kwa mtu yeyote, wakiwemo mawakili, kuongea na vyombo vya habari kwenye viunga vya mahakama baada ya ahirisho la kesi.
Mahakama kuu ya Tanzania iliwakumbusha mawakili wote wanaohudhuria mashauri mahakamani kuzingatia na kuheshimu maelekezo ya chama cha wanasheria tanganyika (TLS) pamoja na maelekezo ya mahakama, kwa lengo la kuhakikisha mwenendo wa mashauri unafanyika kwa ufanisi, heshima na kwa kuzingatia misingi ya haki.
Kauli hiyo imetolewa kwa kuzingatia matakwa ya kanuni ya 137 ya kanuni za maadili ya mawakili na ibara ya 30 (1) (2) (d) ya katiba ya jamhuri ya muungano waTanzania.