Mademu wananikimbia kisa ubahili wangu.

Mademu wananikimbia kisa ubahili wangu.

Tuko wengi broo. Na hata mkinisaliti nitabaki pekee kwenye hiki chama(cha wanaume wasiohonga). Mana kuna kipindi nilijifanya pochi nene nikaja gundua kama pesa zote nilizowahi kuhonga ningekuwa nazijengea nyumba ningekuwa npo napauwa afu zile za vocha ningefanyia finishing .

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hiyo ni hela za vitabuni,ukienda field itakua tofauti.
 
Hata kama sina ghorofa ila nakuwa na utulivu wa maisha,hela yangu naiona na naifanyia kile ninachotamani tofauti na anayehonga honga hovyo.

Hivi mkuu ulishawahi kupigwa asubuhi asubuhi na ile “Naomba nipe 80K nikachukue simu yangu kwa fundi”,na juzi yake mama yako sijui baba yako alikuomba elf20 tu ya Kg 2 za sukari ukamwambia “mama huku hali mbaya sana nitakutumia mwezi ujao nikipata” ila kwa huyu haraka sana utamtumia shida usiweke ya kutolea lazima akuulize mbona hujaweka ya kutolea?asishukuru bado anakulaumu but i swear mama yako ungemtumia hata 10K na usiweke ya kutolea bado angeku-beep akushukuru na akubariki kwa kile kidogo ulichompa.

Ipo siku utanielewa,funguo za mafanikio yako unazo wewe ila baada ya Mungu wapo wazazi wako watakaokuombea ili ukifikie kitasa sahihi cha mafanikio yako na ukiwatupa nao wanakutupa.mimi ni shuhuda,nilipoanza kujizoesha kumpa mama chochote nilicho nacho hata kama nilikuwa nakiona kidogo ndivyo nilivyozidi kuchanua,pale juu niliandika nikiwa najua.huwezi ukampa mtu hela tena bure hajafanya kazi yoyote halafu ashindwe kukushukuru aanze tena kukulaumu hapo hakuna baraka huyo ni jini mnyonyaji stuka tafuta mke owa hela zako wazile na wazifurahie wale wanaokuombea heri.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Daaaa. Maneno yako yanaumiza. Wewe ni mchungaji?
 
Nawaasa mabaharia wenzangu kwa hili. Nimekuja kubaini kwamba pisi zinaamuaga kunipotezea kisa sio mhongaji mzuri. Kutokana na muonekano wangu wa nje mademu wanajuaga ni mhongaji kumbe wapi,mimi nikizidisha sana demu nampa elfu kumi ila mara nyingi buku tano. Wengi nikitongoza wanaanza vizinga huwa nawaambia mpaka siku tukionana na upande wa nauli nawaambia wakope nitarudisha. Sasa kila nikipata demu akiniomba mpunga mara mbili tatu akiona nimemkazia ananifungia vioo. Sasa najiuliza hivi siku hizi hakuna real love? Demu nimemtongoza mchana jioni matatizo kibao. Sawa nitatoa lkn sasa napanda damu mpaka 15,000/= maana nimejifunza sasa ila mziki wake sio wa kipolepole,nitalipiza.
Only kid value fairness, adult value interest
 
Back
Top Bottom