Wakili Peter Madeleka, amewashutumu baadhi ya wasaidizi na watu waliopo pembeni mwa Rais kwa kumhujumu kiongozi huyo wa nchi na kuingiza taifa kwenye hatari.
Madeleka amebainisha kuwa wakati Rais anatumia mabilioni ya fedha kupitia filamu ya Royal Tour na uwekezaji wa miundombinu ya AFCON kuitangaza Tanzania kama nchi salama kwa utalii na uwekezaji, kuna baadhi ya viongozi na vyombo vya sheria vinavyounda mashitaka ya uongo ya 'ugaidi' na 'uhaini' dhidi ya raia.