Madeleka: Swala la jinai haliitaji Tume ya Rais, sitegemei lolote jipya kwenye Tume ya Jaji Lila

Madeleka: Swala la jinai haliitaji Tume ya Rais, sitegemei lolote jipya kwenye Tume ya Jaji Lila

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079


Mahojiano ya Wakili Peter Madeleka, yaliyorushwa na SAUT Digital Agosti 9, 2026
eo:

Madeleka: Kitakachokwenda kupatikana kwenye tume hii ni ripoti. Ripoti ambayo ni mali ya Rais. Mali ya Rais ambayo hawajibikii kuitoa adharani kama alivyofanya kwenye Tume ya Jaji Jishande.

Sasa sitegemee lolote mimi mpya kwenye Tume hii kwa sababu ni Tume ya Rais. Inaenda kumwandalia ripoti, na hiyo ripoti atakabidhiwa Rais na halazimishwi na mtu yeyote kuitoa adharani.

Laiti tungeacha vyombo vya kikatiba na kisheria ambavyo vimepewa mamlaka siku zote na wakati wote kushughulika na jinai, vingenda kupeleleza tingepata ushahidi. Na ushahidi huo hupelekwi kwa Rais, unapelekwa mahakamani.

Kwa hiyo mimi naona haya mambo ya kuunda tume, kuunda tume, kuunda tume ni kupotezeana muda tu. Kupotezeana muda, lakini pamoja na kwamba tume imeundwa kwa mujibu wa sheria, mimi sioni kabisa kwamba kile ambacho kinatakiwa kufanyika kinapaswa kufanyiwa na tume hii. Kwa hiyo nadhani utakuwa umenipata vizuri.

Madeleka: Lekini hivi karibuni kulikuwa na wito ambao unatolewa kwa Mheshimiwa Rais ukieleza ya kwamba ipatikane tume ambayo itakuwa ni tume huru na itakuwa na taswira ya kimataifa. Rais ametimiza hilo, changamoto unayoiona hapa ni ipi ambayo mbeleni pengine inaweza ikaleta mgawanyiko mwingine?

Madeleka: Mimi changamoto ninayoiona hapa ni kwamba swala la jinai halitaji tume ya Rais. Swala la jinai, kwa mfano mtu anaiba kuku, mtu akiiba kuku tunahitaji Mheshimiwa Rais aunde tume? Iwe ni ya kimataifa au ni tume ya ndani? Si Polisi ambao ni chombo kilichopewa mamlaka wakati wote kushughulika na wizi wa kuku kinaingia barabarani kinawatafuta walioiba kuku lakini na kufikisha katika mkono wa sheria kama ambavyo sheria inaelekeza?

Kwa nini tunakubaliana kwamba kuna watu wameuliwa tarehe 29 Oktoba 2025 na siku chache baada ya hapo? Kama tunakubaliana hivyo, kwa nini tunang'ang'ania kuunda tume alafu wajibu huo hutaki kuuelekeza kwenye Jeshi la Polisi?

Kwa hiyo mimi ninachosema ni kwamba, tume itakayoundwa na Rais, iwe ni ya kimataifa au iwe ni tume ya kawaida kutokana na watu wanavyozungumza, hiyo haiondoi ukweli kwamba jinai yoyote, tena mahususi jinai ya mauaji, inatakiwa ifanywe na Jeshi la Polisi na vyombo vingine kama Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambavyo kwenye katiba vimepewa mamlaka ya kushtaki watu mahakamani.

Kwa hiyo mimi naiona changamoto ni kwamba tume, na sio ya kwanza hii Tume ambayo imeundwa na Rais Samia, hii Tume itaenda kutuletea ripoti. Na hiyo ripoti haitakuwa ni mali ya wananchi, na hiyo ripoti haipelekwi mahakamani, hiyo ripoti anapewa Rais.

Sasa kama ripoti atapewa Rais, watu wengine hawajui kama vile ambavyo ripoti ya Jaji Jishande amekabidhiwa Rais, swala la kutafuta na kuwajua walioua litajulikana lini sasa? Kama tunaacha tu kwamba swala hili lishughulikiwe na Tume badala ya kushughulikiwa na vyombo vya kawaida ambavyo vimepewa mamlaka ya kushughulika na jinai, ndio mimi naona changamoto ipo hapo.

Mwandishi: Ni kwa namna gani ambavyo sasa unafikiri kwamba tunaweza tukapata chombo ama ikapatikana hoja ama hatua za kutuondoa hawapa tulipo kama taifa? Nini ambacho unafikiri kinatakiwa kifanyike?

Madeleka: Mimi navihesabia vyombo vya dola ambavyo vimepewa mamlaka ya kutekeleza jukumu hilo, hata kama jukumu hilo linaweza likatiliwa shaka namna gani, lakini wakati wote ndio uzoefu unaonyesha kwamba inapotokea mauaji, mwenye mamlaka ya kupeleleza jinai na kupeleka ushahidi mahakamani ni Jeshi la Polisi ndio linaenda kutoa ushahidi. Hii Tume ya Jaji Lilla na majaji kutoka Uganda na Namibia haiwezi kwenda kutoa ushahidi mahakamani.
 
Back
Top Bottom