Madeleka: Ugaidi ni makosa yanayotumiwa kuwaumiza watu

Madeleka: Ugaidi ni makosa yanayotumiwa kuwaumiza watu

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

"Mimi pia maneno yale, nilikuwa wakili wa kwanza kufanya kesi ya ugaidi mahakamani kuwatetea watu, mashehe wa Arusha, waliokaa gerezani kwa miaka tisa. Halafu baadaye mahakama ikathibitisha haukuwa ugaidi. Kwa hiyo haya ni makosa ambayo yanatumiwa kuwaumiza watu, na sijui kwa faida ya nani kwa sababu nimejaribu kusoma sheria ya ugaidi, nimejaribu kufuatilia hizi kesi, nimejaribu kuzisimamia nikiwa mahakamani, halafu nimejaribu kulinganisha sasa hivi tunapata faida gani za kiuchumi kwenye kusema uongo kuhusu ugaidi au uhaini, sijawahi kuona faida hata moja. Hata moja sijawahi kuona.

Ndio maana nasema, kama wanaozungumzia ugaidi wanadhani ni jambo la mzaha mzaha hivi, nadhani hawajui analopeleka taifa mahala pabaya. Afghanistan hakuna Wizara ya Utalii. Hakuna mtalii anayeweza kwenda kufanya utalii Afghanistan. Hakuna mtu anayeweza kwenda kuwekeza kiwanda cha gesi kule Somalia kwa sababu hakuna usalama. Kwa hiyo unapoendelea kuhubiri ugaidi, ugaidi, ugaidi ukazani unamkomoa sijui Lissu au unamkomoa sijui nani, humkomoi Lissu wala humkomoi nani, unakomoa taifa zima ikiwemo wewe mwenyewe na kizazi chako.

Kwa hiyo mimi wito wangu nadhani watu wangetakiwa waache kulitumia hili neno ugaidi, si neno zuri sana na watu wakishalizoea hata siku ukija kutokea ugaidi wenyewe tunaweza tukawa mahala pabaya kwa sababu watu watakuwa walishazoea. Kama tuna tofauti zetu zingine ziwe za kisiasa ama za kijamii, tupambane na tutafute njia nyingine ya kumaliza hizo tofauti pasipo kutumia mamlaka, tena kwa mfano Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, kuwa unawashtaki watu kwa uongo. Ni aibu kwa mtu kuwa na mamlaka makubwa yanayoweza kuamua na kuathiri hisia za watu kuwa muongo muongo. Wanapeleka kesi mahakamani, kesho kutwa wanasema sina tena nia ya kushtaki. Kwa mfano kesi ya Mbowe, tulihakikishiwa kabisa Mbowe ni gaidi. Yaani kwamba Mbowe na Osama, pale unavyomwona Mbowe na Osama, la pili alafu kesho yake Mbowe anaachiwa, anaenda Ikulu anapiga picha, wanakunywa chai. Sasa ugaidi gani wa hivyo?

Lkn kuna mtu ana mamlaka akatumia mamlaka yake kumshtaki. Hata hivi karibuni tunaambiwa ni muhaini. Muhaini ambaye anaweza kufanya uhaini peke yake, hakunaga uhaini wa mtu mmoja duniani. Kote kule ambako uhaini umefanyika utakuta jeshi, sehemu ya wanajeshi wasio watii walishiriki na watu wengine na nini. Kwa sababu lengo la uhaini ni kupindua serikali, ukipindua serikali maanake unataka wewe ndio uunde serikali kwa njia zisizo halali. Sasa serikali ni kubwa mno, hakuna serikali ya mtu mmoja duniani. Kwa hiyo unagundua ni uongo, wito wangu pia kwamba watu waache kutumia mamlaka yao vibaya na watu waache kuwa waongo waongo. Ni aibu kwa sababu mambo yanabaki yanakuwa sehemu ya historia."
 

"Mimi pia maneno yale, nilikuwa wakili wa kwanza kufanya kesi ya ugaidi mahakamani kuwatetea watu, mashehe wa Arusha, waake unataka wewe ndio uunde serikali kwa njia zisizo halali. Sasa serikali ni kubwa mno, hakuna serikali ya mtu mmoja duniani. Kwa hiyo unagundua ni uongo, wito wangu pia kwamba watu waache kutumia mamlaka yao vibaya na watu waache kuwa waongo waongo. Ni aibu kwa sababu mambo yanabaki yanakuwa sehemu ya historia."
Wakati Mkapa anaanzisha sheria hii ya Ugaidi wengi mlipiga kimya kwa kuwa tu walengwa walikuwa ni waislam pekee. Ilikuwa ukitaja gaidi tu moja kwa moja watu wanajua huyo ni Muislam. Lakini sasa tumeanza kushuhudia hata wagalatia nao wanasweka ndani kwa kutuhumiwa ugaidi basi kelele zimekuwa nyiiiingi.

Ni kama kipindi cha lile shetani la Chato lilipokuwa linateka, linauwa na kuharibu uchaguzi akina Etwege Idugunde and the like walivyokuwa wanashangilia. Baada ya kuona kuna hata kina Polepole wanakula kibano sasa wameenda mpk na chuo cha matusi
 
Back
Top Bottom