Madeleka: Watu wanaomzunguka Rais wanamuhujumu, tumeomba AFCON ifanyike hapa halafu mtu anasema kuna ugaidi!

Madeleka: Watu wanaomzunguka Rais wanamuhujumu, tumeomba AFCON ifanyike hapa halafu mtu anasema kuna ugaidi!

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakili Peter Madeleka, amewashutumu baadhi ya wasaidizi na watu waliopo pembeni mwa Rais kwa kumhujumu kiongozi huyo wa nchi na kuingiza taifa kwenye hatari.

Soma: Heche: Tutawaandikia barua FIFA na CAF kuwaeleza Serikali imesema kuna 'Ugaidi' wasilete Watu AFCON

Madeleka amebainisha kuwa wakati Rais anatumia mabilioni ya fedha kupitia filamu ya Royal Tour na uwekezaji wa miundombinu ya AFCON kuitangaza Tanzania kama nchi salama kwa utalii na uwekezaji, kuna baadhi ya viongozi na vyombo vya sheria vinavyounda mashitaka ya uongo ya 'ugaidi' na 'uhaini' dhidi ya raia.

 
Hakuna anayemuhujumu huyo raisi...

Haya mambo ya ugaidi mimi naamini ni mipango yake...
 
Back
Top Bottom